Mabadilkko ya ccm yasitufanye tuache ajenda ya katiba mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabadilkko ya ccm yasitufanye tuache ajenda ya katiba mpya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Najijua, Apr 11, 2011.

 1. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #1
  Apr 11, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Wadau naomba kuweka hoja,

  mabadiliko ya ccm wanayo yaita kujivua gamba yasitufanye tuache hoja yetu ya msingi toka kuisha kwa uchaguzi mkuu wa mwaka jana, hoja hii ni madai ya katiba mpya

  naweka angalizo hili kwa kuwa nafahamu watanzania huwa hatuna ajenda za kudumu daima tunakuwa tunapelekwa na magazeti tuu, sasa hivi mijadala yote ni kujivua gamba kwa ccm ili hali nyoka ni yule yule anayeendelea kuwauma wa tz.

  Uzoefu unaonyesha ajenda za mpito huwa zina tutoa katika ajenda zetu hata kabla hazijafika mwisho, hivi sasa hao waliojivua gamba wamewasilisha bungeni muswada wenye makosa makubwa na watatufanya tujadili mabadilko yao na kuupitisha muswada wao ili hali ukiwa na makosa hivyo hivyo kwa kuwa tumeicha ajenda hiyo na kuzungumzia mabadiliko ya gamba lao ili hali sumu hawajaitema
   
 2. Mkulima wa Kuku

  Mkulima wa Kuku JF-Expert Member

  #2
  Apr 11, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Nadhani uko sahihi...nyoka aina ya chatu akijivua gamba anabadilika na kuwa nyoka aina ya swira? Hiki ni kiini macho, ukweli kabisa tatizo la ccm ni zaidi ya Makamba, Chiligati na Mkuchika. Tatizo la ccm ni kuanzia mwenyekiti wake ambaye ameshindwa...lakini kwa kuwa mkubwa haambiwi umekosea, wanaoumia ni wengine.
  Natamani Kikwete alijue hilo kwamba tatizo la ccm ni yeye kwanza, Rostam, Lowassa na wazee wengine wasioguswa.
  Mtajionea wenyewe kama hiki si kiini macho kingine...ushahidi unaonyesha kuwa tatizo ni Kikwete hasa baada ya kuonyesha kwa dhati kuwa hapendi na hataki mabadiliko...utendaji wa Magufuli...serious President angempongeza! Kuandikwa kwa katiba mpya, serious president asingeruhusu uhuni unaofanyika sasa wa kutuletea katiba ya ccm...watanzania wenzangu msidanganyike, tatizo ni Kikwete!
   
Loading...