Maaskofu wataka JK awajibishe mawaziri 4 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maaskofu wataka JK awajibishe mawaziri 4

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Oct 3, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 3, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,854
  Likes Received: 83,337
  Trophy Points: 280
  Maaskofu wataka JK awajibishe mawaziri 4 Saturday, 03 October 2009 11:40 *Ni Kawambwa,Wasira, Masha na Kapuya
  *Kama hawataondolewa watawakataa 2010

  Na Benjamin Masese
  Majira

  MAASKOFU na wachungaji 25 kutoka makanisa mbalimbali nchini wamemtaka Rais Jakaya Kikwete kuwawajibisha mawaziri wake wanne ambao wamedai, wameshindwa kutekeleza wajibu wao na kutishia kuwa asipofanya hivyo, watahamasisha waumini wao kutowapigia kura viongozi hao katika Uchaguzi Mkuu ujao mwakani.

  Mawaziri waliotajwa na wizara zao katika mabano ni, Dkt. Shukuru Kawambwa (Miundombinu), Bw. Stephen Wasira (Chakula na Kilimo),Bw. Lawrance Masha (Mambo ya Ndani ya Nchi) na Profesa Juma Kapuya (Kazi Ajira na Maendeleo ya Vijana).

  Wakizungumza katika shamba la Rais Jakaya Kikwete walilotembelea wilayani Bagamoyo juzi, maaskofu hao walidai mawaziri hao wanatia doa serikali na kuonekana kuwa ina upungufu katika katika utendaji wake.

  "Rais ana muongozo mazuri lakini sasa watendaji wake ndio wanaosababisha anaonekane analegalega ingawa naye ana upungufu katika ucheleweshaji wa kutoa majibu yanayohusu masuala magumu yanayolikabili taifa kama mambo yanayoendelea sasa visiwani Zanzibar," alisema Askofu Thomas Faida wa Kanisa la Pentecoste Assemblies of God Shinyanga.

  Walifafanua kuwa Waziri Kawambwa ameshindwa kusimamia shughuli za Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) na kumuachia mwekezaji kufanya jambo lolote analotaka huku akiwadanganya wananchi kuwa kuna mazungumzo yanayoendelea katika ya serikali na mwekezaji huyo.

  Kuhusu Prof. Kapuya walidai amekuwa kimya katika wizara yake badala ya kutafuta mbinu mbadala za kupunguza ombamomba mitaani na vijana wanaoishi katika mazingira magumu ambao wizara yake inahusika .

  Walimlalamikia Waziri mwingine Bw. Masha na kudai kuwa amekuwa akilegalega katika mradi wa vitambulisho vya utaifa na hoja iliyozua malumbano katika Mkutano wa 16 wa Bunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano jambo walilodai ni hatari kwa taifa.

  Maaskofu hao ambao walifika kujionea jinsi Rais Kikwete anavyofanya shughuli zake binafsi kama kilimo, walifurahishwa na shamba lake linalotumia mbolea ijulikanayo kama 'Earth Food'kutoka Marekani na kusambazwa nchini na Kampuni ya TIGI Internation Ltd.

  Shamba hilo lenye hekari 25 ambalo limepandwa minanasi, migomba pamoja na minazi lipo katika Mkoa wa Pwani Wilaya ya Bagamoyo kata ya Kiwangwa.

  Maaskofu haoa wamemtaka Waziri wa Kilimo na Chakula Bw. Wasira naye kujizulu wadhifa wake baada ya kushindwa kujifunza jinsi ya utumiaji wa mbolea kutoka katika shamba hilo na kutoa elimu kwa wananchi. Walisema Bw. Wasira amekuwa akitoa elimu ya kutumia mbolea ya chumvi chumvi yenye kemikali kali zinazoua rutuba katika ardhi na kusababisha njaa katika mikoa 17.

  Walisema waziri huyo anapaswa kujua mbolea inayotumiwa katika shamba la Rais Kikwete ndiyo mkombozi wa wakulima wa Tanzania kwa kuwa inatengenezwa kwa kutumia taka za shamba zisizo na kemikali.

  Akizungumza kwa niaba ya wachungaji wenzake Mchungaji William Mwamalanga wa shirika la Forestry and Enviromental Conservation Association (MRECA), alisema lengo la ziara hiyo ni kujifunza namna mbolea hiyo inayotumika katika shamba hilo.

  Mchungaji Mwamalanga alisema hawaafiki hatua ya kusambaza mbolea ya chumvichumvi mikoani hivyo wanaandaa maandamano nchi nzima kupinga matumizi ya mbolea hiyo pamoja na kudai fidia kwamadhara yatokanayo na mbolea hiyo.

  Alisema kuwa wanahitaji kuonana uso kwa uso na Rais Kikwete ili kutoa sababu za msingi juu ya mbolea hiyo huku wakisisitiza athari kubwa ya uingizaji na usambazaji wa mbolea hiyo kwa mkulima na mazingira.

  Wakizungumzia siasa nchini walidai kuwa kuna utata ulioibuka kati ya wanasiasa na dini hivyo wameahidi kufanya mdahalo nchi nzima kati ya wanasiasa na dini zote ili kutofautisha vitu hivyo.

  Naye Mchungaji wa Kanisa la Christ to All People lililopo Dar es Salaam, Onesmo Mwakyambo alisema kuhusu matumizi ya mashangingi navazi la suti lililokemewa na Waziri Mkuu Bw. Pinda hivi karibuni, yeye mwenyewe anapaswa kuonesha mfano kwa kuanza kutumia gari la kawaida badala ya mashangingi.

  "Hakuna maana yoyote kukataa kitu kwa wengine kisha unakitumia wewe,mbona hajafanya msafara na bajaj au teksi ili awe mfano kwa wenzake? Alihoji Mchungaji Mwakyambo.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Wanajishaua tu hao maaskofu.ni shembenduzi tu hizo.
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Oct 4, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,772
  Trophy Points: 280
  *Ni Kawambwa,Wasira, Masha na Kapuya

 4. O

  Omumura JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Cha muhimu aanze na ndugu yake kipenzi Kawambwa!yaani huyo jamaa ameshajichokea lakini hataki kumtema ila kumbadilisha kila siku wizara while he is underperforming!waziri mzima hata kujieleza ni issue.
   
Loading...