Maandamano yapigwa marufuku Kinshasa- Congo

Maandamano yapigwa marufuku Kinshasa- Congo

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,622
Reaction score
8,427
Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imepiga marufuku kufanyika maandamano wiki hii ya kupinga kuendelea kuwepo madarakani kwa Rais Joseph Kabila.

Taarifa iliyochapishwa katika mitandao ya habari nchini Congo imesema maafisa katika mji mkuu Kinshasa wamepiga marufuku maandamano yote yaliyokuwa yamepangwa wiki hii.

Wafuasi wa Rais Kabila walikuwa wamepanga maandamano kesho Jumanne kuunga mkono kucheleweshwa kwa chaguzi hadi Desemba mwaka ujao. Awali, upinzani pia ulikuwa umepanga maandamano kumpinga Kabila hapo kesho lakini ikaahirisha hadi Alhamisi.

Kiongozi wa upinzani Felix Tshishekedi amesema atapuuza marufuku hiyo na kuwataka Wacongo kujitokeza kwa wingi kuandamana tarehe 30 mwezi huu.

- DW Swahili
 
Kwanza kilianza kwa Mugabe.

Kinaenea taratibu kama cha Tunisia.
 
Back
Top Bottom