Maaskofu ndio wasaliti

viongozi wa kanisa wana wajibu wa kuwaelimisha waumini wao kimwili na kiroho...ndo maana makanisa yaliyokamilika yanajenga na mashule na mahospital pia, vinginevo yangejikita kujenga makanisa tu yasingepata mafanikio yalionayo kiroho. sioni shida kwa viongozi wetu kutupa mwanga katika tusiyoyajua
 
Walikwepo Mjengoni walijadili mwanzo mwisho, sasa kulikoni. WTZ inatupasa kuelewa Bin Adam ye yote siyo Maaika. Makundi yalijadili mapendekezo ikaja katiba inayopendekezwa, sasa tuisome kwanza ndipo tuamuwe, pole sanaaaa wewe unataka kubebewa Akili na maamuzi.
 
Eti Roman Catholic!......ni kati ya maneno magumu mno kuyatamka ikiwa kwa kujitambulisha au chochote kile, as a matter of fact nilishafuta kwenye akili yangu hii kitu,watu weusi tuna shida kubwa sana ambayo sijui kama tutakuja kujitambua...!!
 
Hii ni imependekezwa, haijalitishwa. Kwa kura ngapi imepitishwa. Tusikurupuke tuisome kwanza tielewe nzuri lipj, baya lipj, ukisha ifahamu toa maamuzi yako. Usikubali kubebewa Akili KTK Uamuzi wako,
 

Mbona Viongozi wa Serikali walitoa wito tupige kura za NDIO? Hao hawajakukera?
 
Jibu unalo, Waserikali sio Wading!!!!!!! Pia kumbuka makundi yaliyo shiriki kupendekeza katiba, Wanasiasa wa Ukawa ndo waliona maslahi yao yatakuwa madogo wakasusa sasa Viongozi wamakanisa wanatoka kundi gani? Na wao CDM? NCCR CUF nk wasijifiche.
TANZANIA AMANI KWANZA, TANZANIA KWANZA, UMOJA KWANZA, UPENDO KWANZA, MSHIKAMANO KWANZA.
 
Kama ndio hivyo wewe huna haja ya kwenda kanisani kwa sababu unajua kila kitu na huna haja ya kuongozwa!

 

Mbona Viongozi wa Serikali walitoa wito tupige kura za NDIO? Hao hawajakukera?

Wewe kweli kiazi.. ni vigumu kuelewa.. swali gani hilo!?
 

Serikali ndio inayokusanya kodi na kupanga matumizi yake, walipanga kutumia kiasi cha pesa kilichotumika kwenye mchakato wa katiba mpaka kukamilika kwake, itakuwa ni kitu cha ajabu serikali kusema pigieni kura ya hapana katiba pendekezwa, ni sawa na kusema baba amenunua mboga ili watoto wake wapate kula, anafika nyumbani anaamua kuimwaga mboga eti kwa kuhofia watoto hawata kula, hivyo mzazi ataingia gharama ya kununua mboga nyingine, hapo utakuwa hujawaumiza watoto unajiumiza wewe mwenyewe mzazi ambayo ndiyo serikali
 
Sawa kujenga jengo la gharama halafu anakuja mtu anawaambia watu bomoweni, wewe na watu wako mtaonekana vp?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…