Maana ya Ushirikina na aina zake

Maana ya Ushirikina na aina zake

Abuu Dharr

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2017
Posts
2,912
Reaction score
3,022
Ushirikina ni kufanya Ibada kwa asiyekuwa Allah, au kumchanganya Allah na kiumbe katika Ibada

ZINGATIO
Ibada ni nini?!
IBADA,ni jina lenye kukusanya,kila anachokipenda Allah na kukiridhia,katika kauli na matendo ya dhahiri au ya siri

Turudi katika mada
Uislam ndio Dini pekee inayopiga Vita Ushirikina na aina zake Allah anasema katika suratul Luqmaan akisimulia kisa cha mja mwema,pale akimuasa mwanae anasema Kumbuka aliposema Luqmaan kumwambia mwanae,ilihali akimpa nasaha,''Ewe mwanangu, usimshirikishe Allah,Hakika ya Shirki,ni dhulma kubwa''

AINA ZA USHIRIKINA
Ushirikina umegawanyika sehemu kuu mbili
1)USHIRIKINA MKUBWA
2)USHIRIKINA MDOGO


USHIRIKINA MKUBWA
Ni kufanya Ibada kwa asiekuwa Allah au kumchanganya Allah na kiumbe mfano Kuabudu Majini,Mizimu,Miti nk

Aina hii ya ushirikina inamtoa mtu katika Uislam

USHIRIKINA MDOGO
Shirki ndogo,ni sawa na riyaa(kufanya jambo kwa kujionyesha) Jambo hili,Halimtoi mtu katika Uislam,Bali lile tendo alilolifanya kisha akalichanganya na ushirikina mdogo,ndio tendo pekee litakalokataliwa kwamaana halitapokelewa na kukubaliwa kisheria

Tunamuomba Allah atuepushe na shirki na mfano wake
 
HATARI ZA USHIRIKINA


Kumfanyia Allah mwenza/mshirika,ni katika Dhulma kubwa,ni sawa na kumfanyia uadia katika haki yake pekee

Kumpwekesha Mola,ni jambo Mama,na ni upeo wa juu katika uadilifu
na kumshirikisha Mola,Ni tendo baya na Dhulma iliyovuka mipaka,kwasababu,unampunguzia Haki yake yule aliekuleta katika Dunia hii.
Ushirikina ni dhambi kubwa mno,Yeyote mwenyewe kuabudu pasi na Mola,Basi hakika,ameweka jambo sehemu isiyostahiki,na hii,ni aina ya Dhulma
 
Mola anasema ndani ya Quraan

{وَلَقَدْ أُوحِيَ إِلَيْكَ وَإِلَى الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكَ لَئِنْ أَشْرَكْتَ لَيَحْبَطَنَّ عَمَلُكَ وَلَتَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ (65)} [الزمر/65].
Hakika Umefunuliwa(Ewe Mohammad)kama walivyofunuliwa waliopita kabla yako(Mitume),Ikiwa utamshirikisha Allah,Basi yataporomoka matendo yako,na utakuwa katika wale waliopata hasara
 
angalia Hadithi hii tukufu
وعن أبي بكرة رضي الله عنه قال: قال النبي- صلى الله عليه وسلم-: «أَلا أُنَبِّئُكُمْ بِأَكْبَرِ الكَبَائِرِ؟» ثَلاثاً، قاَلوُا: بلَىَ ياَ رَسُولَ اللهِ، قَالَ: «الإشْرَاكُ بِاللهِ، وَعُقُوقُ الوَالِدَيْنِ»، وَجَلَسَ وَكَانَ مُتّكِئاً «أَلا وَقُولُ الزُّوْرِ» قَال: فَمَا زَالَ يُكَرِّرُهَا حَتَّى قُلْنَا: لَيْتَهُ سَكَتَ. متفق عليه.

Kutoka kwa Abubakar,Allah amridhie,amesema,amesema Mtume wa Allah Rehma na amani ziwe juu yake
Hivi nisikuambieni madhambi matatu makubwa?!!!

wakasema Maswahaba,tuambie ewe Mtume wa Allah
akasema
1)Kumshirikisha Mola
2)kuwafanyia vibaya wazazi wawili
akakaa,na alikuwa ameegemea kitu
3)Na Maneno ya uongo
na hakuacha kuwa ni mwenye kurudia rudia,akisema
na maneno ya uongo
 
Allahumma Amiin
atujaalie sote kwa pamoja
aamin,
ila naomba ufafanue kwa upana kidogo kuhusu aina ya shirki, yani hizo kubwa na ndogo. nahisi km nahitaji ufafanuzi na mifano ya shirki hizo zaid sheikh. Allah akuongoze vema..
 
aamin,
ila naomba ufafanue kwa upana kidogo kuhusu aina ya shirki, yani hizo kubwa na ndogo. nahisi km nahitaji ufafanuzi na mifano ya shirki hizo zaid sheikh. Allah akuongoze vema..
In sha Allah Chief
 
Hivi elimu ya falaq sio moja ya mafundisho ya Kiislam??

Huo sio ushirikina??
 
Hakuna Elimu hiyo katika Uislam


usidhani kisa imeitwa au kuandikwa kwa kiarabu,Basi Uislam unaingia hapo


Uislam
upo mbali na jambo hilo ndg

Elimu ya Falaq, kiswahili inaitwa Elimu ya nyota

kuna wanaotumia kwa ajili ya ushirikina,
Hapa anaingia mtu yoyote yule mwenye kuabudu ushirikina
 
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ



02- Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno

Shirki Ni Aina mbili Na Tofauti Zake





Shirki ni aina mbili; shirki kubwa na shirki ndogo.



Shirki kubwa inamtoa mtu nje ya Uislamu, ‘amali zake zote zinaporomoka, mwenye kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa shirki kubwa huwa ni halali damu na mali yake na ni mwenye kudumu Motoni ikiwa hatotubia kabla ya kufariki kwake. Na dhambi ya shirki kubwa ni dhambi pekee ambayo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Hamsamehe mja atakapokufa bila kutubia. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ۚ

Hakika Allaah Haghufuri kushirikishwa; lakini Anaghufuria yasiyokuwa hayo kwa Amtakae. [An-Nisaa: 48]



Shirki kubwa ni kuelekeza ‘ibaadah na kuomba du’aa kwa asiyekuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Washirikina wao ndio kabisa hawamwabudu Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) japokuwa huenda wengine wanaamini kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ndiye Muumba kama walivyoamini hivyo washirikina wa Makkah. Shirki yao imethibiti katika ‘Uluwhiyyah (‘ibaadah) pale walipoabudu masanamu wakidai kuwa yanawakurubisha kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kama ilivyotajwa katika Qur-aan:

وَالَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ مَا نَعْبُدُهُمْ إِلَّا لِيُقَرِّبُونَا إِلَى اللَّـهِ زُلْفَىٰ

na wale waliojichukulia badala Yake walinzi (wakisema): “Hatuwaabudu isipokuwa ili watukurubishe kwa Allaah ukaribio.” [Az-Zumar: 3]



Wengine ndio wamemshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na viumbe Vyake wakawafanya ni ilaah wao. Juu ya hayo, Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anamghufuria yeyote yule anayerudi kutubia Kwake baada ya kufuru na shirki kubwa kama hizo. Dalili ni kauli zifuatazo katika Qur-aan:

لَقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ ۖ وَقَالَ الْمَسِيحُ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اعْبُدُوا اللَّـهَ رَبِّي وَرَبَّكُمْ ۖ إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ ﴿٧٢﴾ لَّقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ ثَالِثُ ثَلَاثَةٍ ۘ وَمَا مِنْ إِلَـٰهٍ إِلَّا إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۚ وَإِن لَّمْ يَنتَهُوا عَمَّا يَقُولُونَ لَيَمَسَّنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٧٣﴾ أَفَلَا يَتُوبُونَ إِلَى اللَّـهِ وَيَسْتَغْفِرُونَهُ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٧٤﴾

Kwa yakini wamekufuru wale waliosema: “Hakika Allaah ni Al-Masiyh mwana wa Maryam.” Na Al-Masiyh alisema: “Enyi wana wa Israaiyl! Mwabuduni Allaah, Rabb(Mola) wangu na Rabb wenu. (Kwani) Hakika mwenye kumshirikisha Allaah bila shaka Allaah Atamharamishia Jannah, na makazi yake yatakuwa ni Motoni. Na madhalimu hawatopata mwenye kunusuru yeyote.”



Kwa yakini wamekufuru wale waliosema: “Hakika Allaah ni watatu wa utatu. ”Na hali hapana ilaah (muabudiwa wa haki) isipokuwa IlaahMmoja (Pekee). Na wasipoacha yale wanayoyasema, bila ya shaka itawagusa wale waliokufuru miongoni mwao adhabu iumizayo.



Je hawatubii kwa Allaah na wakamwomba maghfira? Na Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu). [Al-Maaidah: 72-74]



Ama shirki ndogo ambayo inakulikana kwa “riyaa” ni kufanya ‘ibaadah au kutenda amali zenye kumridhisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) lakini kwa niyyah ya kujionyesha kwa watu. Shirki hii haimtoi mtu nje ya Uislamu bali ‘amali zake huporomoka na, ni mwenye kuadhibiwa Motoni kwa kadiri ya madhambi yake.



Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amewahofia Swahaabah aina hii ya shirki:



عن مَحْمُودِ بْنِ لَبِيدٍ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إنَّ أخوَفَ ما أخافُعليكم الشِّركُ الأصغرُ، قالوا: وما الشِّركُ الأصغر؟ قال: الرِّياءُ، يقولُ اللهُ عزَّ وجلَّ لأصحابِ ذلك يومَ القيامةِ إذا جازَى النَّاسَ اذهبوا إلى الَّذين كنتم تُرائون في الدُّنيا فانظُروا هل تجِدون عندهم جزاءً؟" - صححه الألباني في السلسلة الصحيحة (951 )

Imepokelewa kutoka kwa Mahmuwd bin Labiyd ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: Hakika nnachokihofia kwenu zaidi ni shirki ndogo. Wakasema: Ni ipi hiyo shirki ndogo? Akasema: Ar-Riyaa. Allaah ‘Azza wa Jalla Atawaambia watu wa Siku ya Qiyaamah pale watakapolipwa watu jazaa: Nendeni kwa wale mliokuwa mkijionyesha kwa ‘amali zenu duniani kisha tazameni je, mtakuta kwao jazaa? [Ahmad na ameisahihisha Shaykh Al-Albaaniy katika Silsilat Al-Hadiyth Asw-Swahiyhah (951)]
 
Allaah (Ta´ala) amesema:

قُلْ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ لَا شَرِيكَ لَهُ

“Sema: “Hakika Swalaah yangu na kichinjwa changu na uhai wangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Allaah Pekee, Mola wa walimwengu – hana mshirika.”[1]
 
mkuu mbona mashehe wengi wanahusishwa na ushirikina hawa wakimajini.
tatizo ni nini
 
Back
Top Bottom