Mvua, Dar: Watu 9 Wafariki, Mabasi ya mwendokasi yamesitisha huduma

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Kampuni inayotoa huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam, UDA Rapid Transit (UDART), inaujulisha umma kuwa, huduma za mabasi hayo kwa baadhi ya njia zimesitishwa kuanzia saa 11:00 alfajiri tarehe 15/04/2018 kutokana kufungwa kwa Barabara ya Morogoro eneo la Jangwani kwa sababu ya mafuriko yaliyosababisha maji kupita juu ya daraja la Mto Msimbazi.

Kwa sasa huduma zinatolewa kwa njia za Kimara - Morroco, Kimara - Magomeni Mapipa, na Gerezani - Muhimbili. Huduma kamili zitarejea mara baada ya barabara kufunguliwa.

Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza. Deus Bugaywa, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UDART.

UPDATES:

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar, Lazaro Mambosasa amesema, watu watatu wamefariki dunia ambapo miili yao imeokotwa eneo la Tabata Kisiwani, Dar es Salaam.

Watu wawili kati ya hao (mama na mtoto) wameangukiwa na ukuta wa nyumba, na mwingine mwili wake umeokotwa mtoni.



=====

Mvua inayoendelea kunyesha kwa siku ya tatu leo Jumatatu Aprili 16, 2018 imesababisha barabara kutopitika, huku baadhi ya wanafunzi wakirejeshwa nyumbani.

Wanafunzi wa shule ya St. Florence Academy iliyopo Mikocheni wamerudishwa nyumbani kutokana na maji kujaa shuleni.

Kutokana na hofu ya madhara ya mvua, baadhi ya wazazi wamewazuia watoto wao kwenda shuleni.

Baadhi ya barabara ikiwamo inayopita eneo la Shoppers Plaza Mikocheni haipitiki kutokana na kujaa maji.

Msongamano wa magari ni mkubwa barabara za Mandela na Nyerere ambako licha ya mvua baadhi ya watu wameamua kutembea kwa miguu.

======

Watu saba wamefariki dunia kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam.




DSC_4715%20(1).JPG

Kamanda wa polisi kanda maalum jiini Dar es salaam Lazaro Mambosasa amethibitisha vifo hivyo, na kueleza kwamba mwili mmoja umekutwa ukielea kuelekea maeneo ya Jangwani jijini Dar es salaam.

Sambamba na hilo Kamanda Mambosasa amesema maeneo mengi jijini Dar es salaam yamejaa maji, na kuwataka watu kuwa makini wanapotumia barabara hasa sehemu zenye makorongo, na kuwaangalia zaidi watoto ambao wanapita mara kwa mara wakienda shule au wakiwa wanarudi kutoka shule.

“Watu wasijaribu maji, ukijaribu maji ujue utaondoka nayo, kwa hiyo watoto wetu wanapokwenda shuleni tuwasindikize, sehemu nyingi zenye makorongo kwa mfano kule Kinyerezi, kule Goba kule Makongo, zile shortcut zote maji yamejaa, watu wajiepushe kutumia njia hizo, watapoteza watoto wakiwa wanaenda au kutoka shule”, amesema Kamanda Mambosasa.

Jeshi la Polisi limesema litaendelea kutoa taarifa za sehemu mbali mbali kuhusu hali ya mvua, ambayo inaendelea kuathiri sehemu kubwa ya nchi.

MWENDELEZO: Idadi ya watu waliofariki kutokana na Mvua inayoendelea kunyesha jijini Dar imefikia 9 huku wengine 6 wakijeruhiwa

> Kamanda Mambosasa amedai jiji linapokea maji mengi kutoka maeneo ya Kisarawe ambayo ndio yanaleta madhara makubwa
 
Kile kituo cha Jangwani katikati ya mto msimbazi kwanini walikijenga? Abiria gani wako pale na kile kituo ndio kinazuia maji na kusababisha mafuriko makubwa sbb wame block maji ya mto msimbazi, Mh. Rais wangu, bomoa kile kituo cha abiria katikati ya mto msimbazi pale Jangwani, yaani una block maji ya mto alafu unategemea nn kama sio mafuriko makubwa..!! Nashikwa na hasira sana once i see that ghost bus station katikati ya mto, i wish i could be JPM.. Ningebomoa from day one..!!
 
Mradi wa kipumbavu sana huo
Hapa tumia akili kidogo, NI BARABARA YA MOROGORO PALE JANGWANI IMEFUNGWA, HATA WEWE UKIENDA NA GARI LAKO HAURUHUSIWI KUPITA, ni polisi na wenye hiyo barabara wameifunga kwa mu
da, sasa ulitaka wao wapite kivipi??
Kimara to moroko to mapipa na fire to muhimbili huduma wamesema ipo.
 
Hii mvua imeanza toka jana usiku pale jangwani ilikuwa lazima pafungwe tu.

Afadhali leo J2 sio watu wengi wanaingia katikati ya jiji na hii mvua imezuia watu wengi kutoka leo
 
Nimeshangaa barabara mpya walishindwa kuinyanyua kutoka fire mpaka mapipa, mradi wa ovyo sana. Magufuli siku zote mirad yake ni hasara tu.
 
UDART jengeni stendi kubwa maeneo ya kibamba, kiluvya kuna maeneo makubwa na salama muda wote, acheni Kung'ang'ania maeneo hatarishi, uwekezaji mkubwa kama huo unahitaji umakini. UDART tokeni hapo jangwani.
 
Hawa wakandarasi waliojenga ile barabara walitakiwa wawe jela hadi muda huu!hivi walishindwa kubuni namna ya kuinyanyua ile barabara kuanzia magomeni hadi fire?au ndo walifanya kusudi.Kutia serikali gharama mara mbilimbili
 
Back
Top Bottom