Mrima (kwa
Kiingereza:
Mrima Coast) ni
jina la sehemu ya
pwani ya
Afrika ya Mashariki inayotazama
Zanzibar. Wenyeji wake walijulikana kama
Wamrima ilhali kati yao walikuwa watu wa
makabila mbalimbali.
Kimrima kinahesabiwa kuwa kati ya
lahaja za Kiswahili.
Mipaka ya eneo hili ilielezwa tofauti katika vyanzo vya
kihistoria. Kwa jumla ilieleweka Mrima ilihusu ukanda wa pwani hadi
umbali wa matembezi ya
siku mbili hivi kutoka
mwambao kuelekea
bara, kwa hiyo takribani
maili 20 au
kilomita 30-35.
Ludwig Krapf aliyekusanya habari zake mnamo
1844 -
1852 mjini Mombasa alitaja eneo la Wamrima kuwa lilianza upande wa
kaskazini kwa
Wavumba, yaani wasemaji wa
lahaja ya Kiswahili ya
Kivumba, wanaotazama
kisiwa cha Wasini (
Shimoni, Kenya), na kuendelea hadi
vilima vya Usambara na "nti ya Mrima" (nchi ya Mrima).
A.C. Madan aliyekusanya habari za
kamusi yake mnamo
1890 pale Zanzibar, alitaja Mrima kuwa eneo kati ya "Oassi" (
Wasini) hadi
Kipumbwi kwenye
mdomo wa
mto Msangasi, takriban km 25 upande wa
kusini ya
Pangani.
Krapf na Madan wanaeleza
jina la "Mrima" kutokana na
matamshi tofauti ya "
mlima", yaani "nchi chini ya milima" (Krapf) au nchi inayopanda juu kuanzia mwambao (Madan).
Watafiti wengine walikuta matumizi ya jina hili kwa eneo pana zaidi upande wa kusini, mfano C. H. Stigand alieleza
lahaja ya Kimrima kuenea kuanzia
Vanga (
Kenya) hadi karibu na
Kilwa
Nchini Kenya kuna
kijiji cha Mrima na
kilima cha Mrima takriban km 20 upande wa kaskazini wa
Vanga,
Kaunti ya Kwale.
Fungu Mrima (pia Fungu Marima) ni
kundi la
miamba ya
matumbawe baharini kati ya
Kisiwa cha Mafia na bara.
(Chanzo:
Mrima - Wikipedia, kamusi elezo huru)