Maaskofu wahofia hatima ya nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maaskofu wahofia hatima ya nchi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Candid Scope, Apr 23, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Askofu Ruwa’ichi alilia na haki
  Kwa upande wake, Ruwa’ichi ambaye ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza, alisisitiza umuhimu wa Serikali na dola kutoa haki kwa umma akisema: “Siyo lazima kelele ya wengi inaporindima ndiyo haki inatendeka.”

  Akihubiri kwenye ibada hiyo iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Epifania, Parokia ya Bugando, Askofu Ruwa’ichi alisema kila mmoja anawajibika kusimamia ukweli ili kuungana na Kristo katika kutenda haki.

  Alisema watendaji wa Serikali wanapaswa kujihoji ni kwa kiasi gani wanatimiza mapenzi ya Mungu katika kuwatendea wenzao haki.

  Rwaichi alihoji ni mara ngapi watu waliopo katika dola wamenawa mikono yao ili kutoa haki dhidi ya wanyonge. Aliwataka kumrudia Kristo kujutia dhambi zao ili watakasike.

  Alikemea tabia ya baadhi ya watu kufanya mambo kisha kuwatwisha mzigo wengine ili kuokoa roho zao na kwamba tabia hiyo ni kinyume na Kristo ambaye hakuwa kigeugeu katika uamuzi wake.

  “Ulimwengu wa leo umebadilika tunapofanya makosa tunatafuta njia za kuwatupia watu wengine mizigo ili kunusuru roho zetu huo siyo mfano ambao tulionyeshwa na Kristo,” alisema Ruwa’ichi.

  Mapema katika mahojiano na gazeti hili, Askofu Ruwa'ichi, alisema Watanzania wana wajibu wa kudumisha amani na kukwepa kila aina ya dalili zitakazoweza kuivuruga.

  Source: Mwananchi
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hawa mafisadi waliomweka Kikwete madarakani wametoswa na kutwishwa zigo la kashfa yote baada y Kikwete kunufaika. Hili limekaaje?
  :kev:
   
 3. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kweli Candid, eti Lowassa anakuja tuhumiwa na ufisadi baada ya Kikwete kuingia ikulu, haingii akili kuwa waziri mkuu anaiba...
   
 4. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #4
  Apr 23, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kwa nini wasiwaite tu huko kanisani hawo akina lowassa na chenge ili wawaeleweshe vizuri kuliko kila kukicha kuongelea pembeni lakini wakiwa uso kwa uso wanawaogopa? If they are real serious wawaite na wawakanye ikiwa ni pamoja na kuwaambia kile walichoiba wakirudishe kwani bano wanacho. Otherwise, they are a day day dreamers.
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nabii ni sawa na mpanzi humwaga mbegu zake shambani, nyingine huangukia kwemye mwamba huota na kwa kuwa hakuna mizizi hudhoofika na kukauka, nyingine huangulia kwemye miiba husongwa songwa na hutoa matunda dhaifu, na nyingine huangukia kwenye udongo mzuri wenye rutuba hukua na kutoa matunda mazuri.

  Mvua inaponyesha haichagui nyumba, shamba au sehemu, bali hunyesha nchi nzima, na kama hukulima na kupanda mimea ni kosa lako lakini aliyejiandaa na kupanda mbegu atafurahia kuvuna alichopanda.

  Ngwendu umepata ujumbe huo???????????
   
Loading...