Kifurukutu
JF-Expert Member
- Aug 29, 2013
- 4,628
- 6,669
Hivi karibuni CCM kimefanya mabadiliko ya chama kwa ikiwa na lengo ya kuifanya CCM mpya na Tanzanania mpya
Lakini kwa hali halisi na uozo uliojaa katika katiba inayotumika kuendesha nchi hii ni ndoto ya mchana kweupe kuipata TANZANIA MPYA kwa kutumia katiba ya CCM
Katiba ya chama haiwezi kufanya mabadiliko yenye tija kwa mustakabhari wa taifa!
Sipingani na mabadiliko ya CCM ila ni vizuri haya mambo yawekwe wazi, kwamba bila katiba mpya ya JMT Tanzania mpya haiwezekani
Ni nini kinakwamisha mabadiliko ya katiba ya Jamhuri ya muungano, na kikawezesha mabadiliko ya katiba ndani ya CCm?
WanaCCM wanajua kuwa bila katiba mpya inayoendana na siasa za sasa maendeleo na kuendelea kumtawala mtanzania haiwezekani
Je hawalitambui hili kwamba Tanzania pia inahitaji mabadiliko kama wanayoyahitaji chamani?
Napenda kuwaasa na kuwakumbusha watanzania kwa ujumla, mabadiliko ya katiba ndani ya CCM tuyachukue na iwe chachu ya kuidai katiba mpya inayotokana na watanzania wote pasi kujali itikadi na mitazamo ya dini siasa, ukabila ubara na uzanzibar!
Tuungane kwa pamoja tuidai katiba mpya, imewezekana CCM kwanini isiwezekane tanzania nzima?