Mabadiliko CCM kuwang'oa mafisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabadiliko CCM kuwang'oa mafisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sumasuma, Feb 14, 2012.

 1. sumasuma

  sumasuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 14, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 331
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  KINGUNGE ADAIWA KUPINGA, ASEMA HAYALENGI KUBORESHA MFUMO WA CHAMA
  Midraji Ibrahim, Dodoma
  SIKU moja baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kupitisha mabadiliko ya Katiba ya mwaka 1977 juu ya namna ya kuwapata wajumbe wa Halmashauri Kuu (NEC), imeelezwa kuwa mabadiliko hayo yanatarajiwa kuwa kitanzi kwa watuhumiwa wa ufisadi ndani ya chama hicho tawala kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

  Juzi, Nec ya CCM ilibariki mabadiliko muhimu ya katiba ya chama hicho kuelekea uchaguzi wa ndani ambayo ni pamoja na kuanzisha utaratibu ambao wajumbe wa NEC waliokuwa wanatoka mikoani, sasa watakuwa wanachaguliwa kutoka wilayani na wabunge, wawakilishi na madiwani sasa hawataruhusiwa kushika nyadhifa za chama.

  Katika marekebisho hayo, viongozi wakuu wastaafu wakiwamo Marais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Marais wa Zanzibar na makamu wenyeviti wa chama hicho, wameundiwa Baraza la Ushauri na sasa hawatakuwa wajumbe wa NEC.

  Hata hivyo, uamuzi huo umepingwa vikali na baadhi ya wajumbe ambao walisema marekebisho hayo hayana tija zaidi ya kutaka kudhoofisha upande mmoja ambao uko kwenye harakati za urais mwaka 2015 na kuutaja kwamba, ni genge la watuhumiwa wa ufisadi.

  “Wamejaribu kuondoa wazee wastaafu ili Kamati Kuu isiwe na watu ‘strong’, lakini yote hayo yanalenga kwa mtu siyo mfumo. Chama kinatakiwa kufanya marekebisho yake kwa mfumo siyo mtu... ngoja twende tutaona itakavyokuwa,” alisema mjumbe mmoja wa NEC ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.

  Mjumbe mwingine ambaye pia hakutaja kutambushwa jina lake gazetini alisema uamuzi huo wa kurejesha nafasi hizo wilayani, unalenga kuwazuia baadhi ya watu wasiingie katika vikao hivyo vya uamuzi na kuwazuia watuhumiwa wa ufisadi kuweka watu wao katika wilaya zote nchini hata kama wana fedha.

  Alisema hata kama watuhumiwa wa ufisadi wana fedha nyingi, itakuwa vigumu kwao kuweza kupandikiza watu wao katika wilaya zote nchini.

  “Kwa hiyo sasa hivi angalau kutakuwa na mkakati wa kuhakikisha mafisadi hawaweki watu wao wengi wilayani. Kwani itakuwa vigumu kumudu kuweka wajumbe wa NEC wilaya zote nchini, lakini pia, wao wenyewe itawawia vigumu kupenya.”

  Mwishoni mwa mwaka jana, mpango wa kujivua gamba ndani ya CCM uligonga ukuta katika kikao cha NEC hatua ambayo ilimfanya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete kutumia busara na kurejesha utekelezaji wa mpango huo kwenye Kamati Kuu (CC) kwa utekelezaji.

  Kingunge apinga
  Hata hivyo, taarifa kutoka ndani ya kikao hicho zilieleza kuwa, kada mkongwe wa chama hicho, Kingunge Ngombale-Mwiru, ndiye mjumbe pekee aliyepinga marekebisho hayo, huku akiituhumu sekretarieti kwa kukiuka katiba ya chama hicho.

  Kingunge anadaiwa kuwatuhumu Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama kwa kuvunja katiba hiyo kutokana na Halmashauri Kuu kutokuwa na uwezo wa kupitisha marekebisho hayo zaidi ya kupendekeza kwa Mkutano Mkuu ambao ndiyo wenye mamlaka hayo.

  "Mzee ametueleza wazi kabisa kwamba marekebisho hayo hayana maudhui zaidi ya kumlenga mtu mmoja, aliuza sekretarieti imepata wapi kwamba Halmashauri Kuu ina uwezo wa kufanya marekebisho haya?,” alisema mtoa habari hayo.

  Lakini, katika utetezi wake, Sekretarieti ilisema kuna kifungu kinachotoa mamlaka hayo kwa NEC kupitisha marekebisho hayo na kutoa taarifa kwa Mkutano Mkuu. Hata hivyo, Kingunge hakukubaliana na hoja hiyo.

  Ilielezwa pia kwamba marekebisho hayo yaliyopitishwa kwa kupigiwa kura na wajumbe kwa kupata theluthi tatu kutoka Tanzania Bara na nyingine tatu kutoka Visiwani, wote walikubali isipokuwa Kingunge pekee.

  “Ila tulichojifunza kwa Mzee (Kingunge) ni kwamba lazima utetee unachokiamini hadi mwisho na alimtaka Katibu Mkuu kuandika kuwa amepiga kura ya hapana ili iwe kwenye kumbukumbu,” chanzo chetu kilieleza.

  Hata hivyo, Kingunge alipotafutwa jana kwa simu kufafanua msimamo wake hakutaka kuzungumza chochote akisema kwamba alikuwa kikaoni...”Samahani niko kwenye kikao, asante.”

  Yapokea taarifa ya Katiba Mpya

  Katika hatua nyingine, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amesema Nec imepokea taarifa ya mchakato wa mabadiliko ya Katiba ya Tanzania na kuridhishwa na hatua iliyofikiwa lakini ikaitaka Serikali kuendelea kutoa elimu kwa wananchi, huku akitaka wanachama wao kujitokeza kutoa maoni pindi tume itakapoundwa.

  Nape alisema mjadala ulikuwa iwapo Tume ya Maadili iundwe au la lakini kutokana na katiba kuruhusu kuundwa kwa tume mbalimbali wajumbe walikubaliana iundwe.

  Aidha, alisema Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alitoa taarifa ya mgomo wa madaktari na wajumbe waliitaka Serikali kuharakisha makubaliano yaliyofikiwa na iwe inachukua hatua kabla ya migomo kusababisha madhara kama ilivyotokea.

  Uchaguzi Mdogo Arumeru
  Alisema NEC imetoa ratiba ya mchakato wa kumpata mgombea wa CCM kwenye uchaguzi mdogo Jimbo la Arumeru Mashariki na viti vinane vya udiwani vilivyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

  Kwa mujibu wa ratiba hiyo, utaratibu utakaotumika katika nafasi ya ubunge ni ule wa kura za maoni kwenye mkutano mkuu wa jimbo na kwamba Februari 13 hadi 18 wagombea watachukua na kurejesha fomu. Februari 20, mkutano mkuu wa jimbo utapiga kura na kesho yake, kamati ya siasa ya Wilaya ya Arumeru itajadili wagombea na kutoa mapendekezo kwa Kamati ya Siasa ya Mkoa ambayo itakutana Februari 24 na kutoa mapendekezo kwa Kamati Kuu ya CCM ambayo itakutana Februari 27.:A S 465:
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Feb 14, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  wataje majina ya nani ccm asiye fisadi?
   
 3. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #3
  Feb 14, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  J.k ni noma,wenye akili tumeelewa anakusudia nini,kweli Rais ajae anamjua,Lowassa sasa aongeze bajet yake ya Urais wilaya zote kuupata Urais,au amtafute best yake Rostam watengeneze ka EPA walau ka bilion 50 ili wakabiliane na hili la mdororo wa kisiasa!!
   
 4. m

  mharakati JF-Expert Member

  #4
  Feb 14, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  naona unamchukulia Lowassa kisivyo kabisa bil 50 tsh ni nini? jamaa ana uwezo mkubwa wa kuziweka mezani hizo 50 peke yake bila ya Rostam wala Mkono na washirika wengine..nafikiri vita ikitanganzwa kabisa atakuja na 150 bil tsh yaani pungufu kidogo tu ya 100m usd
   
 5. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #5
  Feb 14, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mabadiliko haya yanaweza kumgharimu JK mwenyewe kabla hata hajamaliza muda wake.. ngoja tuone..
   
 6. m

  mharakati JF-Expert Member

  #6
  Feb 14, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  ufisadi siyo kama dini yaani dhambi ni dhambi yaani kubwa na ndogo mbele ya dini zote ni sawa.ufisadi katika uongozi na miiko yake una grade zake kuna ufisadi mkubwa unaopoteza pato la taifa na tija ya kufanya kazi na uzalishaji na ufisadi mdogo yaani watalaam wanasema high level corruption (with high impact on society) na low level corruption (with less impact on society). Mheshimiwa mmoja akisaini mkataba wa kinyonyaji kwa sababu yeye binafsi anapata kitu ni ufisadi mkubwa na hasara kwa taifa na jamii yote inakosa wakati mheshimiwa mwingine akifanya kapati pale kempinski kwa gharama za ofisi ni ufisadi mdogo usiokua na impact kubwa kwa taifa na katika muda mfupi unaweza usiathiri jamii kwa sababu hautadumaza uzalishaji kitaifa...sasa kama wote ni mafisadi na hamna aliye msafi sisi tunafikiri kigezo kitakua viwango vya ufisadi na hapo wale mafisadi wakubwa hawatokua viongozi wetu wa kitaifa.
   
 7. m

  mharakati JF-Expert Member

  #7
  Feb 14, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  laikini kama unataka jibu jepesi la swali lako kwa sababu ya uvivu wa kufikiri au la..basi Mh Membe, mh.Sumaye, Dr Migiro, Prof Tibs, Dr Shein, Salim A Salim, Prof Mwandosya, Dr Mwakyembe, Mh Pinda, Mh Warrioba, Prof Sarungi, Mh Mukama, kijana Nnauye, Mh Nundu, hawa ni notables tu ila wapo wengi katika ngazi mbali mbali za chama
   
 8. satellite

  satellite JF-Expert Member

  #8
  Feb 15, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Patachimbika kama ndo anaanza kumzuzia EL kwa stairi hiyo
   
 9. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #9
  Feb 15, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu una hakika unachokinena?
   
Loading...