eden kimario
JF-Expert Member
- Jun 13, 2015
- 10,355
- 16,401
Maandamano ya wanaotaka kujitenga yarindima Katalonia
Waandamanaji wanaounga mkono uhuru wa jimbo la Katalonia nchini Uhispania wamezifunga barabara kuu pamoja na njia ya treni ya mwendo kasi katika jimbo hilo leo. Hayo yanafanyika ikiwa ni mwaka mmoja baada ya zoezi la kura ya maoni lililopigwa marufuku juu ya kujitenga jimbo hilo ambalo liligubikwa na vurugu za polisi. Mamia ya wanaharakati walimiminika katika barabara za Treni ya mwendo kasi katika eneo la Girona Kaskazini mwa mji wa Barcelona wakati pia barabara kuu za mji huo na mji wa Lleida zikifungwa. Maandamano hayo yaliitishwa kupitia mtandao na kundi linalojiita kamati za kuitetea Jamhuri(CDRs).Kundi hili lilianzishwa kwa lengo la kusaidia kufanikisha kura ya maoni ya mwaka jana iliyopigwa marufuku na sasa linadai kuwepo mchakato wa wazi wa kujitenga jimbo hilo la Uhispania.
Dw