OSOKONI
JF-Expert Member
- Oct 20, 2011
- 10,965
- 5,336
Maandamano ya kupinga muswada wa sheria wenye utata kuhusu kulinda taarifa za siri za serikali yameanza katika miji mbalimbali nchini Afrika Kusini.
Muswada huo unatarajiwa kupitishwa hii leo na bunge la nchi hiyo.
Askofu Desmond Tutu ameueleza muswada huo kuwa haufai na ni matusi kwa wananchi wa Afrika Kusini.
Tahariri katika magazeti yote makubwa nchini humo zimeonya kuwa sheria hiyo itawapeleka jela waandishi wa habari watakaofichua kashfa za serikali, kama ilivyokuwa wakati wa utawala wa kibaguzi.
Chama tawala cha African National Congress, ANC kinasema sheria hiyo inahitajika ili kulinda siri za serikali na inaendana na sheria za kimataifa.
[h=2]Taarifa zinazohusiana[/h]
[h=2]Afrika Kusini [/h]
- Muswada tata wapingwa Afrika Kusini dakika 42 zilizopita