Maandiko kama haya yana maana gani?

Maandiko kama haya yana maana gani?

Joined
Dec 19, 2013
Posts
74
Reaction score
13
Wala msijisumbukie mtakula nini na mtavaa nini, baba yenu yupo. Akaongezea kwa kusema,angalini ndege wa angani hawapandi wala hawavuni, hata hivo mungu huwalisha. Upande mwingine maandiko yanasema, ASIYEFANYA KAZI ASILE.
 
Mkuu nenda kwa kiogozi wako wa dini atakufafanulia maana ya hayo maandiko,au mwone Mzee wa upako kesho kanisani kwake
 
Kwa akili ya kawaida unaweza ukagikiri Biblia imejichanganya la hasha, unajua hofu huwa inaondoa uwepo wa Mungu katika maisha ya wanadamu na uwepo wake ukiondoka Mungu hawezi kukubariki. Huu mstari haumaanishi kuwa usifanye kazi bali unamaanisha fanya kazi ya halali kwa kutumia mikono yako na HAKIKA Mungu ataibariki kazi yako na utapata cha kula, pa kulala na vya kuvaa.
 
Ezekiely Charlese,

Mkuu kwa kawaida katika Biblia au maandiko yeyote yale ni vizuri kusoma kwa kina vifungu vilivyo juu au chini ya mstari wenye kukutatiza.

Sasa katika Luka 12:16 YESU aliwaambia watu mfano uliokuwa wa mtu aliyekuwa na mipango mingi katika wingi wa vile alivyonavyo, Sasa kabla ya mfano huo huo akasema UZIMA wa mtu hauko katika vingi alivyonavyo.Mwisho wa mfano/kisa alichotoa YESU alisema KWA SABABU HIYO...msijisumbue kwa neno lolote, yaani katika Luka 12:22.

Pili, Paulo katika Wathesalonike anasema Asiyefanya kazi na asile...Hakuna mtu aliyekataa watu wasifanye kazi. Kumbuka hata kabla ya dhambi MUNGU alimpa Adam(mwanadanu wa kwanza) bustani ya Eden KUILIMA NA KUITUNZA (Mwanzo 2:15) Lakini ni MUNGU huyo huyo aliyeagiza katika amri ya nne kati ya zile kumi kuwa ."..SIKU SITA FANYA KAZI...."(Kutoka).

Hivyo Biblia haipingani, mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Matendo ya mwili ni matokeo ya kiroho, unapompa Mungu maombi yako atayashughulikia kwa muda muafaka, yeye anauangalia ustawi wako.

Mistari iliyotoka sehemu tofauti na mazingira tofauti si lazima iwe na tafsiri moja japo imetumia lugha ya picha inayofanana.
 
Unajua biblia soma yake sio kama gazeti.inaitajika upeo na uwezo wa roho mtakatifu kusoma na kuelewa. Hii ni siri nzito sana kwetu wakristo ndio maana sisi sio watu wa jazba na mapovu.

Wale watoto wa kufikia huwa wanachukua mstari mmoja halafu mapingamizi huanza.hawana siri ya kujua maana za maandiko ktk biblia. Kukosa siri ya kulijua neno utaishia kuwa kichaa,tazama wale wakristo wa "kufikia" wanao sali siku saba za wiki bila kufanya kazi ni wakosefu wa siri na maarifa za maandiko.bila shaka wa wakumbuka wale waliotaka kusafiri kwenda ulaya kuhubiri neno bila kuwa na visa
 
ndo maana paulo akaandika ......upumbavu wamungu unahekima kuliko wa binadamu.....maandiko kama haya mmmhhhh....:i simo
 
Ezekiely Charlese,

Mkuu kwa kawaida katika Biblia au maandiko yeyote yale ni vizuri kusoma kwa kina vifungu vilivyo juu au chini ya mstari wenye kukutatiza.

Sasa katika Luka 12:16 YESU aliwaambia watu mfano uliokuwa wa mtu aliyekuwa na mipango mingi katika wingi wa vile alivyonavyo, Sasa kabla ya mfano huo huo akasema UZIMA wa mtu hauko katika vingi alivyonavyo.Mwisho wa mfano/kisa alichotoa YESU alisema KWA SABABU HIYO...msijisumbue kwa neno lolote, yaani katika Luka 12:22.

Pili, Paulo katika Wathesalonike anasema Asiyefanya kazi na asile...Hakuna mtu aliyekataa watu wasifanye kazi. Kumbuka hata kabla ya dhambi MUNGU alimpa Adam(mwanadanu wa kwanza) bustani ya Eden KUILIMA NA KUITUNZA (Mwanzo 2:15) Lakini ni MUNGU huyo huyo aliyeagiza katika amri ya nne kati ya zile kumi kuwa ."..SIKU SITA FANYA KAZI...."(Kutoka).

Hivyo Biblia haipingani, mkuu.

Mungu akubariki kwa ufafanuzi mzuri wa bible mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom