Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Taarifa mpya ninazowaletea leo ni kwamba CHADEMA wanapanga kufanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2020. Taarifa zilizovuja kutoka chanzo changu ndani ya Ufipa zinasema kuwa awali CHADEMA walikuwa na mpango wa kujaza tu nafasi zilizoachwa wazi na hasa nafasi ya Katibu Mkuu.
Hata hivyo, kutokana na kikao cha mashauriano ambacho kimefanyika juzi usiku nyumbani kwa Lowasa ambapo kimehudhuriwa na watu wazito wachache ndani ya CHADEMA kimeona kuwa kuna haja ya kufumua mfumo mzima wa uongozi ili kuweka watu ambao wanaamini kuwa watakivusha salama chama hicho katika kipindi cha kuelekea 2020. Watu wanaofikiriwa kujumuishwa kwenye safu ya uongozi ni wale waliomfuata Lowasa CHADEMA akiwemo Frederick Sumaye.
Chanzo changu ndani ya Ufipa ambacho hakijawahi kuniangusha kimenidokeza kuwa CHADEMA wana mpango wa kumchagua Edward Lowasa kuwa Mwenyekiti mpya wa chama hicho huku Freeman Mbowe anayeshikilia nafasi hiyo akiteuliwa kuwa Katibu Mkuu. Chanzo hicho kimesema kuwa maamuzi hayo ni kwa maslahi ya chama hasa ikizingatiwa uwezo na uzoefu wa Lowasa katika siasa za nchi hii.
Pia chanzo hicho kinasema kuwa muundo wa sasa haumpi Lowasa nafasi ya kufanya maamuzi ya chama na hivyo kuna haja ya kufumua mfumo mzima wa chama ili aweze kuwasimamia ipasavyo wabunge na madiwani waliochaguliwa kutokana na ushawishi wake. Chanzo hicho pia kimedokeza kuwa Lowasa anataka nafasi ya Uenyekiti ili aweze kusimamia ipasavyo Halmashauri walizoshinda UKAWA na hasa Ilala, Kinondoni, Mbeya na Jiji la Dar es Salaam ili ziongoze kwa ufanisi na hivyo zitumike kuwashawishi wananchi kumchagua mwanasiasa huyo katika uchaguzi mkuu wa 2020.
Taarifa zinasema kuwa Freeman Mbowe kwa ushawishi wa Mzee Edwin Mtei ameridhia mabadiliko hayo na kukubali nafasi ya Katibu Mkuu wa chama na hivyo kufuta kauli ya Tundu Lissu kuwa viatu vya Dk Slaa ni vikubwa na hivyo hakuna wa kuvivaa ndani ya CHADEMA. Jopo hilo linaamini kuwa Mbowe ni mtu pekee anaweza kufuta historia ya Dr Slaa ya utendaji ndani ya CHADEMA.
Aidha, kwa vile Katibu Mkuu ni Mtendaji wa Chama, wanaamini kuwa Mbowe atasimamia ipasavyo mikakati yote ya chama hususan mkakati wa kukusanya fedha kutoka Halmashauri wanazoongoza ambazo zitatumika kwa ajili ya uchaguzi Mkuu wa 2020.
Jukumu langu ni kuwahabarisha tu.