Mabasi ya haraka, daraja la kigamboni et al - Serikali itoe elimu rasmi

Mtangoo

JF-Expert Member
Oct 25, 2012
6,167
5,610
Nimeona video ya Waziri mkuu jana na askari aliyeambatana nae akionya watakaovunja sheria watachukuliwa hatua. Ni jambo jema! Ila kabla ya kuwachukulia hatua lazima tuangalie chanzo cha uvunjaji wa sheria.

Kuna aina mbili za wavunjaji sheria - Wanaojua na wasiojua. Na wote huhukumiwa! Sasa ni vyema tukaondoa kundi la pili ili kubakia na kundi la kwanza, yaani wanaovunja kwa kujua. Ili kuainisha ukweli kuwa kuna kundi la pili nitatoa mfano wangu mwenyewe.

Kuna kipindi nilikaa muda mrefu sana bila kwenda "mjini" hapa Dar es salaam. Siku naenda mjini nilikutana na mabadiliko mengi sana. Kutoka magomeni mapipa kwenda mwenge kwa mfano, ilikuwa unakata kulia ila sasa ulipaswa kunyoosha mpaka mbele amabako kuna U turn. Pia kulikuwa na taa za kuongozea mpya ambazo awali hazikuwepo. Ilinibidi mahali pengine kusimamisha gari na kwenda kumuuliza traffic. Watu wengi walikamatwa kwa kutokujua na faini zilizoharibu bajeti zao. Halikuwa jambo jema kabisa. Ni kama serikali iliwategea wananchi wake ili iwakamate.

Sasa tunaona mabadilko makubwa katika barabara jijini hapa na kwa kuwa watu wengi hawajui kinachoendelea, wataendelea kuvunja sheria na kukamatwa. Kwa hiyo maoni yangu kwa serikali kwa maana ya K/Waziri wa mambo ya ndani, Jeshi la polisi, DART et al watoe elimu rasmi kwa njia hizi:
  1. Watengeneze Picha za kielektronic zitakazokuwa na maelekezo na watoe link ya kupakua ili watu wasambaziane kwa whatsapp facebook et al
  2. Watengeneze video ya mfano inayohusisha mabasi ya BRT, Bodaboda, watembea kwa miguu, daladala na magari binafsi ili kila mmoja ajue jinsi sahihi ya kutumia barabara
  3. Waweke channel ya watu kuuliza maswali at least kwa miezi sita tangu leo na majibu yawekwe hadharani kama "Frequently asked questions" mtandaoni

Kwa kufanya haya ni maoni yangu kuwa tutaondoa kundi kubwa katika kuvunja sheria na vilevile tutaokoa bajeti za watu na kuondoa usumbufu ambao unaepukika.

Nimemaliza kazi yangu kama mwananchi
Mugu Ibariki Tanzania!
 
Back
Top Bottom