Maandamano ya CHADEMA Jiji la Mbeya-Picha na Matukio

Maandamano ya CHADEMA Jiji la Mbeya-Picha na Matukio

Kuna mtu alishawahi kushauri huku kwenye mtandao kuwa kuna haja ya kitengo cha habari cha CDM kujipanga vizuri. Pamoja na kuwa siku-comment kwenye thread hiyo, lakini nilikubaliana na mtoa mada kimya kimya. Ukimya huo naona unanishinda kwa leo. Ni kipi kinazuia kitengo hicho kuwa na kamera, laptop na modem ya voda yenye kifurushi cha sh30000 kwa mwezi?

Ni vyema Mhe. Regia anayeongoza kitengo hicho na timu yake wakajipanga vyema. Ikumbukwe kuwa wakati maandamano au shughuli fulani ya chama (public event) inapofanyika pahali; wanachama na wapenzi wa CDM walio mbali na tukio wanakuwa wanashiriki kwa namna moja ama nyingine. Njia nzuri ya kuwashirikisha kikamilifu, hasa wale tunaoonana kwenye mtandao wa JF ni kuhakikisha taarifa zote muhimu na sahihi zinafikishwa kwa wakati.

Matukio kama ya leo ni sawa na mechi kubwa za kimataifa ambazo hurushwa hewani moja kwa moja na mashabiki wakashiriki furaha ya mchezo hata kama hawapo kwenye eneo la mchezo. Kwa kukosa picha hadi wakati huu ni kutunyima furaha ya "mchezo wa ligi" ya leo na hivyo kuwapa nafasi timu pinzani kutunyanyasa hapa mtandaoni kwa kutumia udhaifu huo.

Naomba kutoa hoja!
 
CDM walivyoanza maandamano walisema ni kwa ajili ya kupinga ulipwaji wa DOWANS, je na Nyanda za juu kusini ni nini, DOWANS pia, tunataka ruzuku itumiwe katika kuleta chachu ya maendeleo na si kununua magwanda na kutalii mikoani.

Ndugu yangu Gamba jipya,kumbe wewe unadhana maendeleo yanafanywa kipropaganda kama ilivyozoeleka na chama chako cha Magamba?
Kumbuka maendeleo yanamchakato wake,na mchakato ndio kama unavyoona ulianzishwa na CDM na bado unazidi kupiga kasi,for instance kujivua gamba kwa chama kilichoko madarakani ni kutokana na mchakato ninaouzungumzia hivi sasa,ambao bila cdm kuwafanya watz kufahamu jinsi wanavyoibiwa na hao wavua magamba bado mpaka sasa wangekuwa wameyavaa.Sasa wameyavua,hii ni sababu ya maandamano ya cdm na hapo mwenyewe utakubaliana nami kuwa maendeleo ya nchi hii yanaletwa na cdm kwa kuwashurutisha wavua magamba kimchakamchaka.
Sasa je unahitaji uumbwe na macho mangapi ili uyashuhudie haya ninayoyasema?Ondoa kizibo kwenyeubongo wako ili uweze kuona mbele.
 
Leo hali ngumu Mbeya nimeongea sasa hivi na jamaa yangu ananiambia watu hamna kabisa mji mweupe, Chadema taingia mwanzo niliwapa ushauri hizo pesa za ruzuku mnazofanyia maandamano na kugawana posho si bora mgechimba visima au kununua madawati watoto wetu wasome Watanzania labda wangewaelewa, sasa leo mpaka saizi saa kumi jioni picha za maandamano mtihani Regia Mtema mtamlaumu bure watu amna, sasa sijui leo mtagawanaje posho na watu amna imekula kwenu wana Chadema inauma sana
 
GB!

Jamaa wameshikwa pabaya, AR walisababisha watu kupoteza maisha kwa ajili ya madaraka ya umeya, lakini sasa wamekubali walichemsha, wanaomba unaibu meya, maandamano ya AR hayakuwa na maana yoyote, wamekuja kujua wakati ni too late.

Hili la kufanya maandamano Njanda za juu kusini kwa kodi zetu ili kuwasafisha mapacha watatu inabidi tuzifanyie kazi, na kama ni kweli wanyimwe vibali vya maandamano na mikutano ya wazi.

Slaa anazunguka Tanzania nzima kuwaambia watu kuwa mapacha 3 wameonewa, kweli huyu mzee ana akili ? hashishi anayo vuta safari hii nadhani ni imelimwa kwenye mkondo wa maji machafu, kwani ndio huwa kali sana
 
Ndugu yangu Gamba jipya,kumbe wewe unadhana maendeleo yanafanywa kipropaganda kama ilivyozoeleka na chama chako cha Magamba?
Kumbuka maendeleo yanamchakato wake,na mchakato ndio kama unavyoona ulianzishwa na CDM na bado unazidi kupiga kasi,for instance kujivua gamba kwa chama kilichoko madarakani ni kutokana na mchakato ninaouzungumzia hivi sasa,ambao bila cdm kuwafanya watz kufahamu jinsi wanavyoibiwa na hao wavua magamba bado mpaka sasa wangekuwa wameyavaa.Sasa wameyavua,hii ni sababu ya maandamano ya cdm na hapo mwenyewe utakubaliana nami kuwa maendeleo ya nchi hii yanaletwa na cdm kwa kuwashurutisha wavua magamba kimchakamchaka.
Sasa je unahitaji uumbwe na macho mangapi ili uyashuhudie haya ninayoyasema?Ondoa kizibo kwenyeubongo wako ili uweze kuona mbele.

Chama cha Democrasia na Mapacha watatu.
 
Ziara ya Kufanya Maandamano inayofanywa na CDM nyanda za Juu Kusini sasa imedhihilisha kuwa CDM ni Chama Cha Demokrasia na Maandamano! CDM imekuwa inatangazia Watanzania kuwa tutakua na Maandamano Mikoa ya Kusini pasipo kutoa hoja ya Msingi ya Kukusanya watu zaidi ya Maandamano! Yani kina wahamasisha watu waende kuandamana! Hoja hapa ni Kuandamana! Kwenye Kikao Cha Kamati Kuu ya CDM iliyo kaa wiki iliyopita kulikua na mkanganyiko kwa wajumbe kutanguliza neno maandamano kama agenda ya kwenda Mikoa ya kusini! Walio tetea zaidi ni Mbowe,Slaa na Lema na ndio vinara wa maandamano! Hakuna ubishi sasa CDM ni Chama cha Demokrasia na Maandamano! Neno maendeleo limepata natural death kutokana na mwenendo wa sasa wa CHADEMA!
 
Ndugu yangu Gamba jipya,kumbe wewe unadhana maendeleo yanafanywa kipropaganda kama ilivyozoeleka na chama chako cha Magamba?
Kumbuka maendeleo yanamchakato wake,na mchakato ndio kama unavyoona ulianzishwa na CDM na bado unazidi kupiga kasi,for instance kujivua gamba kwa chama kilichoko madarakani ni kutokana na mchakato ninaouzungumzia hivi sasa,ambao bila cdm kuwafanya watz kufahamu jinsi wanavyoibiwa na hao wavua magamba bado mpaka sasa wangekuwa wameyavaa.Sasa wameyavua,hii ni sababu ya maandamano ya cdm na hapo mwenyewe utakubaliana nami kuwa maendeleo ya nchi hii yanaletwa na cdm kwa kuwashurutisha wavua magamba kimchakamchaka.
Sasa je unahitaji uumbwe na macho mangapi ili uyashuhudie haya ninayoyasema?Ondoa kizibo kwenyeubongo wako ili uweze kuona mbele.

Enhe, hebu tueleze wanaibiwaje ?
 
Mkuu nachojaribu kuelezea ni kwamba, kodi zetu wanazopewa kama ruzuku zitumike kwa utashi wa hali ya juu, wawekeze kwenye ofisi za majimbo, wilaya, mikoa na taifa, ili come 2015 wawe wametapakaa kiutendaji sio kuuza sura tuu.
Kuwekeza katika ofisi bila kuaanda au kuwahamasisha wananchi na kuelewa nini hasa kinacho hitajika ni sawa ya kujenga majengo kama zilivyo shule za kata,msingi,zahanati zisizo na walimu na madaktari wakati mwingine wanafunzi na miradi mingi ya CCM ambayo kumbukubu inayobaki si zaidi ya majengo ambayo hayana uangalifu na hayana faida kwa wananchi.Kutokana na mipango ya CCM ambapo kujenga ofisi za CCM, shule zahanati na miradi mingi dhana au walengwa sio wananchi bali ni upenyo wa viongozi hao kujipatia fedha na wananchi kurithi majengo yasio na tija.Pesa ya kujenga ofisi moja ya chama inaweza kutumika vizuri kwa mikutano na maandamano ambayo itawahamasisha,kuwaelimisha watu wengi zaidi ambao mbali na kupata mwamko wa kutosha wanaweza kua zao la kujenga ofisi kwa kwa kujitolea au hata hizo zitakazojengwa kuzitunza na kutumika kuendeleza moto uliowashwa na maandamano na mikutano.Hapa CHADEMA moto wanaouwasha wanauwasha kwa kiberiti na cheche zake kusambaa kote,CCM wanawasha moto kwa KURUNZI mwanga wake unakuwepo kwakati wa ziara za viongozi wakiondoka wanaondoka nao. OFISI AU MAJENGO PASIPO NA UFAHAMU WA ITIKADI NA FALSAFA YA CHAMA KWA WALENGWA NI MWILI BILA MOYO HIVYO NI UPUUZI.Hili unaweza kuliona kwa kutizama hali ya ofisi za CCM.
 
Slaa anazunguka Tanzania nzima kuwaambia watu kuwa mapacha 3 wameonewa, kweli huyu mzee ana akili ? hashishi anayo vuta safari hii nadhani ni imelimwa kwenye mkondo wa maji machafu, kwani ndio huwa kali sana

Akirudi Dar mwisho wa Mwezi anakula milioni saba 7,000,000 pamoja na marupurupu na posho za maandamano, huku wapiga kura wake hata mlo mmoja kwa siku hawapati.
 
CDM walivyoanza maandamano walisema ni kwa ajili ya kupinga ulipwaji wa DOWANS, je na Nyanda za juu kusini ni nini, DOWANS pia, tunataka ruzuku itumiwe katika kuleta chachu ya maendeleo na si kununua magwanda na kutalii mikoani.[/QU

Ni Malaria Sugu.
 
Slaa anazunguka Tanzania nzima kuwaambia watu kuwa mapacha 3 wameonewa, kweli huyu mzee ana akili ? hashishi anayo vuta safari hii nadhani ni imelimwa kwenye mkondo wa maji machafu, kwani ndio huwa kali sana

Kitu cha AR kutoka kwa Godbless, lol
 
GB!

Jamaa wameshikwa pabaya, AR walisababisha watu kupoteza maisha kwa ajili ya madaraka ya umeya, lakini sasa wamekubali walichemsha, wanaomba unaibu meya, maandamano ya AR hayakuwa na maana yoyote, wamekuja kujua wakati ni too late.

Hili la kufanya maandamano Njanda za juu kusini kwa kodi zetu ili kuwasafisha mapacha watatu inabidi tuzifanyie kazi, na kama ni kweli wanyimwe vibali vya maandamano na mikutano ya wazi.

haaaaaah haaaaaaaa....mbumbumbu utamjua tu.Hivi wewe hujui kuwa unaweza kumyima mtu chakula kwa sababu zako mwenyewe,lakini si democrasia ?? Democrasia hii si mali ya magamba ndugu yangu kama unataka tz uione kama Libya wanyimeni democrasia yao muone .....tatizo mlishatuona wabonbo maboguz sana kumbukeni huo wakati umekwisha pitwa na wakati na hilo viongozi wako wanalijua.
Na hao,mapacha watu wanaihusu nini cdm? jipya hamna nyie, iwaibue cdm na ile matapishi yake eti kuwasafisha?
 
Hoja mkuu, mwaga hoja mkuu, tunajadili hoja hapa.

Maslahi ya Taifa Mbele.
 
Regia Mtema mbunge wa kupewa wa maandamano, baada kuona leo watu wamegoma kwenda kwenye maandamano ya wahuni kafupisha maandamano kasema leo wataandamana kilomita mbili tu. kama kutoka K,koo mpaka Mnazi mmoja sasa hayo ni maandamano au uhuni tu wa kugawana pesa zetu walipa kodi
 
Back
Top Bottom