STEIN
JF-Expert Member
- Aug 29, 2010
- 1,770
- 553
Sijamsikia bingwa wa sheria mabere marando yuko wapi? pamoja na Fredie Mpendazoe, na Acardo Ntagazwa au wamewa-shibuda. hata katika kamati ya kwenda kumuona Rais wamewekwa pembeni. vivyo hivyo, nilitegemea Kitila Mkumbo angekuwa miongoni mwa wanakamati saba walioteuliwa kumuona Rais kwani ni mtambo katika kujenga hoja.
kuna tetesi kwamba kilichompoza marando ni kutetea mafisadi mahakamani akiwemo Jitu patel?
my take: 1. kama unatetea mafisadi unawezaje kujitenga na ufisadi?
2. marando anasimamia haki ipi kwa kachanganya sheria na siasa?
3. chadema hawawezi kuchafuka kwa kiongozi mkuu wa chama kuwatetea mafisadi?
4. je, marando hawezi kutoa siri za chadema kwa mafisadi juu ya namna chadema ilivyojipanga kuwashughulikia mafisadi?
acha uchokozi, Marando anafanya kazi ya kuwatetea baadhi ya watu waliofanywa kondoo wa kafara.
Mimi sina tatitzo profession ya mtu, ila kama mtu kapigwa risasi na polisi kwa tuhuma za ujambazi akifikishwa hospitali inamaana Dk atakayemsaidia ni jambazi, jibu ni HAPANA.
Marando anawatetea wale jamaa ili wampe DOCs. muhiu zinazohitajika katika Ustawi na ukuaji wa CDM.