Tatizo Lako Mkuu Bado Hujamuelewa Vizur MUSAMI Kwa Ufupi ilitakiwa Maaskofu Wakae Pamoja Na Mashekhe Wajadil Msimamo Wao Ndo Wautoe Hadharani. Lakin Kusema Maadhimio Ya Maaskofu Tz Ni ... Juu Ya Katiba. Swali, Je Masheikh Nao Wakija Na Msimamo Wao Kinyume Na Maaskofu Huoni Kama Itatokea Balaa Kubwa?.
Sio kila mtu anaelewa maana ya KATIBA. wengine wanafikiri labda ni kitabu cha shule km vingine. Hivyo mtu km MAASKOFU wamekaa wakajadili na kiona haifai mimi naona ni sawa. Km ipo sawa hii KATIBA Kwanini walioshoka dola washawishi kupiga kura ya NDIYO? Hata aliyepo Madarakani aelewe kabisa nae atakuwa raia wa Kawaida japo atakuwa ananeemeka na Pension.
Viongozi wa SERIKALI watafakari ktk pande zote za KURA YA NDIO na HAPANA ina maana yake.
Na km ingewezekana leo hii kuleta RASIMU YA KATIBA ya mh. WARIOBA na KATIBA INAYOPENDEKEZWA NA BUNGE lililopita halafu zote zitolewe ELIMU, halafu tuzipigie KURA.
Majibu ya maswali yaliyopo mtaani yangepata majibu
Kwa hiyo wewe unakubali serikali inavyoipigia debe katiba? Serikali yenyewe ina ajenda gani inapowaambia watu wapige kura ya NDIYO? Kwa nini serikali wasitoe tu uhamasishaji wa kusoma katiba wakawaacha watu kuamua wenyewe? Mifano halisi ninayo. Waziri Mh Mary Nagu juzi kati alikuwa na wamasai akawaambia hii katiba ni nzuri wapige kura ya NDIYO (Hiyo ni kampeni ya serikali) Makamu wa pili wa rais kule Zanzibar naye hivi majuzi kule Zanzibar aliwaambia wananchi kuwa wapige kura ya NDIYO. (Pia hiyo ni kampeni ya serikali) Sasa inakuwaje vibaya Maaskofu kuwaambia waumini wao wapige kura ya HAPANA wanapoona inatakiwa kuwa hivyo? Jamii forum ni ya watu wenye akili wanaoweza kuchambua mambo lakini nasikitika kuona watu wengi wanashindwa kuielewa vizuri hii nchi yetu. Tukubaline hapa kama Maaskofu wamekosea basi na serikali ishakosea zamani na hakuna wa kumlaumu mwenzie...
wao ni viongozi wa dini,kwa nafasi yao wametushauri wauumini tupinge katiba mbovu.wewe unaanza kuhoji.kanisani unafuata nini?zaidi ya yote akili za kuambiwa changanya na zako.say no to fake constitution.wajulishe na wenzio
Tokea Kardinali Pengo atoe kauli ya kupinga mapendekezo ya Maaskofu juu kura ya hapana kwa katiba inayopendekezwa,amekuwa akiitwa msaliti hata kufikia kutukanwa na akina Gwajima, lakini nionavyo mimi wasaliti ni maaskofu.
1. Wameusaliti wito wao wa kuutangaza Ufalme wa Mungu badala yake wamekaa wakipoteza muda kuujadili ufalme wa duniani Luka 9:2 Yohana 18:36 labda watuambie wameongozwa na andiko gani
2. Wamesaliti umoja wa Taifa la Tanzania maana unapotoa tamko la wakristo kupiga kura ya hapana unawaambia nini watu wa imani nyingine?je na wao wakikutana kupiga kura ya ndio,mustakabari wa Taifa utakuwaje?
3. Je huu sio mwanzo wa kutumia umoja huu kufanya kampeni za viongozi wanaoona wao wanafaa kuongoza kipindi cha uchaguzi?
4. Makanisa yanahusisha watu kutoka makundi mbalimbali, wapo wanaoipinga katiba inayopendekezwa na wapo wanaoikubali,je huu sio mwanzo wa kukaribisha migogoro ya kiitikadi ndani ya makanisa.
Mungu atusaidie...
.wao hawajajadili na waumini wao,wamewaambia wapige kura ya sio.wewe binafsi unaionaje rasmu hii?na ilivyopitishwa unaridhika?Kanisani sio sehemu ya kujadiliana katiba ya nchi,bali ni sehemu mahususi kwa ajili ya kumuabudu Mungu,sababu ni kwamba kwa ulimwengu wa leo ni kawaida kukuta watu wa mataifa mbalimbali ndani ya kanisa,sasa mkianza kuleta mijadala ya katiba yenu kwenye ibada wewe unaona litakuwa jambo la hekima?Hawa wageni watafaidikaje na mijadala yenu?
Kwa kuwa huzijui ToR za wachungaji ninakushauri unyamaze au uulize uambiwe. Soma Biblia kama wewe ni Mkristo utaona manabii walivyokuwa wanawakemea wafalme. Kumbuka Eliya aliwahi kuizuilia mvua kunyesha. Najua wewe siyo Mkristo ndo maana hujui kazi za watumishi wa kweli walioitwa na Mungu.
Kanisa linahusisha watu kutoka mataifa mbalimbali ndio maana kuna makanisa hapa nchini yanaongozwa na raia wa kigeni,mfano kuna Wachungaji kutoka Kenya,Nigeria,Uganda n.k wanachunga makanisa hapa nchini,sababu ni kwamba Kanisa lipo kwa ajili ya kueneza ufalme wa Mungu na si wa dunia,Sasa kuleta mijadala ya katiba ndani ya kanisa ijadiliwe na watu kutoka mataifa mbalimbali ni ukengeufu.Tafakari
Sina cha kutafakari. Hao Wanigeria unaowazungumzia hata wakiwa kwao huwakemea watawala. Kama huna ToR za wachungaji endelea na imani yako.
na serkal inavosema uipigie kura ya ndiyo haijakukera? je wewe umeipata au hata kuisoma hiyo katiba pendekezwa??? umeielewa????? kwani kazi ya viongozi wa dini ni kuhubiri neno la Mungu tu? wao walichofanya ni kuelimisha uma na kwa kuwa wengi hatujasoma hiyo katiba, wao wamesoma na kuiona ina walakini ndo maana wametoa kama angalizo....but hujalazimishwa kupigia kura yoyote...wao wametoa angalizo ili yakikupata usimtafute mchawiMimi ni Roman Catholic lakini hawa maaskofu wamenifanya niufikirie mara mbili mbili huu ukatoliki wangu.
Kwanini hawa maaskofu watudharau kwa kiasi hiki? Yani wametuona sisi ni ma-Robot tusioelewa chochote hadi tuelekezwe cha kufanya?
Hawa maaskofu kwa akili zao wanadhani Mungu alishindwa kutufanya ma-Robot tufanye anayoyataka yeye tuepukane na haya mateso ya hii Dunia?
Wamenikera sana hao maaskofu.
Mimi ni Roman Catholic lakini hawa maaskofu wamenifanya niufikirie mara mbili mbili huu ukatoliki wangu.
Kwanini hawa maaskofu watudharau kwa kiasi hiki? Yani wametuona sisi ni ma-Robot tusioelewa chochote hadi tuelekezwe cha kufanya?
Hawa maaskofu kwa akili zao wanadhani Mungu alishindwa kutufanya ma-Robot tufanye anayoyataka yeye tuepukane na haya mateso ya hii Dunia?
Wamenikera sana hao maaskofu.