Mabadiliko Elimu ya Msingi: Mwisho kuwa darasa la sita

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,695
149,921
Gazeti la Mtanzania linaripoti katika ukurasa wa mbele habari ya mabadiliko elimu ya msingi ambapo kuna uwezekano wa elimu ya msingi kuishia darasa la sita huku masomo yakipunguzwa.

Chanzo: Mtanzania
 
Ni sharti la nchi moja ya ulaya nadhani Finland kama sijakosea inayotaka kutoa ufadhili wa elimu kuanzia chekechea hadi form four.

Ndio wanaolazimisha kama tunataka watufashili basi elimu ya msingi iwe mwisho darasa la sita kisha elimu ya msingi kwa ujumla iishie form four, kwamba kila mtoto anaeanza darasa la kwanza lazima afike form four. form six hadi chuo ni elimu ya hiyari.

Huo mpango waliiuintroduce kwa zanzibar miaka kadhaa iliyopita sijajua kama umeanza huko au la,nadhani pia ndio hao wanaotaka hayo mabadiliko yafanyike hata huko Tanganyika ili watoe ufadhili.

Hii nchi inafadhiliwa hadi elimu, sijui sisi tunaweza kujisimamia kwenye nini kama mambo ya msingi tu hatuwezi kujisimamia hadi tupate ufadhili.
 
Ni kweli sisi tanzania elimu yetu ni ndefu sana.
Kwa mfano kama zambia sisi tuko mbele mwaka mmoja kielimu. nao kenya sisi tupo mbele miaka miwili kielimu.
 
Haya maamuzi ya mtu mmoja huwa yanafanyika kutokana na tafiti ambazo zimefanywa na wataalamu na wadau? mbona inakuwa ghafla, Msimu wa matamko mwaka mpya umeshaanza rasmi.
 
Tuta mkumbuka Mwl.Nyerere,Mwinyi enzi zao..na elimu bora sio bora elimu
Hatuna misingi ya nchi tunaenda kama gari bovu..kila kiongozi akija anafumua hiki ana aanza yake
 
Tueleze anayetaka kuleta hayo mabadiliko,Je ni waziri wa elimu,au ni jopo la wanazuoni waliofanya utafiti.Kama ni waziri sikubaliani lakini kama ni mfumo yaani wadau wameshirikishwa ktk utafiti naunga mkono
 
Gazeti la Mtanzania linaripoti katika ukurasa wa mbele habari ya mabadiliko elimu ya msingi ambapo kuna uwezekano wa elimu ya msingi kuishia darasa la sita huku masomo yakipunguzwa.

Chanzo: Mtanzania
Ni kwel mkuu mwaka jana baadhi ya walimu walipelekwa semina september/october kwa ajili ya hayo mabadiliko na wakaambiwa hakutakua na mitihan ya kumaliza shule ya msingi,ukimaliza la sita unaunganisha form 1 hadi form four. Sasa hyo elimu sijui itakuaje..
 
Wizara ambayo ni kichwa cha mwenda wazimu Tanzania ni Wizara ya Elimu, ndipo kila wajiitao wasomi wanakojifunzia. Tunachezea elimu, tumeshaona athari zake na bado mbaya zaidi zinakuja!
 
Ni sharti la nchi moja ya ulaya nadhani Finland kama sijakosea inayotaka kutoa ufadhili wa elimu kuanzia chekechea hadi form four.

Ndio wanaolazimisha kama tunataka watufashili basi elimu ya msingi iwe mwisho darasa la sita kisha elimu ya msingi kwa ujumla iishie form four, kwamba kila mtoto anaeanza darasa la kwanza lazima afike form four. form six hadi chuo ni elimu ya hiyari.

Huo mpango waliiuintroduce kwa zanzibar miaka kadhaa iliyopita sijajua kama umeanza huko au la,nadhani pia ndio hao wanaotaka hayo mabadiliko yafanyike hata huko Tanganyika ili watoe ufadhili.

Hii nchi inafadhiliwa hadi elimu, sijui sisi tunaweza kujisimamia kwenye nini kama mambo ya msingi tu hatuwezi kujisimamia hadi tupate ufadhili.
Lakini inaweza kuwa sawa tu 6:4:2:3or 4

Wakati Kenya wana 8:4:4 kawaida..

Inawezekana lakini kitu cha kwanza tungeanza kubadiri lugha ya kufundishia ni tatizo yaani Kijana anamaliza form 4 mweupe kabisa hawezi zungumza lugha ya kingereza?

Elimu yetu ilitakiwa itumie kingereza kuanzia nursery school.
 
Back
Top Bottom