Mabenki na mikopo ya biashara kwa graduates | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabenki na mikopo ya biashara kwa graduates

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by NasDaz, Dec 1, 2011.

 1. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #1
  Dec 1, 2011
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280
  Thread hii ni summary ya makala ambayo niliitoa kwenye gazeti la Rai wiki kadhaa zilizopita. Aidha, makala hiyo ilikuwa ni matokeo ya informal survey ambayo nilipata kuifanya siku za nyuma.
  Kwa kifupi, katika utafiti huo usio rasmi nilitaka kufahamu graduates wa hapa Tanzania wanavipa thamani gani vyeti vyao vya taaluma. Hivyo, moja ya maswali ambayo nilikuwa nawauliza wadau, ni kiasi gani cha fedha ambacho wangekuwa tayari kulipwa ili kuviuza vyeti vyao permanently! Katika utafiti huo, hakuna hata mmoja ambae alitaja fedha chini ya TZS 50 million!! Hapo, ndipo nilipokuja kubaini kwamba kumbe graduates wetu hapa TZ wanavipa thamani kubwa sana vyeti vyao! Hata hivyo, bado thamani hiyo inaelekea haijaonekana na mabenki yetu!

  Miezi michache baadae(tangu nilipofanya hiyo informal survey) nikahudhuria on job training wakati nikiwa kibarua wa benki moja nchini. Katika training hiyo, trainees wengi walikuwa ni wale ambao walikuwa waajiriwa wa benki chini ya mwaka mmoja. Wakati huo, mimi nilikuwa na experience ya miaka 3. Trainees wenzangu hawa walikuwa na malalamiko dhidi ya mwajiri kwamba (mwajiri) alikuwa na ubaguzi katika utoaji wa mikopo kwa wafanyakazi wake (bank staff). Kwa ufupi, waajiriwa wa benki ambao walikuwa ndani ya ajira chini ya miaka mitatu walikuwa na unfavourable terms ambazo majority (Tellers + Loan Officers) zisingewawezesha kupata mkopo hata wa TZS 2million! Hata hivyo, niliwahabarisha wenzangu hao kisa cha mwajiri kuwa na double standards kwa wafanyakazi wake mwenyewe. Kwamba, staff wengi walikuwa wanachukua mikopo na kuingia mitini na hatimae kuwa ni loss ya benk! Na kwavile staff hao wanakuwa wamekaa kwenye ajira kwa muda mfupi, basi hata benefits zao za PPF zisingeweza kufidia mikopo hiyo. Hivyo, nikawaambia wazi kwamba, hata wakikutana na mwajiri na kutoa malalamiko yao hilo ndio jibu watakalopewa na hivyo nikawapa changamoto ya kuanza kwanza kutafuta jibu la ku-defend dhidi ya hoja ya mwajiri. Isingeingia akilini kusema “hivi sasa tutakaochukua mkopo hatutaacha kazi!” Hiyo ingekuwa ni hoja dhaifu kwa vigezo vyovyote vile!
  Wote, hawakuwa na jibu la kuridhisha!

  Hapo nikawauliza, wanaonaje wakimweleza mwajiri kwamba wapo tayari kuweka Original Academic Certificates kama hati ya dhamana kwa mikopo watakayochukua! Hapo mjadala ulikuwa mkali huku kila mmoja akiona ugumu wa kuweka cheti chake kama hati ya dhamana......bila shaka ni kwavile, kwao cheti ni kitu muhimu sana!

  Hapa tena, ndipo nikaja kuona thamani ya vyeti vyetu; thamani ambayo bado haijaonekana na mabenki yetu!
  Hapo ndipo nikaja kujiuliza, hivi thamani iliyo bora kwa benki ni ipi!!! Hakuna shaka yoyote kwamba wengi wetu (including bankers) tunaamini dhamana iliyo bora kwa benki ni ile inayouzika kirahisi! But the question follows; what will happen pale benki itakapokuwa na dhamana (say, nyumba) kadhaa za wateja ambao wameshindwa kulipa mikopo yao?! Bila shaka, kitakachotokea ni kile kilichotokea America na kusababisha msukosuko wa uchumi duniani. Mabenki yalikuwa na nyumba kadhaa za wateja walioshindwa kulipa mikopo yao na kusababisha thamani ya nyumba kwenda chini na hatimae mabenki kupata hasara!
  Hivyo basi, ukichunguza kwa makini, utagundua kwamba dhamana iliyo bora siyo tu ile ambayo inauzika kirahisi (easily sold), bali pia ile ambayo mkopaji hatakuwa tayari kuipoteza kirahisi huku umuhimu wa vigezo hivyo viwli ukiwa almost the same! Therefore, kwa msomi, hususani yule ambae hana tangible asset (collateral), bila shaka kitu pekee ambacho hatakuwa tayari kukipoteza kirahisi ni cheti chake (ACADEMIC CERTIFICATE). Huyu, ukimpa mkopo wakati hati ya dhamana aliyoiweka ni cheti cake, basi bila shaka atakuwa makini kwenye mkopo aliouchukua ili aweze kuurudisha. Kama hivyo ndivyo, ni kwanini basi mabenki yasifanye tathimini ya kina kuangalia uwezekano wa kutumia Academic Certificates kama hati za dhamana?! Is it worthless?! I don’t think so! Ni kweli kwamba Academic Certificates has no market value (haviuziki) in case mkopaji akishindwa kulipa mkopo, lakini tusisahau vilevile kwamba hii ni dhamana ambayo mwenye nayo hatakuwa tayari kuipoteza kirahisi. ACADEMIC CERTIFICATE ndiyo maisha yenyewe kwa msomi!

  Kutokana na ukweli huo, ningependa kutoa changamoto kwa mabenki ya biashara pamoja na serikali (decision makers) kuangalia ni namna gani jambo hilo linaweza kutekelezeka in a WIN-WIN situation! By the way, huu ni wakati wa mabenki kuacha ku-rely in traditional banking practices! Dunia ina-change very fast huku sekta hiyo (banking sector) ikiwa inatishiwa na changamoto nyingi zinazotokana na maendeleo ya sekta ya teknolojia ya mawasiliano. Ingawaje Tigo Pesa na M-Pesa imeanza miaka michache tu iliyopita, lakini tayari idadi ya wateja wake ipo almost the same as wale walio kwenye traditional banking sector iliyopo zaidi ya miaka 50 iliyopita! Tayari, upande wa deposits kwa mabenki umeshatikiswa na uwepo wa mobile banking! Sooner or later, mabenki yatarajie kutikiswa upande wa mikopo....!! Tayari, kampuni za simu zinakopesha wateja wake muda wa maongezi, hivyo muda si mrefu utakuja kusikia wanaanza kutoa mikopo midogomidogo! Hili linawezekana kabisa....let’s wait and see; time will tell. Na hilo likitokea, utakuwa ni mtikisiko mwingine kwa mabenki, husani yale ambayo ni purely, retail banks. Sasa, ni kwanini basi mabenki yetu yasiwe creative enough na kuangalia other options?! Suala la kutumia ACADEMIC CERTIFICATES kama hati ya dhamana, linawezekana; kinachohitajika ni mipango tu. Binafsi, nina mawazo yangu katika hili. Hivyo, ni wakati wa wadau kutoa mchango wao ni namna gani wanadhani jambo hili linaweza kufanyika very succesful.

  Hili likiwezekana, litakuwa limesaidia sana kwenye uchumi wetu. Kwanza, mabenki watakuwa na portifolio za wateja wasomi wenye ufahamu mkubwa....kwa kawaida watu wa aina hii wanakuwa motivated na expansionsm. Hii ni opportunity kwa mabenki! Kwa upande wa serikali, hii itasaidia sana kupunguza tatizo la ajira nchini. Sina shaka wasomi wengi wana viable business ideas lakini wanashindwa kuzitekeleza kwa ajili ya ukosefu wa mtaji! Sio siri, endapo hata yale mabilioni ya JK yangetumika kudhamini program kama hizi basi bila shaka productivity yake ingekuwa kubwa zaidi kuliko ilivyokuwa. Na overall outcome ya hii kitu ni kuongezeka kwa uwekezaji toka kwa wazalendo!

  Ningeshauri Mods, wai-sticky thread hii ili wadau wapate kutoa maoni yao na huenda wakatokea wa kuona (decission makers, from gvts and commercial banks) umuhimu wa ki2 na kuamua kuifanyia kazi.

  NAWAKILISHA!

   
 2. M

  Magezi JF-Expert Member

  #2
  Dec 1, 2011
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mkuu nashukuru sana kwa mada hii. Mimi pia nimekuwa nikifikiria ni kwa vipi naweza pata hata ka-mkopo ka kuweza kuanzisha hata ka gereji kadogo (Mimi ni mechanical Eng. tena mwenye FTC na kazi naijua vyema). Huwa sipati pa kutokea kwani mikopo ya mabenki mpaka uwe na dhamana ya mali isiyohamishika..... mlala hoi kama mie sina mali hiyo.

  Lakini kama ulivyo eleza kwa makini, mabenki na serikali wangeweza kuwasaidia vijana wengi kwa kuwakopesha na dhamana iwe vyeti vyao originals, hapo vijana wengi tungetoka.
   
 3. f

  fisi 2 JF-Expert Member

  #3
  Dec 1, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,337
  Likes Received: 521
  Trophy Points: 280
  YES hili ni wazo vumbuzi na linafaa sana kupewa structure lifanikiwe. Muhimu ni kuwa uwekwe mfumo wa kudhibiti ufuatiliaji wa recoveries. Hii ni kwa sababu kinyume na secuirty zingine what do you do with a certificate (Degree or diploma) in case of default.
   
 4. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #4
  Dec 1, 2011
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280
  u're right, na ndio maana nimetangulia kuisema hiyo weakness ya kutouzika na ndio maana nimeshauri kuihusisha serikali. Kama ulivyozungumza, ni sula la kulipa good structure!!
   
 5. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #5
  Dec 1, 2011
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280
  umeona enh?!
   
 6. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #6
  Dec 1, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  post nzuri sana nasdaz hata mimi nitalidiscuss na wadau wenzangu then nitakupa feedback
   
Loading...