Mabango yenye ujumbe kwenye ziara za Viongozi

Mabango yenye ujumbe kwenye ziara za Viongozi

Mapambano Yetu

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2012
Posts
1,133
Reaction score
2,128
Suala hili ni muhimu sana kwani husaidia kufahamu nini wananchi hawajaridhika nacho. Ni vema kwenye ziara za raisi na wasaidizi wake jamii ijipange kuwasilisha matatizo yake kwa njia ya mabango. Kwa sasa CCM imekuja na mbinu mpya. Kupitia kwa watendaji wa vijiji na kata wanawashinikiza wakuu wa shule kubadili vyumba vya madarasa ambavyo wameisha anza ujenzi wake ili viwe maabara.

Vyumba hivi havina ubora hata kuwa darasa la chekechea. Hebu fikiria mtendaji wa kata pamoja na mratibu elimu wanamwendea mkuu wa shule na kumshinikiza ahakikishe ameinua jengo ndani ya siku mbili mpaka level ya kumwaga zege (renta ) ili lizinduliwe na rais au aje mkuu wa Mko/wilaya kukagua na kusifia jitihada kwenye vyombo vya habari, na hapo hata utakuta labda ramani ya msingi iliku wa ni darasa au hata msingi hakuna. Hivi hapa lengo litafikiwa?

Huu sio sawa na kupaka kaburi rangi? Madarasa mengi yaliyojengwa 2011 - 2014 hayatamaniki kwa sasa. Yamechakaa sana, yana nyufa, utadhani ni ya kabla ya uhuru. Kwa mtindo huu hatutafika. Njia bora kufichua uhuni huu ni kushika mabango kwenye ziara za hawa viongozi.
 
Nchi inaongozwa na watu wasiojali maendeleo ya watu wao ubinafsi umewajaa sana
 
Back
Top Bottom