MABASI YA MWENDOKASI UBEBAJI WA MIZIGO UMEKUWA KERO SASA

Euphransia

JF-Expert Member
Jan 26, 2017
937
778
Hakika dhana ya mabasi ya mwendo kasi ya kuwa yatakuwa tofauti Na daladala zetu haipo tena kutokana Na utendaji wake kuwa ule ule wa daladala.Utofauti uliopo labda ni
1.Aina ya mabasi
2.Kwenda haraka
3.Vituo vya kisasa, tiketi Na kadi za kieletroniki.
Lakini ubebaji wa abiria ni wa kugombania kama daladala za kawaida,Ubebaji Mizigo hasa Kutika Kivukoni kwenda Kimara ni zaidi ya Daladala Mizigo inawekwa mpaka chini ya viti kwenye sehemu ambayo watu husimama Na hata upitaji huwa mgumu sana.
Pia kuna suala la kugombania kupanda hasa kituo cha Kivukoni Na Kimara, Tunauomba Uongozi itoe elimu ya kutosha au kuwe Na watendaji wa kuwaongoza abiria maana watanzania bado sana katika mambo ya ustarabu unakuta mama MTU mzima Na baba MTU mzima wanagombea kiti.
 
Waweke maloli ya mwendo kasi kwa ajili ya mizigo...au kuwe na tela la mizigo nyuma ya basi
 
Waswahili waswahili tu hata uwaletee mabas ya kupaa bado atataka kufungua dirisha anunue kandolo
 
Hivi kuna tatizo kwa mtu kusafiri na mzigo wake? Hata huko tulipoiga, watu husafiri na mizigo yao. Tatizo ni kwamba mabasi yanajaza kupita kiasi
 
Back
Top Bottom