Mabilionea nane wanamiliki mali sawa na nusu ya watu duniani

sylvertical

Member
Dec 29, 2016
15
9
Mabilionea wanane wanamiliki mali sawa na nusu ya watu duniani

Mabilionea wanane matajiri zaidi duniani
1. Bill Gates (US): mwanzilishi wa Microsoft (utajiri wake $75bn)

2. Amancio Ortega (Spain): mwanzilishi wa Zara na mmiliki wa Inditex (utajiri wake $67bn)

3. Warren Buffett (US): mwenyehisa mkubwa Berkshire Hathaway (utajiri wake $60.8bn)

4. Carlos Slim Helu (Mexico): mmiliki wa Grupo Carso (utajiri wake $50bn)
5. Jeff Bezos (US): mwanzilishi na afisa mkuu mtendaji wa Amazon (utajiri wake $45.2bn)

6. Mark Zuckerberg (US): mwanzilishi mwenza na afisa mkuu mtendaji wa Facebook (utajiri wake $44.6bn)

7. Larry Ellison (US): mwanzilishi mwenza na afisa mkuu mtendaji wa Oracle (utajiri wake $43.6bn)

8. Michael Bloomberg (US): mmiliki wa Bloomberg LP (utajiri wake $40bn)

Chanzo: Orodha ya mabilionea ya Forbes, Machi 2016
 
Mada ni kuhusu inequality, mwaka jana ilikua ni watu 63(kama kumbukumbua ipo vizuri) walikua na umiliki wa mali sawa na nusu idadi ya watu wote duniani. Shida hapa ni ongezeko tabaka la wenyenacho na wasionacho tofauti ya mtu wa kima cha chini ukilinganisha na yule wa kima cha ju. Madhala ni makubwa ikiwemo ongezeko la maasi katika jamii na mengineyo
 
Hii ni shida, inaonyesha jinsi gani maskini wanaongezeka kwa kasi kubwa duniani, sasa sisi third world countries sijui kama hata tutapanda kiuchumi, wachumi waje kutusaidia kuhusu hill.
 
Mkuu....
Hongera kwa kutoa taarifa ila kifupi cha neno bilioni ni ( b ) na milioni ni ( m )
Ukiandika bilioni - bn wengne hawataelewa na kanuni za hesabu haziruhusu kuandika hivi.

Nakumbusha tu mkuu....
 
Siku nikiuza mipaina yangu 10,000 pale Mufindi na mimi nitakuwa bilionea kwa hiyo tutakuwa Tisa
 
Nasikiaga kuna bilionea mmoja anaitwa Roschild mbona yeye hayupo kwenye list?

Kaka hiyo familia acha kabisa hao walioorodheshwa hapo ni mbulula tu wote hao. Familia ya rothschold ina net worth ya $500blns. Na ndio walioanzisha banking system inayotumika duniani kote.

Huyo billget na wenzake mbona masikini tu, kwanza huyo mark anatembelea porche ya $73,000 wakati huo shemeji yako nimemnunulia mchuma wa Tsh160mlns.
 
Aisee unajua waren buffet anatembea na gari gani?
 
Back
Top Bottom