Maaskofu: Kataeni Katiba

Maaskofu: Kataeni Katiba

mandili

Senior Member
Joined
Mar 16, 2013
Posts
141
Reaction score
15
Jukwaa la Wakristo Tanzania limewataka waumini wake kujiandikisha kwa wingi katika Daftari la Kudumu la Wapigakura, kuisoma Katiba Inayopendekezwa na kujitokeza kuikataa kwa kupiga kura ya "hapana".

Taarifa iliyotolewa na Jukwaa hilo jana na kusainiwa na mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Askofu Dk Alex Malasusa, mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa na mwenyekiti wa Kanisa la Pentekoste Tanzania (CPCT), Askofu Daniel Awet, imetaja sababu mbili za uamuzi wake kuwa ni muswada wa Mahakama ya Kadhi kukiuka misingi ya Taifa kuwa na Serikali isiyo na dini, na Kura ya Maoni kusababisha mgawanyiko.

"Hivyo basi, Jukwaa linawataka waumini wake wote wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, waisome Katiba Inayopendekezwa na kushiriki kikamilifu vipindi vya elimu juu ya Katiba Inayopendekezwa na kisha wajitokeze kwa wingi kupiga kura ya hapana kwa Katiba Inayopendekezwa kwa sababu zilizotajwa hapo juu," linasema tamko hilo la kurasa nne.

Taarifa hiyo imekuja siku moja tu baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kutangaza kuwa muswada wa uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi uliokuwa umeondolewa kwenye mkutano uliopita wa Bunge kwa ajili ya mashauriano zaidi, utawasilishwa katika vikao vya chombo hicho vinavyoanza Jumanne ijayo baada ya kufikiwa kwa maridhiano baina ya viongozi mbalimbali wa dini.

Pia tamko hilo limekuja siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kuiagiza Hazina itoe fedha kwa Tume ya Uchaguzi (Nec) kwa kadri inavyohitaji ili kuiwezesha kukamilisha mchakato wa Kura ya Maoni.

Viongozi wa Jukwaa la Wakristo walikutana Machi 10, mwaka huu kujadili kwa kina kuhusu hali ya usalama wa nchi ilivyo sasa na mustakabali wake, Katiba inayopendekezwa na uanzishaji wa Mahakama ya Kadhi.

Katiba inayopendekezwa

Taarifa hiyo ya maneno 712 inasema: "Katiba Inayopendekezwa imeleta mgawanyiko mkubwa katika Taifa kwani imepatikana kwa njia zisizo za kiadilifu na mchakato wake umeendeshwa kwa hila na ubabe.

"Pia haijajibu matakwa na malalamiko ya wananchi kwenye masuala mbalimbali kama muundo wa Serikali, miiko na maadili ya viongozi wa umma, haki za binadamu, madaraka ya rais na uwiano wa mihimili ya dola.

"Ikumbukwe Katiba Inayopendekezwa ilipitishwa kwenye Bunge Maalumu la Katiba kwa ahadi ya Serikali kuipa dini ya Kiislam Mahakama ya Kadhi. Inashangaza kuwa hata Serikali inatoa rushwa ili kufikia malengo yake. Kwa hali kama hii, Kanisa haliwezi kuunga mkono kupitishwa kwa Katiba Inayopendekezwa," ilisema sehemu ya tamko hilo.

Mahakama ya Kadhi

Kuhusu uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi, taarifa hiyo inasema, "Suala la uanzishwaji wa Mahakama hii nchini kama tulivyotoa maoni yetu kwa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria (Januari 16, 2015); barua yetu kwa Waziri Mkuu na matamko mbalimbali yaliyokwisha kutolewa kuhusu jambo hili; Mahakama ya Kadhi inakiuka misingi ya Taifa hili kuwa na Serikali isiyokuwa na dini wala mfumo wa sheria unaobagua raia wake kwa misingi ya dini."

Chanzo: Mwananchi
 
Ngoja tusubiri akina Muhagachi nao waje na matamko yao.
 
Wakiweka mahakama ya Kadhia, Wakristo watasema NO. Wasipoweka, mujahidina nao watasema NO. Ngoma bado mbichiiiii!!!!

Katiba ya Chenge a.k.a Mzee wa Escrow, Nyoka mwenye makengeza.
 
Nchi imegawanyika hii.......JK Atuachie nchi ikiwa moja kama alivyoikuta
 
Kwa kweli hata mimi nimeamua kura yangu ni HAPANA
 
haiki kifungu ndio moyo wa kataba

safi sana Baraza

wapi shekh mataka wa bakwata

[“Pia haijajibu matakwa na malalamiko
ya wananchi kwenye masuala
mbalimbali kama muundo wa Serikali,
miiko na maadili ya viongozi wa
umma, haki za binadamu, madaraka ya
rais na uwiano wa mihimili ya dola]

cc: FaizaFoxy
 
Last edited by a moderator:
Kwa kweli hata mimi nimeamua kura yangu ni HAPANA

Pigieni hapana kwa mambo ya msingi, mahakama ya kadhi inawakera sana na sijui kwa niñi , wabongo tujitahidi Kuwa waelewa. Watu wanakurupuka tu.
 
Wakiweka mahakama ya Kadhia, Wakristo watasema NO. Wasipoweka, mujahidina nao watasema NO. Ngoma bado mbichiiiii!!!!

Katiba ya Chenge a.k.a Mzee wa Escrow, Nyoka mwenye makengeza.

Nawaunga mkono viongozi wangu wa kiroho kwa tamko lao naamini jumapili makanisa yote tutasomewa hlo tamko.
 
Mimi ninafikiri hii mahakama ya kadhi ni vema na ni busara ikaanzishwa na waislamu wenyewe kama chombo chao cha dini. Wakianzishe wenyewe na kukiendesha wenyewe. Si busara hata kidogo kwa nchi kama Tanzania Taasisi ya dini fulani ikawa sehemu ya mhimili wa dola. Ikiwa hivyo ina maana Tanzania tayari itakuwa ni nchi ya dini fulani maana sehemu ya serikali yake ni chombo cha dini hiyo. Hii ni kusema kwamba Tanzania itakuwa ni nchi ya kiislamu. Halafu hili la kadhi ni mwanzo tu. Hawatakomea hapo, wakipewa hili watarudi kushinikiza Tanzania kuwa mwanachama wa nchi za Kiislamu (OIC). Wakipata hilo, Watashinikiza nchi iongozwe kwa sharia. Wakipata hilo watashinikiza kwamba Ukristo uharimishwe kama ilivyo kwa nchi za kigaidi kama Irani. Huko ndiko tunakoelekea endapo watapatiwa ombi lao.
 
Wagala kwenye suala la mahakama ya kadhi ni kama 'joka la mdimu'
 
Hakuna kura ya katiba...mambo yamekwenda kinyume na matarajiwa....na hii imefanywa maksudi baada ya kusoma alama nya za nyakati.HAKUNA KURA YA MAONI tunataka AMANI ....tupendane Wakirsto na Waislamu tusidanganywe na wachache wanaotaka madaraka.
 
Ngoma inogile. Pinda yuko njia panda, hajui atoke vipi tena. Jamani nyinyi viongozi wa kiroho mbona mnakiweka chama chetu kwenye wakati mgumu namna hii?
 
Mimi ninafikiri hii mahakama ya kadhi ni vema na ni busara ikaanzishwa na waislamu wenyewe kama chombo chao cha dini. Wakianzishe wenyewe na kukiendesha wenyewe. Si busara hata kidogo kwa nchi kama Tanzania Taasisi ya dini fulani ikawa sehemu ya mhimili wa dola. Ikiwa hivyo ina maana Tanzania tayari itakuwa ni nchi ya dini fulani maana sehemu ya serikali yake ni chombo cha dini hiyo. Hii ni kusema kwamba Tanzania itakuwa ni nchi ya kiislamu. Halafu hili la kadhi ni mwanzo tu. Hawatakomea hapo, wakipewa hili watarudi kushinikiza Tanzania kuwa mwanachama wa nchi za Kiislamu (OIC). Wakipata hilo, Watashinikiza nchi iongozwe kwa sharia. Wakipata hilo watashinikiza kwamba Ukristo uharimishwe kama ilivyo kwa nchi za kigaidi kama Irani. Huko ndiko tunakoelekea endapo watapatiwa ombi lao.

Mkuu,

Watanzania wanarudishwa nyuma kwenye ubaguzi wa kidini ambao ulishafutika kwa sababu za kipuuzi tu za viongozi wachache.
Hali hii haikubaliki hata kidogo. Sheria zitazowagawa wananchi kwa misingi ya dini, kabila au mahali mtu anapoishi /alipozaliwani ndani ya Tanzania ni kinyume kabisa na katiba ya nchi! Viongozi wabinafsi na waovu hawalioni hili.
 
Wakiweka mahakama ya Kadhia, Wakristo watasema NO. Wasipoweka, mujahidina nao watasema NO. Ngoma bado mbichiiiii!!!!

Katiba ya Chenge a.k.a Mzee wa Escrow, Nyoka mwenye makengeza.

Mkuu, watakaoshinda Ndo wengi kiimani hapa nchini.(refer censor ya 2012)
 
Safi sana Maaskofu wetu kwa msimamo uli thabiti kupinga umma kupokwa maoni yetu!
 
Back
Top Bottom