Mabasi ya mikoani kugoma Jumapili

Mabasi ya mikoani kugoma Jumapili

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
26,703
Reaction score
59,224
CHAMA cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa) kimesema kitasitisha huduma ya kusafirisha abiria kwenda mikoa yote nchini Jumapili ili kufanya ukaguzi wa mabasi yake, hatua ambayo itakuwa sawa na mgomo.

mabasi.jpg

Aidha, Taboa imesema inapinga uamuzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) kutangaza kuyafungia mabasi yote ya kampuni ya City Boy badala ya moja ambalo lilisababisha ajali mkoani Singida hivi karibuni.

Julai 4, mabasi mawili ya kampuni hiyo yaligongana uso kwa uso na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 30 wilayani Manyoni mkoani Singida.

Taboa imesema pia itaipeleka serikali mahakamani kutokana na kufungiwa kwa mabasi hayo kwani kwa mujibu wa sheria, aliyetakiwa kulifungia ni waziri mwenye dhamana na si Sumatra kama ilivyofanyika.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana mara baada ya kumaliza kikao cha dharura cha wamiliki wa mabasi ya mikoani, Katibu wa Taboa, Enea Mrutu, alisema hawatakatisha tiketi kuanzia Jumapili ili kujipa muda wa kukagua mabasi yao kama yana uwezo wa kufanya safari ama la.

"Tumeamua kwa pamoja kuwa, kwa sababu tayari tumeshafanya 'booking' ya abiria, kuanzia Agosti 21 mwaka huu, tuanze kufanya ukaguzi wa mabasi yetu kote nchini ili yale ambayo hayana sifa yakae pembeni na yale yanayostahili kusafirisha abiria yafanye hivyo, kuliko utaratibu huu wa serikali wa kuyafungia yote bila kujali gari lililohusika kwenye ajali," alisema Mrutu.

Aidhja alisema wanapinga vikali agizo la Sumatra la kuyafungia mabasi 60 ya kampuni 12 kwa makosa ya kusababisha ajali na wanataka mabasi yanayohusika pekee ndio yafungiwe.

Alizitaja kampuni zilizofungiwa mabasi yake kuwa ni Mohamed Trans, City Boy, Ota High Class, Kisbo Safari, Kisbo Express, Lubonelo na Kanda Safari.

WAPIGA SAFARI SIKU 2

Mrutu pia alisema kikao kicho kilipinga azimio la serikali kutaka mabasi yanayoenda masafa marefu kama mikoa ya Mwanza na Mbeya kutumia siku mbili na badala yake yatumie siku moja kama ilivyokuwa awali.

Alitaja azimio la tatu kuwa ni kufunga mfumo maalum wa udhibiti wa magari (Car Track System) ambao utaunganishwa na ule wa Sumatra ili kuliona gari lilipo kwa lengo la kudhibiti ajali.

Aidha, Mrutu alisema wamekubaliana mabasi yote yatatembea kilometa 80 kwa saa moja na 50 pale inapohitajika kama kwenye matuta ili kuepuka ajali.

Alisema wamekubaliana pia dereva atakayehusika kutembea zaidi ya mwendo waliokubaliana, afukuzwe kazi na kumchukulia hatua stahiki.

"Kama magari yetu tutayafanyia ukaguzi na pia kufunga kifaa cha kulionyesha basi na kupunguza mwendo, hakuna haja tena ya kutaka tusafiri zaidi ya siku moja... maeneo wanayoona kuna hatari ya usalama ni bora yakasubiriana na askari wakayasindikiza mpaka yanapokwenda," alisema.

Aliendelea kueleza kuwa wamekubaliana Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, awahakikishie hakuna askari atakayedai mabasi hayo rushwa.

Mrutu alisema wamekubaliana mabasi yasikaguliwe kila kituo ili kuepuka kupoteza muda wakati wakisafiri kwenda mikoani ambako kunasababisha madereva kutembea mwendo kasi ili kuokoa muda waliopoteza njiani.


Chanzo: Nipashe
 
Aidha, Taboa imesema inapinga uamuzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) kutangaza kuyafungia mabasi yote ya kampuni ya City Boy badala ya moja ambalo lilisababisha ajali mkoani Singida hivi karibuni.
Aisee hawa ndio wamiliki wa mabasi, je madereva watakuwa na akili gani?!! Sasa lililosababisha ajali ni write-off utalifungia vipi? Vile vile bus halisababishi ajali ni dereva ambae yupo chini ya kampuni ndio anasababisha ajali. Ukimfungia dereva hizi kampuni uchwara wanachukua dereva mwingine mnywa viroba anaenda kuua watu wengine. Kampuni ndio inastahili adhabu.
 
Kwa mbali naona ufumbuzi wa kudumu kutokana na SGR kama kweli itakamilika. Usiniulize kwa nini kwa sababu ni suala mtambuka.
 
ila hawajatuambia hiyo service itachukua siku ngapi.....dawa ni kuwa makini barabarani kusafiri kwa siku mbili si mchezo nauli zetu tu za kuunga unga sasa ufike njiani ulale mpaka siku ya pili duh....dawa ni speed 80 na huku unaibia 120 kwa umakini zaidi
 
Aisee hawa ndio wamiliki wa mabasi, je madereva watakuwa na akili gani?!! Sasa lililosababisha ajali ni write-off utalifungia vipi? Vile vile bus halisababishi ajali ni dereva ambae yupo chini ya kampuni ndio anasababisha ajali. Ukimfungia dereva hizi kampuni uchwara wanachukua dereva mwingine mnywa viroba anaenda kuua watu wengine. Kampuni ndio inastahili adhabu.
Sawa lakini pia serikali ifunge hospitali zake zote kwa sababu hospitali yake moja ilimfanyia upasuaji wa kichwa mtu aliyetakiwa kufanyiwa upasuaji wa mguu! Na nyingine ilisababisha mjamzito kujifungulia bafuni!!
 
Sawa lakini pia serikali ifunge hospitali zake zote kwa sababu hospitali yake moja ilimfanyia upasuaji wa kichwa mtu aliyetakiwa kufanyiwa upasuaji wa mguu! Na nyingine ilisababisha mjamzito kujifungulia bafuni!!
Sawa.
 
Reli ifufuliwe tuachane na kasumba za mabasi kutesa raia kila mara. Kuua wawaue kwa kusababisha ajali kutokana na uzembe na mwendo kasi, halafu bado wawatese kwa kuwanyima kusafiri. Ifikie mahali tuwe na mbadala wa hawa watu.
 
Gomeni tu mbona Hata mkuu Amegoma Anakagua wafanyakazi hewa
 
Heko Taboa hoja mko nayo msikubali kuyumbishwa. Simameni imara simamieni haki zenu. Msikubali kuburuzwa kiuchwara uchwara namna hii.

Dar Mwanza haiwezi kuwa siku 2.

Wafanye test drive kwa magari yao ili waone mwendo upi ungekuwa sahihi kutumika safari kuchukua siku 1 na pia mwendo kuwa salama. Siyo kukurupuka tu na kujifanya wao ndiyo wenye akili za kufikiria.

Kisheria hakuna makosa ya jumuiya. Kosa la dereva mmoja haliwezi kuwa kosa la basi, wala basi jingine wala la mtu mwigine yeyote asiyehusika. Tunayo safari ndefu pasipo na kufuata utaratibu wa sheria.
 
Kwanza pesa itakayopotea siku hiyo daaah yaani hata sijui nisemeje ;!!
 
Back
Top Bottom