Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,502
- 9,282
Nguzo zimewakuta wananchi. Je, watalipwa??Zaidi ya nyumba miambili zimebomolewa zilizopo karibu na umeme mkubwa wa TANESCO katika eneo la Mabibo hadi bonde la Msimbazi na kuziacha familia bila ya makazi hali iiliyosababisha vitendo vya wizi na uharibifu wa mali zikiwemo Samani,Magodoro pamoja na vifaa mbalimbali
ITV imefika katika tukio hilo la bomoabomoa na kukuta watu wakiangaika kuokoa baadhi ya mali huku wengine wakiwa na nyuso za kukata tamaa baada ya mali zao kufunikwa matofali, wengine wakilalamikia vitendo vya wizi unaofanywa na baadhi ya vijana katika eneo hilo.
Wakati hao wakilalamikia upotevu wa mali zao ITV imeshuhudia baadhi ya wananchi wakiangaika kubomoa wenyewe nyumba zao kwa lengo la kuokoa mabati na vifaa vingine vya ujenzi, huku wengine wakihamisha vitanda, magodoro ambapo wakizungumza na waandishi wa habari wamesema licha ya kuwekewa alama ya x kwenye hizo nyumba lakini kesi ili kuwa mahakamani hivyo wangepewa taarifa ili waweze kuondoa mali zao.
ITV imemtafuta msemaji wa shirika la umeme nchini ili kuzungumzia swala hilo ambapo ametoa taarifa kuwa yuko katika kikao, ambapo kumbukumbu zinaonyesha kuwa nyumba hizo ziliwekwa alama ya x muda mrefu na wakazi hao walitakiwa kubomoa nyumba wenyewe na kuondoka katika maeneo hayo hatarishi yanaliyo chini ya umeme mkubwa wa TANESCO ambayo kwa mujibu wa sheria yanamilikiwa na shirika la umeme nchini TANESCO, jambo ambalo walipinga na kuamua kwenda mahakamani.
View attachment 631792
ITV
Wajinga mtasema wanaonewa!!Bomoa time hii
Ova
We hujui madhara ya hizo nyaya za high tension! Usingefyatua uharo wako huo!!Aisee huyu ngosha huyu kuna siku yake
Halafu kuna majitu yanalaumu serikali hii!! Laiti wangejua hatari yake! Duh!Hivi hawa Wananchi wanatoa wapi ujasiri wa kujenga Nyumba chini ya line ya Umeme wa zaidi ya 33KV???
Mimi nimeishi pale long time, hapakuwa na nyumba chini ya nguzo, watu ndio wamefuata nguzo, pale Peninsula lilikuwa dampoNguzo zimewakuta wananchi. Je, watalipwa??
Wajinga ni Wale waliyowapa ruhusa kujenga hapoWajinga mtasema wanaonewa!!
Hakuna aliyewapa ruhusa wewe!! Mi nakwambia nimekaa mabibo zaidi ya miaka 25 iliyopita, walikuja wenyewe tu, na pale palikuwa jalala kubwa tu, wakajimegea maeneo kimya kimya basi! Ila wenyeji tulikuwa tunawacheka tuWajinga ni Wale waliyowapa ruhusa kujenga hapo
Ova