SoC01 Mabadiliko yanayochochea Uongozi Bora

Stories of Change - 2021 Competition

Skrancho

New Member
Jul 13, 2021
1
2
Utawala bora na uwajibikaji ni nyenzo mojawapo muhimu sana inayohitajika katika kila Taifa hapa duniani kwa ajili ya kusonga mbele. Ni kupitia utawala bora na uwajibikaji ambapo utu wa binadamu unaweza kudhihirika na kusaidia kumtofautisha na wanyama wengine, lakini pia kumsaidia binadamu kutumia vipawa na talanta alizopewa na Mwenyezi Mungu. Bila Utawala bora na uwajibikaji hakuna binadamu ambaye anaweza kudhihirisha uwezo wake katika nchi aliyomo. Baadhi ya masuala ambayo yanachochea utawala bora na Uwajibikaji ni kama vile;

Uwepo wa Katiba inayokidhi matakwa ya wananchi katika nchi husika; Katiba ni mfumo wa kisheria ambao husaidia kuonesha dira ya nchi katika masuala yote ya uongozi. Ili nchi yoyote ipige hatua katika Nyanja ya Utawala bora na Uwajibikaji katiba ni suala la muhimu sana, Katiba husaidia kuipatia nchi dira na maono ya wapi wanatoka na wapi wanaenda, lakini pia katiba husaidia kuwakumbusha viongozi waliopewa dhamana ya kuwaongoza wenzao wajibu wao ili wasiweze kuvuka mipaka katika utendaji wa kazi zao. Lakini pia katiba husaidia kulind haki za wananchi wake na kuwapa Uhuru wa kuwaelekeza na kuwapa ushirikiano viongozi wao. Nchi nyingi za Ulaya zimepiga hatua kubwa katika suala la utawala bora na uwajibikaji sio kwamba wananchi wake wana akili sana kuliko wa mabara mengine kama Afrika la hasha, bali ni mfumo mzuri wa katiba walizonazo.

Elimu Bora; Ili nchi iweze kupiga hatua katika suala zima la Utawala bora na Uwajibikaji, elimu inabidi ipewe kipaumbele kikumbwa, Ukomavu wa wananchi katika masuala mbalimbali ya kijamii, kiuchumi pamoja na kisiasa, husaidia viongozi kuwa upeo mkubwa katika kubuni mikakati mbalimbali ya kimaendeleo na uadilifu katika kusimamia haki za binadamu.

Nchi nyingi za Afrika zimeshindwa kupiga hatua katika kuleta Utawala bora na uwajibikaji kutokana na elimu duni inayotolewa kwa watu wake ambayo haiendani na kasi ya mabadiliko katika dunia ya leo. Mitahala mibovu, miundombinu hafifu, ukosevu wa wataalam waliobobea katika masuala ya taaluma, uhaba wa vitendea kazi kama vile vitabu na maabara za kisasa. Kupitia changamoto hizi imepelekea nchi za kiafrika kuwa na wimbi kubwa la vijana walio tegemezi kutokana na ukosefu wa ajira pamoja na mbinu stahiki za kuwawezesha vijana kujiajiri ambapo sababu kubwa ni mifumo duni ya Elimu katika nchi nyingi za Afrika.

Sera bora na mifumo stahiki katika utumiaji wa Rasilimali za nchi; Ili nchi iweze kupata Utawala bora na uw ajibikaji lazima pawepo na sera bora katika utumiaji wa rasilimali zake, kupitia suala hili inaweza kuakisi aina ya utawala katika nchi husika.

Bara la afrika limebarikiwa na rasilimali za kila aina kama vile madini, mito, maziwa, ardhi yenye rutuba pamoja na wanyama pori wa kutosha lakini kutokuwepo mika kati mbadala katika utumiaji wa rasilimali hizi imepelekea kufujwa kwa rasilimali hizo na kupelekea kuwepo kwa matabaka ndani ya jamii za kiafrika ambapo watu wachache wameweza kujinufaisha na kusababisha kuibuka kwa migogoro mbalimbali katika nchi za kiafrika.

Migogoro mikubwa ambayo imepelekea vita ya wenyewe kwa wenyewe na kusababisha vifo vya mamia ya watu na kuongeza idadi kubwa ya wakimbizi katika nchi za kiafrika. Lakini pia kutokuwepo uwiano katika mishahara ya watumishi wa umma ambapo imepelekea baadhi ya nchi kuwa na viongozi wanaoishi kama Miungu watu kutokana na kujinufaisha wao wenyewe, hivyo basi uwepo wa sera bora katika utumiaji wa rasilimali za nchi pamoja na rasilimali watu huchagiza uwepo wa utawala bora na uwajibikaji katika nchi husika.

Uwepo wa Ushirikiano na Mshikamano baina ya Nchi moja na nyingne, Ili nchi iweze kujipambanua katika kuwa na utawala bora pamoja na uwajibikaji, lazima iweze kushirikiana na nchi nyingine ili kuweza kusaidiana katika kutatua na kuelekezana mambo mbalimbali ya kiutawala na kiuchumi. Lakini pia suala hili husaidia nchi moja kujifunza kutoka nchi nyingine na pia kupata nafasi ya kuakisi aina ya utawala iliyonayo una madhaifu gani na yarekebishweje.

Nchi nyingi za kiafrika zimeshindwa kupiga hatua katika suala la la Utawala bora na uwajibikaji kwa sababu hakuna mishikamano bora kati ya nchi moja na nyingine ambayo inaweza kusaidia kutatua matatizo mbalimbali yanayozikumba nchi za kiafrika kama vile, ukabila, udini, ubadhirifu mali za umma na ukoloni maomboleo, magonjwa, majanga ya ukame mfumuko wa bei katika bidhaa mbalimbali. Iwapo nchi zitaweza kusimamia ipasavyo suala hili maarufu kama diplomasia itasaidia kukua thamani ya pesa yao lakini pia kukomaa kwa utawala bora na uwajibikaji.

Kuthamini na kuimarisha Utamaduni na Mila za nchi husika, Inabidi ikumbukwe kuwa hakuna nchi ambayo iliweza kupiga hatua za utawala bora na uwajibikaji pasipo kuzingatia tamaduni na mila za nchi husika. Uwepo wa tamaduni na mila nzuri ndani ya taifa husaidia wananchi wake kuwa utu wa uzalendo na kuipenda pia nchi yao. Lazima suala hili liangaliwe katika muktadha wa hali ya juu.

Maadili, imani na mshikamano unajengwa kuanzia ngazi za chini kabisa katika jamii, hivyo bhas viongozi hawana budi kuhakikisha nchi zinaenzi na kuimarisha tamaduni nzuri ambazo zinaweza kusaidia katika kukumbusha vijana kujituma, kupenda kufanya kazi, heshima, nidhamu, unyenyekevu, busara, hekima katika kufanya maamuzi pamoja na upendo. Hivyo bhasi uwepo wa tamaduni bora ndani ya nchi husika inaweza kusaidia kupata kizazi chenye hekima na kupelekea uwepo wa Utawala bora pamoja na uwajibikaji, mfano nchi za magharibi zinapambana sana kulinda utamaduni wao kupitia vyombo vya habari, sanaa pamoja na elimu inayotolewa.

Ni vigumu sana kukuta majina kama Nyerere, Mandela, Kaunda hata Lumumba. Hawa ni baadhi ya vongozi shupavu walioweza kuonekana katika uso wa dunia na kufanya mambo makubwa katika dunia hii, lakini kwa kuwa hawakuwa watu wa magharibi hivyo bhas watu wa magharibi hawajataka kuwapa nafasi kubwa ili kuharibu tamaduni zao, Lakini kwa Afrika ni jambo la kawaida kukuta mtoto amepewa jina ambalo hajui hata maana yake na yule aliyempatia hajui maana yake lakini kwa sababu aliona mzungu fulani anaitwa hivyo na yeye akamwita mtoto wake pasipo kujua madhara ya kupoteza uthamani wa tamaduni zetu.
 
Back
Top Bottom