Maandamano ya wanahabari Iringa kwa RC

Maandamano ya wanahabari Iringa kwa RC

Waandishi habari Tanzania walikwisha goma siku nyingi zilizopita,na ndio maana hatupati habari makini,bali habari baada ya bahasha.

Ni kweli mkuu, siku hizi habari muhimu utazipata katika mitandao kama hii, ambapo sisi wanachama hutuma habari
bila kutegemea posho...wamemaliza mgomo sasa wanaandamana, Jibu halisi ni wao kujiunga na kuwadai waajiri wao
maslahi bora ya kazi zao ili wawe huru bila kuendekeza bahasha...Mara nyingi matukio muhimu yamekuwa hayaripotiwi
kisa hawajapewa posho...je wanaitumikia jamii au wanatumikia posho???
 
Hivi kwa nini tusijulize maswali haya kabla ya kulaumu au kuunga mkono maandamano hayo.
1:Je mwandishi wa habari analipwa mshahara?
2:kama analipwa ni nini mafao yake awapo nje ya kituo chake cha kazi?
3:Kama anataka kupokea malipo toka kwa chanzo cha habari,je habari yenyewe itakuwa halisi?
4:kama ni mwandishi wa kujitegemea.nini mkataba wake na wale anaowapelekea habari?

Mkuu

Maswali ya msingi sana hayo. Hili sio suala la kujadiliwa kishabiki, linahusu objectivity katika journalism. Watamkasirikiaje RC ambaye ni sehemu ya source na kumwacha mwajiri wao.

Watakuwaje huru iwapo nao watakuwa sehemu ya mfumo!

Katika hili siwaungi mkono, wangetoa tamko la kugomea kazi za serikali yao ya mkoa hata wanene wajapo hapo ningewaelewa.
 
Waandishi wa habari mkoani Iringa wamefanya maandamano yao kuelekea kwa MKUU wa MKOA kwa lengo la kulalamikia kunyanyaswa na Ofisa Habari wa Mkoa huo. Moja ya malalamiko yao ni kunyimwa posho wakati wa safari za viongozi mbalimbali mkoani humo. Nawaleteeni picha soon. TAFAKARI, CHUKUA HATUA!

Waandishi wa Habari wa Iringa Hawana HOJA YA MSINGI!Ni hulka ya Mtanzania kulia lia,wanalazimisha wamezibwa mdomo hadi kuvaa plasta ni uzushi na uharibifu wa vifaa tiba(plaster)!Gari la kwenda msafara wa makamu wa raisi walipewa,kama hawakuandaliwa sehemu ya kulala wakiwa ziarani na ilikuwa stahiki yao kulipwa wangepeleka malalamiko kwa mkuu wa mkoa ili warejeshewe na si kukimbilia kuandamana!
Wandishi wa Iringa hamna jipya!
Chapeni kazi acheni UTOTO!
 
Mkuu

Maswali ya msingi sana hayo. Hili sio suala la kujadiliwa kishabiki, linahusu objectivity katika journalism. Watamkasirikiaje RC ambaye ni sehemu ya source na kumwacha mwajiri wao.

Watakuwaje huru iwapo nao watakuwa sehemu ya mfumo!

Katika hili siwaungi mkono, wangetoa tamko la kugomea kazi za serikali yao ya mkoa hata wanene wajapo hapo ningewaelewa.

wanataka waweke historia kwamba walishawahi kuandamana
 
habari nilizopokea ni kuwa veta na green resource ya mufindi waliwalipa ila walitaka zaidi

Hao waandishi Iringa posho ndio zao, tuwe wakweli wametia aibu, hilo ni jukumu la waajiri wao. Wamekubali kuwafanyia kazi wamiliki pasipo malipo wakitegemea watalipwa na sources, hapo uandishi makini haupo.

Manzingira haya ya kutegemea kulipwa na sources ndiyo yameifanya Iringa isiwe na habari nzito za kiuchunguzi zaidi ya zile za ajali, ushirikina na majanga.

Iringa badilikeni mheshimike katika jamii na sio viongozi na matajiri hapo mjini!!
 
Tumewasikia kupitia radio maria wanasema wamebandua plasta na wanashukuru RC amepokea mabango yao. Kwa mujibu wa maelezo yao ya awali RC aliwasihi wakutane lakini wakagoma na kuamua bila kufikiri kuingia barabarani. Kumbe walichukua chukua viposho kila mahali. Tunatonywa pia kuwa hawa jamaa wana kawaida ya kutishia kuwaandika au kuwatangaza watu vibaya wasipopewa kitu ndogo.
 
Habari baada ya posho ni tamko tata sana katika maadili ya tasnia ya habari na mawasiliano.
 
Waandishi wa habari mkoani Iringa wamefanya maandamano yao kuelekea kwa MKUU wa MKOA kwa lengo la kulalamikia kunyanyaswa na Ofisa Habari wa Mkoa huo. Moja ya malalamiko yao ni kunyimwa posho wakati wa safari za viongozi mbalimbali mkoani humo. Nawaleteeni picha soon. TAFAKARI, CHUKUA HATUA!

Kama kawaida ya serikali watatumia ubabe wao wa kuwapeleka mahakamani ili kuwafunga mdomo
 
Back
Top Bottom