Maana ya Neno " Toothpick" Kwa kiswahili

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,142
13,216
Hili neno linasumbua wengi (wengine wameishia kuita hivyo hivyo, wengine huita vijiti vya meno na wengine huita kichokonoo hasa kule Zbar) lakini naomba kushirikisha hapa kwamba maana yake ni kimbaka, vikiwa vingi vimbaka...(mchango zaidi)

Chanzo: Malenga wa Kiswahili-Kipindi cha kiswahili TBC FM
 
.....Ngojeni kwanza, mnadhani chanzo cha matatizo mashuleni ni Kiswahili? Hata kama una mwalimu anayejua kuwa “kimbaka” ni neno la Kiswahili lenye maana “tooth-pick”, ni kielelezo tosha kuwa wanafunzi watamuelewa?

www.vijana.fm/2010/10/11/swahili-labs/
 
Nakuomba ubadilishe kichwa cha habari kisomeke 'Tafsiri ya neno toothpick'. Unapotumia neno ' maana' ni kama unataka kuelezea kitu. Mfano, Nini maana ya Ngamizi mpakato? Atakayekujibu atakuelezea ni kitu gani. Naye akisema ni Laptop atakuwa amekosea kwasababu Laptop ni tafsiri ya ngamizi mpakato.

Hili la kimbaka au vimbaka sina ufahamu nalo na kama ndivyo nashukuru kuleta msamiati.
 
Jibu limo kwenye swali. Kichokoo au kichokoleo na hayo mengine uliyotoa ya kimbaka na vimbaka ambayo mie sikuwa nikiyaenga wala kuyamanya. Kama utafanya translitilation itakuwa kichokoa jino.
 
kichukua meno!
sio kila kitu lazima utafsiri kwa kiswahili,ni bora uende ukahimize waislamu kuhesabiwa
 
Nakuomba ubadilishe kichwa cha habari kisomeke 'Tafsiri ya neno toothpick'. Unapotumia neno ' maana' ni kama unataka kuelezea kitu. Mfano, Nini maana ya Ngamizi mpakato? Atakayekujibu atakuelezea ni kitu gani. Naye akisema ni Laptop atakuwa amekosea kwasababu Laptop ni tafsiri ya ngamizi mpakato.

Hili la kimbaka au vimbaka sina ufahamu nalo na kama ndivyo nashukuru kuleta msamiati.
Hii kwenye bluu nilikuwa naitafuta sana....
 
sasa mpaka watz woote tujue laptop ni ngamizi mpakato na kuweza kutumia msamiati huu katika maisha ya kila siku, wenzetu watakuwa hawatumii tena hizo ngamizi mpakato......
na Ipad nayo inaitwaje?

nadhani ifike wakati tafsiri ya hivi vitu vinavyoletwa zifanyike mapema wakati uleule ambao ndio kazi ya usambazaji imeshika hatamu.
 
Back
Top Bottom