Maaskofu 'wagombea' waraka wa Mtikila | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maaskofu 'wagombea' waraka wa Mtikila

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, May 28, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,437
  Likes Received: 22,352
  Trophy Points: 280
  MAASKOFU waliohudhuria mkutano wa siku moja wa Jukwaa la Wakristo, juzi walifanya kazi ya ziada kupata nakala ya waraka ulioandaliwa na mwenyekiti wa Chama cha Kidemokrasia (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, ambaye alitumia mkutano huoo kuusambaza.

  Mkutano huo ulikuwa wa kuzindua chombo hicho kikubwa cha mshikamano baina ya Wakristo, lakini Mchungaji Mtikila, ambaye anaongoza kanisa la Full Salvation, aliutumia kugawa takriban nakala 60.
  Alikuwa akigawa waraka ambao ulisababisha polisi kuvamia nyumba yake iliyo Mikocheni na kufanya upekuzi kabla ya kuondoka na mwanasiasa huyo ambaye pia ni kiongozi wa kiroho na kwenda kumuhoji kituo cha polisi kwa saa kadhaa zaidi ya mwezi mmoja uliopita.

  Waraka huo wenye kurasa 24 ambao Mwananchi ina nakala yake, unazungumzia harakati za kuwaamsha waumini wa dini ya Kikristo kuamka kutetea dini yao dhidi ya utawala wa sasa ambao mchungaji huyo anautuhumu kuwa unawabagua.

  Waraka huo pia unawataja watu mbalimbali, kuanzia Rais Kikwete, viongozi wengine wa kisiasa na watu maarufu ukiwahusisha na tuhuma mbalimbali kubwa.
  Maaskofu kadhaa walionekana kumfuata Mtikila ili kupata nakala ya waraka huo ambao mchungaji huyo alikuwa amebeba nakala zake kwenye mkoba wa mkononi.

  “Nilikuja na nakala chahe sana... 60 tu, zikaisha na wengine wakawa wanautaka tena," alisema Mtikila mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kuzindua chombo hicho ambacho kazi yake kuu itakuwa ni kutetea haki za Wakristo.

  "Nimegawa hapa kwa sababu viongozi wenyewe waliutaka ndiyo nikaona niwape; nisiwe mchoyo,” alisema Mtikila.

  Mtikila alisema kuwa kuzinduliwa kwa jukwaa hilo ni kuzaliwa kwa tatizo kubwa kwa Rais Jakaya Kikwete na kumtaka ajihadhari, akidai kuwa ajira yake sasa ipo kwenye "danger zone (sehemu ya hatari).”
  Mtikila, ambaye ana ujasiri wa kutoa kauli zisizo na simile, alisema jukwaa hilo ni gharika kubwa kwa Rais Kikwete kwa sababu alizodai kuwa kiongozi huyo wa nchi ni adui mkubwa wa Ukristo.

  “Wakristo nchini tupo milioni 27 hivyo ajira ya JK hivi sasa ipo shakani," alisema.
  Viongozi wa makanisa ambayo yalishirika katika kuunda jukwaa hilo ni pamoja na Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (Tec), Jumuiya ya Makanisa ya Kikristo (CCT) na Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste (PCT).
   
 2. M

  Makanyagio Senior Member

  #2
  May 28, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mwenye nao atuwekee tafadhali
   
Loading...