Mabanda ya kuku ya kukodi

Mabanda ya kuku ya kukodi

kichakorojack

Member
Joined
Sep 19, 2011
Posts
78
Reaction score
12
Habari za muda huu wanajamvi.

Mimi nina shida naombeni msaada. Kama kuna mtu yeyote mwenye access ya upatikanaji au anayo mabanda ya kukodi kwa ajili ya ufugaji wa kuku naomba anifahamishe. Ninataka kuanza na kuku 1000 na hayo mabanda yawe maeneo ambayo ni salama na yawe maeneo ya kuanzia mbezi, tegeta, boko, bunju na kuendelea, yaani ukanda huu wa kuelekea bagamoyo ukianzia mbezi. Asanteni sana kwa msaada wenu.
 
Mkuu nimeona nikupe ushauri...kwa uzoefu wangu wengi wa watu waliojenga mabanda ya kuingiza zaidi ya kuku 1000 kwa ukanda wa barabara ya Bagamoyo ni watu wenye mitaji na wengi wao wanafuga kwa wingi wao wenyewe.Hivyo hata ukipata pa kukodi watakulipisha tozo kubwa na kukufanya ukose faida uliyotegemea.... Naweza kukushauri yafuatayo; Tafuta mtu mwenye miundombinu tayari ya ufugaji anayetaka kutanuka na mkaingia mkataba wa kufuga pamoja huku wewe ukitoa mtaji wa ufugaji,pili unaweza ukajichanga polepole ukatafuta sehemu yako binafsi,Pia unaweza ukafanya sehemu nyingine za Dar tofauti na ukanda wa bagamoyo...thanks
 
Back
Top Bottom