Maarifa na mapinduzi katika jamii na Taifa

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Katika binadamu kuna hazina iliyojificha ndani kabisa ya roho ya binadamu, Ni kazi ya fikra kuitafuta kwa kutafakari, na kwasababu pasipo kutafakari hazina hii haitofichuka


Ni wajibu wetu kutafakari kila siku ili kupata majibu ya matatizo yanayo tutatiza kila siku katika maisha yetu.

Pasipo kutafakari kamwe majibu haya kuhusu maisha hatutaweza kuyapata. Ni wajibu wetu kuchukua hatua na kutafakari ili kupata suluhisho la matatizo yetu mengi yanayo tukabili.


Hizi ni changamoto ambazo binadamu ameumbwa nazo na ni wajibu wake kukabiliana nazo na kugeuza maisha na
mazingira anayoishi. kuwa bora zaidi. Ni wajibu wetu kupiga hatua kama binadamu na kama taifa. Lakini bila kutafakari kwa kina suluhisho la matatizo yetu yanayo tukabili itakuwa ni vigumu kuyapata.



Matatizo mengi ambayo binadamu anayoyapata ni kwasababu hakai na kupata muda wa kutafakari. Kutafuta suluhisho la matatizo yake ya kila siku. Kama ikiwa tabia yetu ya kila siku kukaa katika kiti na kutafakari basi haitochukua muda kwetu kuyashinda maisha.



Sitaki kuongea matatizo yetu tuliyonayo kama jamii ya watanzania lakini kitu ninachojua sisi tumekuwa wepesi mno wa kuongea kuliko kufikiri na tunajiona wajuzi sana. Tunaishi katika giza bado tuko gizani mwanga wa maarifa bado haujatumulikia ipasavyo. Tunahitaji maarifa na kujitambua kama taifa tutoke hapa tulipo.



Tunaishi ili tuvune maarifa ili maarifa hayo tuyatumie kufanya mapinduzi katika maisha yetu na katika jamii zetu na katika nchi zetu ili maisha ya binadamu yaimarike.



Binadamu wa miaka 10,000, iliyopita sio sawa sawa na wa sasa. kuna kazi ilifanyika katika utafutaji wa maarifa kutoka kwa wenzetu wa ulaya. Binadamu wa sasa ameendelea zaidi ingawaje bado tunachangamoto za hapa na pale katika dunia yetu. Lakini ni wajibu wa binadamu kuendelea kufikiri ili kukabiliana na changamoto hizi.



Ni akili pekee ambayo hufanya kazi kubwa kumwendeleza binadamu, wale wanaotumia akili zao vizuri huendelea. Ni lazima na ni wajibu wetu, kuhangaika kupata maarifa ili tufanye mapinduzi katika taifa letu.

Maendeleo ya ulaya na marekani hayakuja kwa bahati mbaya watu walihangaika kutafuta maarifa na kufanya kazi. Kwa kufikiri na kutafakari , akili hukua na mambo mapya ugunduliwa.

Tunatakiwa kubadilisha hii tabia na kuanza kufikiri. Tutafikia maendeleo yetu pale tu tutakapoanza kufiiri kutafuta maarifa.


Mapinduzi ya kweli katika taifa letu yataletwa kwa kufikiri. Kama tutabadilisha mwenendo wetu kama taifa wa kuwa wepesi wa kuongea kuliko kufikiri tutafanikiwa.



Hakuna kitu kinachofurahisha nafsi kama kufikiri , kupata tabu katika kufikiri , kisha kugundua kitu kitakachosaidia maisha ya binadamu. Ni muhimu kukuza akili zetu.



Ni fikra pekee huleta mapinduzi . Tuna mshukuru Mungu kwa kutupa roho ndani yetu kwakuwa kwa kutumia akili na kufikiri tunagundua hazina iliyojificha ambazo zina thamani zaidi ya dhahabu na Lulu.



Ni kipi chenye thamani kwenye maisha ya binadamu zaidi ya maarifa ?? Je ni Lulu ? dhahabu? au Almasi ?

Kwa kukosa maarifa kwetu tunashindwa kuchimba almasi wenyewe na dhahabu wenyewe. Tunaita makampuni ya nje. Tunashindwa kuchimba gesi tunaita makampuni ya nje. Suluhisho pekee ya matatizo tuliyonayo ni kutafuta maarifa. Hatuwezi kuendelea pasipo maarifa.


Ni lazima tupambane na ujinga kwa nguvu zote kama tunataka jamii zetu na taifa letu liendelee. Tuwape maarifa watoto wetu na tujenge tabia zao.



Tukifanya hivi tutakuwa na matumaini kwa baadae ya taifa letu. Taifa la wajinga haliwezi kuendelea watarithishana ujinga kizazi kimoja hadi kingine.



Lakini mwisho lazima tuue tabia zote za ubinafsi na tujenge taifa la watu wamoja na wenye malengo yanayofanana katika mwelekeo wa taifa. Kwa kutambua wajibu tatu muhimu kwa taifa lolote kuendelea.

Wajibu wa mtu kwa taifa lake. Kwa Jamii yake na kwa familia yake.
 
Back
Top Bottom