MKL
Senior Member
- Mar 2, 2012
- 126
- 77
WAFANYABIASHARA watano, Said Bakhressa Gulam Dewji, Rostam Aziz, Reginald Mengi na Ali Mufuruki, wametajwa na Jarida la Ventures Africa linalozungumzia masuala mbalimbali ya uchumi wa Afrika kuwa ndiyo matajiri zaidi nchini.
Anayeongoza katika orodha hiyo ni Bakhressa anayemiliki mali na fedha zenye thamani ya Dola za Marekani 620 milioni sawa na Sh992 bilioni (Dola moja Sh1,600) akifuatiwa na Dewji ambaye utajiri wake ni Dola 560 milioni (Sh896 bilioni). Wengine na kiasi cha mali na fedha wanazomiliki kwenye mabano ni Rostam (Sh672 bilioni- Dola 420 milioni) Mengi (Sh448bilioni- Dola 280 milioni) na Mufuruki (Sh176 bilioni - Dola 110 milioni).
Chanzo ni Gazeti Mwananchi la leo
MY take
Wako wapi wezi wetu, mbona waliotajwa ni wafanyabiashara ambao hata katika hali ya kawaida tukimwondoa Rostam Azizi wengine wote hela zao zinajustification? hivi hata mtoto mdogo anaweza kubisha kuwa Bakhresa anahela Uswis?
au Mengi? Isije ikawa mafisadi wa nchi hii wameshirikiana kutengeneza habari hii ili kupindisha ukweli na hivyo sakata zima likaoshwa kiaina. kwani mtoa taaartifa alisema kuwa hela zilizofichwa nyingi zinatokana na rushwa kwenye mikataba hasa ya ujenzi, madini, Vitalu vya uwindaji na wizi mawizarani. sasa najiuliza hivi tangu lini Mengi alianza kuingia mikataba kwa niaba ya serikali au wengine waliotajwa hapo tukimwondoa Rost tamu na Ndizi....