Mabadiliko Ya Dhati Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabadiliko Ya Dhati Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by zomba, Jul 17, 2011.

 1. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hakuna kuficha wala kutafuna maneno katika hili, kweli kabisa, mabadiliko ya dhati yanatakiwa Tanzania katika kila nyanja, hususan uongozi.

  Mabadiliko yanayotakiwa Tanzania ni katika uongozi wa nchi (Administration) na si mabadiliko ya chama fulani au watu fulani, la hasha. Leo Tanzania, mfumo wetu wa uongozi unawafanya wana siasa ndio waongoze nchi katika kila nyanja, nadhani hapo ndipo tunapokosea, na hii iwe kwa chama chochote kitachoingia madarakani mambo ni hayo hayo.

  Siasa na wanasiasa wabaki kuwa wanasiasa na wapiga porojo, no matter elimu na fani zao zilivyo. Mfumo mzima wa uongozi Tanzania hautegemei ujuzi wa mtu, hautegemei mapungufu anayoyaonyesha katika utendaji wala hautegemei nyadhifa anayoshika inataka iwe vipi?

  Unakuta waziri daktari anaongoza wanajeshi? hata JKT hajawahi kupitia. Huu ni mfano mmoja tu.

  Wanasiasa walikuwa wachaguliwe kuwa wanasiasa na wapige porojo za kisiasa. Badala ya kuwa na mawazori weeengi na wizara nyiiingi. Ziwepo wizara sita tu. Kusiwe na idara kibaaao kartika hizo wizara.

  Mamlaka yote ya kuendesha nchi kiutendaji yarudi majimboni, haina haja ya kuwa na mikoa kibaao na wakuu wa mikoa kibaaao. majimbo manne tu yanatosha Tanzania nzima.

  1) President awe anachaguliwa na si lazima awe wa chama fulani.

  2) Waziri mkuu ndio awe mtendaji mkuu akiendesha wizara 6 tu.

  3) Magavana wawe 4 kwa Tanzania nzima, na waongoze majimbo yao kwa ushindani.

  4) Badala ya mikoa tuwe na majimbo manne ambayo yatakuwa na mabunge yake. Wabunge ndio watakuwa wakuu wa wilaya zao. Kila jimbo liwe na wilaya zisizo zidi kumi na mbili na wote watakuwa wa kuchaguliwa hakuna wa viti maalum.

  5) Magavana wote watawajibika kwa majimbo yao kwa yote, magavana si lazima wawe wa chama fulani.

  6) Baada ya mabunge ya majimbo kutakuwa na Bunge kuu ambalo litahusisha wabunge wanne kutoka kila jimbo wakiongozwa na gavana wao. Kwa hiyo bunge zima halitozidi wabunge 30, mawaziri sita watakuwa wabunge automatic. Hakuna wabunge wa viti maalum.

  7) Kamati zote za bunge zitazokuwa formed zitahusisha watendaji wasio bungeni watu wenye fani zao na wenye sifa za kielimu na uzoefu katika fani zao. mbunge anaweza kuwa mwenyekiti tu wa kamati.

  Hayo ni machache tu, tuendelee....
   
 2. m

  muafaka Senior Member

  #2
  Jul 17, 2011
  Joined: Oct 30, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Bwana zomba mawazo yako mazuri sana, ninachitaka kuuliza mawazo hayo umeyapataje, nia yangu kuuliza ni njema tu ili tuwe na uhakika wa mapendekezo tunayoyatoa kwa viongozi wetu. Endapo ni mawazo binafsi how sure are we kwamba the ideas will work? Endapo mawazo hayo yanatokana na case study ya nchi nyingine ni masuala gani mengine yamelinganishwa ya nchi hiyo na nchi yetu, mfano historical background, mazingira ya kisiasa na kiuchumi n.k. Nijuavyo mifumo ya nchi mbalimbali hu-evolve kutegemea mqmbo mengi sana.mfano ni friction za kisiasa zilizopo nchini kwetu kwa sasa zitalazimisha wahusika katika nafasi mbalimbali kufikiri zaidi na kuboresha utendaji wa kazi kila mmoja katika eneo lake. The only thing I hate is violence. Otherwise thx for the post
   
 3. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Mkuu nakubaliana nawe kuwa mifumo tuliyo nayo ni moja chanzo kikubwa cha kustall kwa maendeleo ktk nchi yetu. Tumechelewa sana kutoka nje ya box... Tunahitaji kuwa na revolutionary leader atakayeweza kusimamia mabadiliko kama hayo. Tazama mfano...Mawaziri kutokana na wabunge - mawaziri wana kauli ya mwisho over technical people!! Viti maalumu - representing who?Wabunge zaidi ya 300 what for?Wakuu wa mikoa doing what Wakuu wa wilaya -they will teLl you wanasimamia usalama Mikoa inaanzishwa kama asante tuImagine wabunge waonatakiwa kuisimamia serikali ndio kwanza wanatumia fursa hiyo kwa kuisifia serikali hence wanateuliwa kuwa waziri spika etcKifupi mfumo tulionao kimsingi umekaa kisiasa zaidi ni mfumo tulioridhi toka kwa waingereza ambao waliuweka kwa lengo mahususi. Tunahitaji kuwa na mfumo ambao unalenga zaidi ktk ukuaji wa kiuchumi...maswala mazima ya kuendeleza rasilimali. Nakubaliana na mtoa hoja unakuta anybody can be a minister worse enough leo yuko kilimo kesho elimu keshokuwa afya...this is utter nonsense. Mbunge anakuwa waziri...tayari kuna conflict of interest ndio maana tunashuhudia mbunge tu wa kawaida anaitetea serikali kwa hoja ambayo imeuliwa na mbunge mwingine. Kifupi niseme mfumo tulionao unawafanya watendaji wawajibike kwa serikali na si kwa wananchi...this is completely wrong
   
Loading...