Mabere Marando asema Meseji zilizodaiwa kutumwa kwa Mwigulu ni za kuchonga!

mayenga

JF-Expert Member
Sep 6, 2009
4,118
1,966
Mwanasheria wa Chadema Mabere Marando ameieleza Clouds Tv muda huu kuwa katika uchunguzi uliofanywa wamegundua kuna teknolojia ambayo mtu anaweza kukutumia msg kwa namba yoyote na ikaonesha kuwa ametumiwa na mtu mwingine tofauti na mtumaji wa awali kwa kutumia mtambo maalumu.

Inaaminika mtambo huo umenunuliwa tangu mwaka jana na kigogo mmoja wa serikali kutoka Israel.
 
Tatizo hawakujua kuwa kuna technolojia ya kugundua upotoshaji huo. Halafu hawakuwa smart enough katika kuzichonga zile msg, zimekaa kipropaganda zaidi. Nawasikitikia kwa kuingia gharama za bure katika kununua huo mtambo.
 
Nini tena? Mbona habari inaanzia juu juu. Tupeni habari kuna msg gani tena za Nchemba?
 
Mwaigulu Nchemba alidaiwa kutumiwa meseji za vitisho na viongozi wa Chadema wakimtishia.Baadhi ya meseji hizo ziliwekwa hapa jamvini.Kwa uchunguzi wa CDM meseji hizo no za kuchongwa na si za kweli.Kimbunga nadhani mpaka hapo tuko pamoja.
 
Tatizo hawakujua kuwa kuna technolojia ya kugundua upotoshaji huo. Halafu hawakuwa smart enough katika kuzichonga zile msg, zimekaa kipropaganda zaidi. Nawasikitikia kwa kuingia gharama za bure katika kununua huo mtambo.


Kuna gazeti moja limeandika kuwa baba wa yule kijana aliyeuwawa huko Singida ni kiongozi wa CHADEMA huko Singida. Na tukurudi nyuma tunaambiwa kuwa CHADEMA walikuwa na taarifa juu uwepo wa vijana wa UVCCM waliotayarishwa kuleta fujo kwenye huo mkutano. Sasa hili linaleta swali, je marehemu ambaye alikuwa ni UVCCM anaweza kuwa 'alishughulikiwa' na CCM kwa kudhani kuwa yeye nduye alitoa 'siri' za mpango wa kuleta fujo kwenye mkutano wa CHADEMA?
 
Marando naona anatumia ile technic ya kina Lipumba mwaka 2000 waliposhindwa kwenye uchaguzi na jembe BWM, wakaja na uongo eti CCM wamechapisha karatasi za kura china zimewekwa kifaaa kinacho hamisha alama ya vema kutoka kwa Lipumba kwenda kwa Kikwete.
 
Mtambo unaitwa sms spoofing, Marando anasema alifanya kiapo na kila mbunge wa Chadema na kila mmoja alisema hakutuma hizo sms na ndipo alifanya uchunguzi kujua teknolojia iliyotumika ndipo ikasemekana kunauwezekano ulitumika mtambo huo ulionunuliwa na mtoto wa kigogo mmoja.
 
en.png
de.png
fr.png
ru.png
es.png
[h=1][/h]

6:15pm 20/07/12




logo3.jpg

slogan.jpg







home.jpg


homecontent2.jpg
Welcome!
Send text messages from any sender ID to any mobile in the world. You can customize
homecontent3.jpg
the sender ID as alphanumeric text or any phone number. You can set a scheduler to send a message at any time you want.
homecontent_b.jpg






 
Source ITV habari

Adai ushahidi anao ni mtambo ulio nunuliwa Israel una uwezo wa kuingiliana namba na mtu kwa umbali wa Kilometer 5 na unauwezo wa kuandika sms na kuituma na sms ikaingia kama inetoka kwa mbaya wako.

Kasema mtambo huo umenunuliwa na mtoto wa kigogo aliyeko Ikulu na baba yake ni mtu mkubwa sana nchini.

Na kinachofanyika ni kuwachafua CDM
 
Mbona Marando hamtaji huyo mtu na baba yake? Hili nalo limekuja na litapita tu. Marando anasema anazo data za kutosha basi angetaja na kimwambia mtajwa kama anaona si kweli nasi akashitaki. Marando si upasue jipu?
 
​huna mshiko kalale au ongea na kisomo cha watu wazima
Marando naona anatumia ile technic ya kina Lipumba mwaka 2000 waliposhindwa kwenye uchaguzi na jembe BWM, wakaja na uongo eti CCM wamechapisha karatasi za kura china zimewekwa kifaaa kinacho hamisha alama ya vema kutoka kwa Lipumba kwenda kwa Kikwete.
 
Haaa, ndo naipata hii ITV Kamanda Mabere akitoa ufafanuzi kuwa huyu ni mtoto wa kigogo nchini.......yule kijana aliye maliza chuo juzi tu na leo ni tajiri kupindukia lazima anahisika hapa, na hatimae kamuingiza king Mchemba......kiukweli CDM inapendwa na Mungu baba wa Mbinguni
 
Back
Top Bottom