Maarifa ya Kiasili/kienyeji ktk ufugaji. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maarifa ya Kiasili/kienyeji ktk ufugaji.

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Malila, Feb 25, 2012.

 1. M

  Malila JF-Expert Member

  #1
  Feb 25, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Kwa wafugaji wa kienyeji wa wanyama na ndege huko vijijini kwetu, kuna vitu au maarifa ya kienyeji ambayo huwa wanatumia, naomba tuyajadili na kujulishana pia tuonyeshane kama kweli yanafanya kazi. Na kama ni muhimu kuyaendeleza kwa manufaa yetu.

  Mfano; Kuku mgeni akiletwa nyumbani, nimekuwa nikiona watu wakinyoa manyoya kisha kuyachoma motoni, wanamzungusha kuku na baadae wanamwachia. Mkulima huamini kuwa kwa kufanya hivyo kuku hawezi kutoroka. Juzi nimeipata mpya, eti vitoto vya bata ili visife, wenyewe huwa wanavivuta shingo mapema,wanaamini kwamba vinapona vyote.

  Vitu ni vingi vinafanyika huko vijijini, ukikijua tupa hapa ili tujadili.
   
 2. m

  mwalwisi Member

  #2
  Feb 27, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 46
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Malila kwa hilo la moto sijalisikia bado, ila hili la bata kama utakumbuka mwaka jana niliwahi kuandika hapa nikiomba msaada wa dawa, bata wangu wadogo walipofikisha wiki 2 wakaanza kuanguka miguu juu wanakufa. Nilishauriwa dawa nyingi hapa including OTC plus, lakini waliendelea kufa nilipoteza vifaranga watano. kuna siku nikapita pale Ukonga magereza kuna mzee mmoja amefuga bata wengi sana, nikamfuata akaniambia kila bata wakifikisha wiki moja unawashika huku shingo yake ikiwa imelala katika vidole viwili vya mkono mmoja na vidole viwili yaani gumba na hiki cha shahada unavuta shingo taratibu hadi usikie mlio kama kijiti kikavu kinavunjika. Nikafanya hivyo kwa wale waliobaki, hata wale waliokuwa hoi wakapona na wakaendelea kuzaliana huku nikifanya hivyo kila baada ya vifaranga kutimiza wiki moja. Sijajua kama wakiwa wengi mtu atafanyaje maana zoezi ni kubwa na gumu. KITAALAMU SIJUI NINI KINAFANYIKA NAJUA TU BATA WALIPONA
   
 3. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #3
  Feb 27, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  haya mambo ya imani magumu sana
   
 4. M

  Malila JF-Expert Member

  #4
  Feb 27, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Kuna mambo mengine ni mpaka uwe umefanya ndio unaweza kuamini. Ni nini huwa kinafanywa kwa mnyama mpaka asahau kwao,kumbuka ni just few meters toka ulikomnunua? Kuna watu wanaweza kufanya maarifa hayo. Tuachane na hayo. Kuna mzee mmoja yy, huwa anachukua majani fulani anayatandaza kuzunguka zizi,siafu hawapiti hapo. Kumbe sisi wafugaji wa mjini tunaingia gharama kubwa kununua dawa na ushauri kibao. Ujanja huu wa kutumia malighafi na rasilimali zilizopo ktk mazingira yetu ndio ninao utaka.
   
 5. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #5
  Feb 27, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  hiyo ya kumnyonyoa kuku manyoya na kuyachoma ni dodoma.

  1. sis kwetu ukinunua ng'ombe wakati wa kumuingiza zizini kwa mara ya kwanza ni lazima aingie kinyumenyume asipoingia hivyo hataweza kuzaa na pia anaweza kuleta mikosi nyumbani

  2. babu alikuwa akimpiga kila ng'ombe kofi kabla ya kuingia zizini

  3. Huwa hatununui mbuzi/ng'ombe wa kufuga kutoka kwa wagogo.. kwakuwa huwa wanawafanyia mazingara kabla ya kuwauza ili wasizae

  4. kuna kijijini ilikuwa ukinunua mnyama ni lazima atoroke na arudi kwao
   
 6. M

  Malila JF-Expert Member

  #6
  Feb 27, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Hii hapo pekundu nimekutana nayo Vingunguti, pale unaweza nunua mbuzi na asizae kabisa. Tumejaribu mara kadhaa,ndio tukapewa siri hiyo kuwa hawa jamaa wa Dom wanafanyizia mbuzi wao.

  Hii ya kuingia kinyumenyume inafanya kazi mpaka leo?

  Kule home kuna babu alikuwa na uwezo wa kuwazuia ng`ombe wasile mahindi ya mtu. Swali liko pale pale, wanafanyaje hawa wazee?
   
 7. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #7
  Mar 29, 2012
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  hahaha mmenifurahisha na kuna ile ukimchinja kuku koromeo ama ile wind pipe unarusha inase kwenye ukuta wa jiko kule jikoni................nilikutwa ikifanywa sana maene ya Dabaga kule wilaya ya Kilolo ......mpaka kesho sijawahi jua ni kwa nini
   
Loading...