Mabasi ya mikoani kugoma Jumapili

Mabasi ya mikoani kugoma Jumapili

Aisee hawa ndio wamiliki wa mabasi, je madereva watakuwa na akili gani?!! Sasa lililosababisha ajali ni write-off utalifungia vipi? Vile vile bus halisababishi ajali ni dereva ambae yupo chini ya kampuni ndio anasababisha ajali. Ukimfungia dereva hizi kampuni uchwara wanachukua dereva mwingine mnywa viroba anaenda kuua watu wengine. Kampuni ndio inastahili adhabu.
Hii ni hakika kabisa, ifike wakati hizi kampuni ndio ziwajibishwe kwelikweli si kwa kufungia tu hata kwa faini kubwa ili kufidia wahanga kwa kuwa wao wenyewe wamekua wakiwaruhusu madereva wao washindane barabarani, hivyo wamekuwa wakijali maslahi yao tu bila kujali usalama abiria
 
Mkuu unafahamu kuwa hakuna makosa ya jumuiya? Kosa la mwanao haliwezi kuwa kosa lako wala la mtu mwingine yeyote asiyehusika. Mawazo uchwara kama yako ni mwendelezo wa haya haya yaliyotufikisha hapa tulipo tunapodhania kuwa nchi huendeshwa kwa mawazo ya mtu badala ya kufuata katiba.
 
Sidhani kama umenielewa, umekurupuka tu kujibu. Mfano uliotoa wala haufanani na mazingira haya.
Matajiri wa mabasi ndio huwapa kiburi madereva mpaka imefikia wanavunja sheria za barabarani ili tu kuwaridhisha matajiri zao. Katika hili unawezaje kusema tajili hahusiki?
 
Kuanzia Jumatatu wiki ijayo hakutakuwa na usafiri wa mabasi nchi nzima, baada ya Wamiliki wa mabasi yaendayo mikoani (Taboa) kuamua kusimamisha huduma hiyo ili yafanyiwe ukaguzi na Polisi.

Katibu Mkuu wa Taboa, Enea Mrutu amesema zaidi ya mabasi 4,000 yanayohudumia safari za mikoani, yatasimamisha huduma kuruhusu ukaguzi uliolenga kupunguza ajali za barabarani na kwamba, wameshaiandikia Sumatra barua kuitaarifu juu ya suala hilo.

“Tunataka mabasi yetu yakaguliwe kwa pamoja ili mamlaka husika zithibitishe ubora na kama yanaweza kuendelea kutoa huduma za usafiri bila wasiwasi wowote,” amesema.

Chanzo:Mwananchi
 
hivi hiyo car tracking ni kuzuia wizi au ajari?

huo ni mradi wa wachache kama ule wa speed governor (romantic).... hii nchi usanii kila sehemu.

hilo la madereva kufukuzwa kazi wakizidisha mwendo(kph 80), hiyo adhabu itawaumiza madereva wengi...
 
Kama unaishi nje ya dar, huko ni mkoani..
Mkoani ni Dar-es-salaam
Dodoma ndio Makao Makuu kila siku Majaliwa anawaambieni.
mimi li-Basi linalokwenda kilomita 80/h masaa 10 kutoka Dodoma hadi Mkoani Dar sipandi.
waacheni wagome
 
Huu ubabe wa serekali na viongozi wake utaligarimu taifa. Wafanya kazi wa serekali nao ni bomu linalosubiriwa kulipuka muda wowote
 
Sidhani kama umenielewa, umekurupuka tu kujibu. Mfano uliotoa wala haufanani na mazingira haya.
Matajiri wa mabasi ndio huwapa kiburi madereva mpaka imefikia wanavunja sheria za barabarani ili tu kuwaridhisha matajiri zao. Katika hili unawezaje kusema tajili hahusiki?

Kwa andiko lako "wewe nidyo mwenye akili" na unaowaita matajiri wa mabasi "ndiyo wajinga". Ama kweli tunayo safari ndefu. Si hivyo tu umeenda mbali kusema kuwa Matajiri hao ndiyo wanawapa kiburi madereva kama symbiotic identity yako. Hivi kwa mawazo ukiwa tajiri wa basi hilo tu ndiyo ndiyo linalokufanya pia unakuwa wa kuwapa kiburi madereva wala hakuna namna nyingine?

Kwa taarifa yako hao unaowaita matajiri wa mabasi si wajinga kama unavyofikiria. Fanya utafiti kwanza kabla ya kusema. Vinginevyo utadhani wenzako wamekurupuka kumbe wewe ndiyo haswa.

Ama kweli nyani hawezi ona "Kundule".
 
Back
Top Bottom