Nyakarungu
JF-Expert Member
- May 1, 2011
- 472
- 377
Habari zenu ndugu zanguni,
Leo napenda kufafanua kidogo kuhusu huu msamiati pengine ni tata kwa baadhi ya watu.
Utangulizi,
Watumishi wote wa serikali walioajiriwa majina yao yapo kwenye paroll ya serikali, mishahara yao inapitia hazina ndogo, inakatwa kodi na makato mengine, kama vile fao la ustaafu, mkopo na mengine.
Ili mtumishi alipwe jasho lake ni lazima mkurugenzi wake athibitishe kuwepo kwake kwa kipindi husika ma orodha ya watumishi waliopo kila mwezi huwasilishwa hazina ndipo mishahara yao huwekwa kwenye akaunti zao za benk
Na ikiwa mtumishi hakuwepo kwa kipindi hicho bila taarifa mshahara wake husimamishwa kwa barua maalum au taarifa maalumkutoka kwa mkurugenzi kwenda hazina ndogo
Watumishi hewa
Watumishi hewa ni watumishi ambao mishahara yao inalipwa kwa halimashauri husika bila wao kuwepo kazini kwa utoro wa makusudi au kwa kuachishwa kazi, kufariki dunia au kufukuzwa kazi
Kwa hali kama hii mkurugenzi alitakiwa atoe taarifa hazina ndogo ili isimamishe mishahra hiyo kabla ya hatua zaidi, inapotokea mtumishi anaendelea kulipwa bila uwepo wake ni uzembe au makusudi ya idara yake ya nidhamu, na mara nyingi mishahara hii huwa haiwafikii hao watumishi hewa bali huishia mikononi mwa mkurugenzi au mkuu wa idara yake
Mifano
Mkurugenzi anapogundua mtu fulani ameacha kazi au amefukuzwa au kufa, huacha kupeleka taarifa za huyo mtumishi hazina na badala yake huchukua yeye mshahara huo kirahisi sana, na pengine huchukua taarifa za mtumishi na kufungua akaunti mpya na kubadilisha akaunti kisha mshahara huanza kwenda huko au huuchukua mshahara kama ulivyo kabla ya kupelekea haziana
Pili wakurugenzi na wakuu wa idara huweza hata kuomba mikopo kwa kutumia details za watumishi hao na hupewa vyema,
Tusije tukadhani watumishi hewa wanapata hata huo mshahara bali ni hao mabosi huko kwenye vitengo na idara za serikali huko mikoani na wilayani wanafaidi pesa za nchi
Wakisakwa hao watumishi hewa wapatikane kisha uchunguzi ufanyike mtathibitisha kuwa wamepokea pesa miaka kadhaa lakini hazikuwa zikifika kwenye akaunti zao, hivyo pesa zilikuwa zikichukuliwa na wajanja
Nimeamua kuandika hili baada ya kuona wengi wakidhania kwamba watumishi hewa walikuwa wakipata hizo pesa kitu kisicho kweli, hili nimeliandika kutokana na uzoefu wangu katika utumishi na mmoja wa waathirika wake
Mtemi Nyakarungu. 0754 459 572