Maazimio ya ACT wazalendo kuhusu zanzibar.

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
20,054
23,505
12729041_1121442707865864_6954632606889229961_n.jpg


CHAMA CHA ACT-WAZALENDO
NACHO CHALIZIA BUNDI
UCHAGUZI WA MARUDIO WA
ZANZIBAR.
Kamati Kuu ya Chama cha siasa
cha ACT-Wazalendo imekutana
kwa kikao cha dhahura ambapo
pamoja na mambo mengine
imejadili hali ya kisiasa ya
Zanzibar na kuazimia kama
ifuatavy;
i. Kupinga marudio ya uchaguzi
uliopangwa kufanyika tarehe 20
Machi 2016, na kwamba Chama
chetu cha ACT-Wazalendo
hakitashiriki katika uchaguzi huo
kama utaendelea kama
ulivyopangwa.
ii. Kutoa wito maalumu kwa Rais
wa Jamhuri wa Muungano wa
Tanzania kuchukua hatua stahiki
za kiuongozi katika kumaliza
mkwamo wa kisiasa Zanzaibar, na
kuacha kutoa vitisho vya kidola
katika kushugulikia tatizo hili.
Kamati Kuu imemtaka Rais
Magufuli kutumia mamlaka
aliyepewa kikatiba kuhakikisha
kwamba Umoja na Amani ya Taifa
inaendelea kuimarika nchini kwa
kuzingatia misingi ya demokrasia,
utawala wa sheria na utawala
bora.
iii. Kamati kuu ya ACT-Wazalendo
inahimizi kuwa madiwani na
wawakilishi walioshinda na
kutangazwa rasmi na ZEC katika
uchaguzi uliofanyika Oktoba
25/2015 watambuliwe na waanze
kuwatumikia wananchi.
iv. Kamati Kuu imeendelea
kuhimiza wadau wote muhimu
katika siasa za Zanzibar
kuendelea kufanya mazungumzo
katika kutatua mkwamo wa
kisiasa.
Kamati Kuu haiamnini kwamba
suluhu ya kudumu kuhusu
changamoto za kisiasa Zanzibar
zitapatikana kwa ubabe na
matumzi ya nguvu za kidola.
Chanzo : Mwandishi Wetu.
 
Back
Top Bottom