Jana nikiwa kazini mara nikamuona sharo-b mmoja katinga t-shirt yake iliyochorwa fuvu la mtu akiwa amechuchumaa kuonyesha ana-fart. Kuna maandishi yameandikwa
'SILENT BUT DEADLY'.
Ikanikumbusha t-shirt nyingine ya jamaa mmoja hapohapo kazini iliyokuwa imeandikwa
'FIFTEEN MEN ON DEADMAN'S CHEST' huku imechorwa vikaragosi 15 kwenye eneo lililosawa na kifua cha jamaa.
Jana tarehe 30.10.2012 nikitoka kazini narudi home maeneo ya Amana Stand kuna binti mmoja halfcaste alivaa t-shirt rangi ya kijani kifuani ikiwa na maandishi makubwa yaliyoandikwa kwa herufi kubwa "HARLOT" Binti alionekana yuko busy anarukaruka akiwa amebeba tangazo hilo kifuani mwake. Haaaaaaa haaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!
Mmoja naye nilipishana nae maeneo ya Ubungo kavaa tshirt imeandikwa kwa juu BEER IN huku kukiwa na kidole kinachooint kwenye koromeo na kwa chini yake imeandikwa BEER OUT kukiwa na pointer inayoonyesha chini ya kifua.
hivi unavaa nguo km hiyo huna watoto nyumbani ama wadogo zako? ama tuseme ndo sehemu ya ile asilimia inayomaliza shule haijui kuandika hata jina!!! just curious
jana my close friend tena yupo chuo kavaa tshert apa kwenye matiti imeandikwa just for you,nkamuuliza wot is for me akabaki anakenua,ningekua namuwinda jana ningejihalalishia
Nipokuwa form 1 nilikuwa na T-shirt ina picha ya papa John Paul 2 akivuta sigara kubwa,imeandikwa I Like Pope,The Pope Smokes Dope,Wale wababe wa F4 walikuwa wanaiwinda hadi wakaniibia