Maana ya udikteta ni nini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maana ya udikteta ni nini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TZ biashara, Apr 15, 2012.

 1. TZ biashara

  TZ biashara JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 523
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nimeona mara nyingi watu wakizungumzia udikteta lakini tafsiri huwa zinatofautiana.Kuna wengine wanaitafsiri kwamba kiongozi anayekaa madarakani kwa muda mrefu ndio dikteta.

  Na kunawengine wanasema kwamba raisi anaeongoza nchi kwa sheria kali ndio dikteta.Na vilevile wengine wanaona kiongozi anayeua na kuweka amri kama za kijeshi ndio dikteta. Nadhani wapo wengine wanazo tafsiri zingine labda sizijui.Je na wewe unaitafsiri vipi kuhusiana na udikteta.

  Maana wengine utawasikia wanasema bora ya kutawaliwa na dikteta.Lakini kwamimi nadhani udikteta ni hatari sana kwasababu mwananchi atakosa uhuru wake katika maisha yake na vilevile kunakuwa hakuna haki za kibinaadamu.Kiongozi atakuwa na uwezo wa kumiliki nchi pamoja na mali zote za nchi.

  Na anauwezo wa kutoa amri au kama mmiliki sehemu zote kama mahakama,Polisi na jeshi.Hata Media zote zinakuwa chini ya kiongozi na kuwaweka waandishi wa habari kutokuwa huru kutoa habari za ndani ya nchi.

  Hata upigaji kura vilevile pengine hatoruhusu kuwa na mpinzani au kuweka kura ya ndio au hapana.Sasa sijui wale wenye kuomba kutawaliwa kidikteta wanatafsiri vipi kuhusu udikteta.
   
Loading...