Mabibo, Dar es Salaam: Zaidi ya nyumba 200 zabomolewa zilizochini ya umeme mkubwa jijini DSM

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,482
9,242
Zaidi ya nyumba miambili zimebomolewa zilizopo karibu na umeme mkubwa wa TANESCO katika eneo la Mabibo hadi bonde la Msimbazi na kuziacha familia bila ya makazi hali iiliyosababisha vitendo vya wizi na uharibifu wa mali zikiwemo Samani,Magodoro pamoja na vifaa mbalimbali

ITV imefika katika tukio hilo la bomoabomoa na kukuta watu wakiangaika kuokoa baadhi ya mali huku wengine wakiwa na nyuso za kukata tamaa baada ya mali zao kufunikwa matofali, wengine wakilalamikia vitendo vya wizi unaofanywa na baadhi ya vijana katika eneo hilo.

Wakati hao wakilalamikia upotevu wa mali zao ITV imeshuhudia baadhi ya wananchi wakiangaika kubomoa wenyewe nyumba zao kwa lengo la kuokoa mabati na vifaa vingine vya ujenzi, huku wengine wakihamisha vitanda, magodoro ambapo wakizungumza na waandishi wa habari wamesema licha ya kuwekewa alama ya x kwenye hizo nyumba lakini kesi ili kuwa mahakamani hivyo wangepewa taarifa ili waweze kuondoa mali zao.

ITV imemtafuta msemaji wa shirika la umeme nchini ili kuzungumzia swala hilo ambapo ametoa taarifa kuwa yuko katika kikao, ambapo kumbukumbu zinaonyesha kuwa nyumba hizo ziliwekwa alama ya x muda mrefu na wakazi hao walitakiwa kubomoa nyumba wenyewe na kuondoka katika maeneo hayo hatarishi yanaliyo chini ya umeme mkubwa wa TANESCO ambayo kwa mujibu wa sheria yanamilikiwa na shirika la umeme nchini TANESCO, jambo ambalo walipinga na kuamua kwenda mahakamani.

umeme(17).jpg

ITV
 
View attachment 631792
ITV
Nguzo zimewakuta wananchi. Je, watalipwa??
 
Walijenga kabla au baada ya umeme mkubwa kupitishwa?
Why ubomoaji ufanyike wakati huu na si huko nyuma?
Kiongozi wa uharibifu kaingia. Simaanishi watu waachwe wavunje sheria ila twapaswa kujiuliza kwanini huu uharibifu ufanyike kipind hk kwa scale kubwa zaidi?
 
Hapo wameonewa huruma walitakiwa tolewa zamani sana
Maana ingetokea ule waya ukashuka chini mmmmmh
 
Naona wanahasira kweli hapo jengo Lao halijabomolewa likishabomolewa wataziamisha hasira zao kubomolea
 
Wajinga ni Wale waliyowapa ruhusa kujenga hapo

Ova
Hakuna aliyewapa ruhusa wewe!! Mi nakwambia nimekaa mabibo zaidi ya miaka 25 iliyopita, walikuja wenyewe tu, na pale palikuwa jalala kubwa tu, wakajimegea maeneo kimya kimya basi! Ila wenyeji tulikuwa tunawacheka tu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom