Abuu Dharr
JF-Expert Member
- Dec 28, 2017
- 2,912
- 3,022
- Thread starter
- #21
Sababu kuu 2mkuu mbona mashehe wengi wanahusishwa na ushirikina hawa wakimajini.
tatizo ni nini
1)Ujinga
2)Njaa
Sababu kuu 2mkuu mbona mashehe wengi wanahusishwa na ushirikina hawa wakimajini.
tatizo ni nini
AminUshirikina ni kufanya Ibada kwa asiyekuwa Allah, au kumchanganya Allah na kiumbe katika Ibada
ZINGATIO
Ibada ni nini?!
IBADA,ni jina lenye kukusanya,kila anachokipenda Allah na kukiridhia,katika kauli na matendo ya dhahiri au ya siri
Turudi katika mada
Uislam ndio Dini pekee inayopiga Vita Ushirikina na aina zake Allah anasema katika suratul Luqmaan akisimulia kisa cha mja mwema,pale akimuasa mwanae anasema Kumbuka aliposema Luqmaan kumwambia mwanae,ilihali akimpa nasaha,''Ewe mwanangu, usimshirikishe Allah,Hakika ya Shirki,ni dhulma kubwa''
AINA ZA USHIRIKINA
Ushirikina umegawanyika sehemu kuu mbili
1)USHIRIKINA MKUBWA
2)USHIRIKINA MDOGO
USHIRIKINA MKUBWA
Ni kufanya Ibada kwa asiekuwa Allah au kumchanganya Allah na kiumbe mfano Kuabudu Majini,Mizimu,Miti nk
Aina hii ya ushirikina inamtoa mtu katika Uislam
USHIRIKINA MDOGO
Shirki ndogo,ni sawa na riyaa(kufanya jambo kwa kujionyesha) Jambo hili,Halimtoi mtu katika Uislam,Bali lile tendo alilolifanya kisha akalichanganya na ushirikina mdogo,ndio tendo pekee litakalokataliwa kwamaana halitapokelewa na kukubaliwa kisheria
Tunamuomba Allah atuepushe na shirki na mfano wake