Maandamano ya wanahabari Iringa kwa RC

bibikuku

JF-Expert Member
Feb 16, 2011
832
495
Waandishi wa habari mkoani Iringa wamefanya maandamano yao kuelekea kwa MKUU wa MKOA kwa lengo la kulalamikia kunyanyaswa na Ofisa Habari wa Mkoa huo. Moja ya malalamiko yao ni kunyimwa posho wakati wa safari za viongozi mbalimbali mkoani humo. Nawaleteeni picha soon. TAFAKARI, CHUKUA HATUA!
 
Picha zaidi cheki hapa
Tanzania Yetu

1waandishi-iringa-waandamana-kudai-posho.gif
 
Na kingine walicho kasirika ni kitendo cha ziara ya makamo wa rais hivi karibuni na kulazimishwa wanahabari 8 wakike na wakiume walale ndani ya gari moja toyota cresta..
 
Kumbe kila nyanja na secta mbalimbali hapa Tz zinakabiliwa na matatizo mbalimbali pamoja na ufisadi wa hali ya juu kana kwamba tukiamua kuandamana Tz haitakalika
 
Shukrani kwa CDM kwa hii elimu ya uraia..watanzania wengi walikuwa hawajui kuwa kuandamana ni haki ya msingi kikatiba.
 
asante sana
ni unyanyasi kwa waandishi wa habari nchini
 
Attachments

  • 1waandishi-iringa-waandamana-kudai-posho.png
    1waandishi-iringa-waandamana-kudai-posho.png
    48.3 KB · Views: 171
Maandamano ya kudai posho...posho-posho kila mtu anadai posho tu. Madr, waalimu, wabunge, madiwani,.....nk.

Wengine viongozi wa vyama kama dr S.L.AA posho yake ni milioni 7.

Ama kweli, Uzalendo ulishatushinda tz.
 
Na kingine walicho kasirika ni kitendo cha ziara ya makamo wa rais hivi karibuni na kulazimishwa wanahabari 8 wakike na wakiume walale ndani ya gari moja toyota cresta..

kwani hakukuwa na magari mengine ambayo wangeweza kulala? walipokwenda mabosi wao waliowatuma kufanya coverage walijua watalala wapi?? au walitumwa na RC?
 
kwani hakukuwa na magari mengine ambayo wangeweza kulala? walipokwenda mabosi wao waliowatuma kufanya coverage walijua watalala wapi?? au walitumwa na RC?

Ni muhimu kusikitikia manyanyaso ya wanahabari. Kama ilivyoripotiwa, ukweli wamenyanyaswa.Naungana na wote wanaolaani kitendo hicho. Baada ya kusema hayo, naungana nawe katika hoja zako:waliowatuma kwanini wasiwajibike katika kuwa kimu:ni RC au vyombo wanavyofanyia kazi?
 
Kingine ni kitendo cha bendera za sisiem "magamba" kutawala katika ziara za viongozi wa kiserikali.
 
Wana habari wawapigie kifua watapata masilahi yao siku mbilitu,lakin kama hawaja shilikisha chama chao itakula kwao.hivi waandishi wakigoma nchi nzima itakuaje?wasichezee sekta hiyo kabiisa
 
Nilitegemea kuwaona na Askari polisi wakiongoza maandamano kwani nao walilazwa watu kumi kwenye chumba kimoja

Au wao ni sehemu ya mazoezi? watanzania bwana kwa kufungua mabook ya sababu hatujambo
 
Kingine ni kitendo cha bendera za sisiem "magamba" kutawala katika ziara za viongozi wa kiserikali.

Bendera zinawasuhusu nini wao wanahabari ama zinawakera nini? kwani wao wanasiasa??
 
Waandishi wa habari mkoani Iringa wamefanya maandamano yao kuelekea kwa MKUU wa MKOA kwa lengo la kulalamikia kunyanyaswa na Ofisa Habari wa Mkoa huo. Moja ya malalamiko yao ni kunyimwa posho wakati wa safari za viongozi mbalimbali mkoani humo. Nawaleteeni picha soon. TAFAKARI, CHUKUA HATUA!

Hivi kwa nini tusijulize maswali haya kabla ya kulaumu au kuunga mkono maandamano hayo.
1:Je mwandishi wa habari analipwa mshahara?
2:kama analipwa ni nini mafao yake awapo nje ya kituo chake cha kazi?
3:Kama anataka kupokea malipo toka kwa chanzo cha habari,je habari yenyewe itakuwa halisi?
4:kama ni mwandishi wa kujitegemea.nini mkataba wake na wale anaowapelekea habari?
 
Wana habari wawapigie kifua watapata masilahi yao siku mbilitu,lakin kama hawaja shilikisha chama chao itakula kwao.hivi waandishi wakigoma nchi nzima itakuaje?wasichezee sekta hiyo kabiisa

Waandishi habari Tanzania walikwisha goma siku nyingi zilizopita,na ndio maana hatupati habari makini,bali habari baada ya bahasha.
 
Back
Top Bottom