Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,933
Idadi kubwa ya vyuo mbalimbali vikiwemo vya ufundi na ualimu vimejengwa na kanisa. Hospitali mbalimbali na zahanati zinaendeshwa na maaskofu. Miradi mbalimbali ya umeme vijijini imeanzishwa na kuhudumiwa na maaskofu.
Viongozi wengi hapa nchini wamesoma katika shule na vyuo vilivyojengwa na kanisa.
Nashangaa leo CCM ikisema maaskofu wavue majoho maana yake wafunge shule, vyuo, hospitali, dispensary, nk
mkuu uzi wako uko na utata.............
sasa kwa mfano kama mimi nikiuliza: mashehe na maimamu wamejenga nini? utanijibu nini?
kumbuka mkuu kuwa roho inakaa kwenye mwiliNafikiri kuna sababu kubwa ya kuuwambia wasiingilie siasa, kwani wao wana ushawishi mkubwa wa kiroho na mtu yuko tayari kufa kwa imani yake ya kiroho kuliko kufa kwa ajili ya CCM au CHADEMA kwani hivi ni vikundi vya mpito tu leo vipo kesho havipo. Ndio maana nchi zote za Demokrasia watu wa dini wanawekwa pembeni washughulikie wafuasi wao kiroho, kama wanataka kuingia kwenye siasa inawabidi waache kimoja.
Taasisi za kidini zinapewa upendeleo wa kodi kwa ajili ya hili. Sasa kweli wakijiingiza na kuanza kutoa matamshi yasiyokuwa neutral nchi inaweza ikawaka moto, kwani wakijibiwa wasijifanye kwamba hawewezi kukosolewa, nchi itagawanyika kwani Waislamu kamwe haitawaona kuwa wako kupigania interest zao. Tusijidanganye kila mtu anajua viongozi wote wa dini wanataka upande wao ndio uwe mbele awe mkristo au muislamu, sasa awa maaskofu wasipokuwa makini tutageuka Lebanon... Ndiyo maana Nyerere licha kuwa mkatoliki mzuri lakini hakuwaachia maaskofu na mashekhe kuzungumzia siasa na aliondoa sensa ya idadi ya wakristo na waislamu tangu 1967 kwa kuona mbali. Sasa watu wasiokuwa na busara wanataka kuliamsha zimwi ambalo litaiangamiza Tanzania wasipotumia akili. Maaskofu na Mashekhe wanatakiwa kuwa waleta amani katika jamii na sio kuchochea uhasama kutokana na kutofautiana kimau .
huyo anayesema maaskofu wasiingilie mambo ya siasa , kwa nini NEC iliwapa kazi ya kisiasa kutoa elimu ya uraia wakati wa uchaguzi 2010 ???
Nafikiri kuna sababu kubwa ya kuuwambia wasiingilie siasa, kwani wao wana ushawishi mkubwa wa kiroho na mtu yuko tayari kufa kwa imani yake ya kiroho kuliko kufa kwa ajili ya CCM au CHADEMA kwani hivi ni vikundi vya mpito tu leo vipo kesho havipo. Ndio maana nchi zote za Demokrasia watu wa dini wanawekwa pembeni washughulikie wafuasi wao kiroho, kama wanataka kuingia kwenye siasa inawabidi waache kimoja.
Taasisi za kidini zinapewa upendeleo wa kodi kwa ajili ya hili. Sasa kweli wakijiingiza na kuanza kutoa matamshi yasiyokuwa neutral nchi inaweza ikawaka moto, kwani wakijibiwa wasijifanye kwamba hawewezi kukosolewa, nchi itagawanyika kwani Waislamu kamwe haitawaona kuwa wako kupigania interest zao. Tusijidanganye kila mtu anajua viongozi wote wa dini wanataka upande wao ndio uwe mbele awe mkristo au muislamu, sasa awa maaskofu wasipokuwa makini tutageuka Lebanon... Ndiyo maana Nyerere licha kuwa mkatoliki mzuri lakini hakuwaachia maaskofu na mashekhe kuzungumzia siasa na aliondoa sensa ya idadi ya wakristo na waislamu tangu 1967 kwa kuona mbali. Sasa watu wasiokuwa na busara wanataka kuliamsha zimwi ambalo litaiangamiza Tanzania wasipotumia akili. Maaskofu na Mashekhe wanatakiwa kuwa waleta amani katika jamii na sio kuchochea uhasama kutokana na kutofautiana kimawazo kidini au kisiasa .
kumbuka mkuu kuwa roho inakaa kwenye mwili
Tunapowaongelea maaskofu tujaribu kuelewa sana kazi zao, Maskofu wanaiongoza na kuihudumia jamii Kiroho na Kimwili maana Huwezi kutenganisha mwili na roho.
Hivyo wanayo haki ya kuikemea serikali maana Nchi ya MUNGU na serikali huwekwa na MUNGU. Na ukiingia ndani zaidi Rais au kiongozi yeyote wa serikali yu chini ya uangalizi wa viongozi wa kidini. Ndiyo maana machifu na watemi zamani hawakufanya jambo lolote bila baraka za ma priest vinginevyo mambo yalienda ovyo.
Nadhani kwa kuanza CCM wasingemteua mama Lwakatare kuwa mbunge.