Maana na umuhimu wa hati miliki

Surveyormunkondya

New Member
Dec 22, 2019
3
6
*FAIDA ZA KUWA NA HATI MILIKI YA KIWANJA AU NYUMBA*

*Hati miliki ni nini?*
-Ni document ya kisheria inayoonyesha mmiliki wa kipande cha ardhi. Ikionyesha ramani ya upimaji ya eneo husika, ukubwa wa eneo, mipaka ya eneo husika(beacons au mawe) pamoja na ramani za upimaji za majirani.

*Hati miliki inapatikana vipi?*
Hati miliki inapatikana baada ya eneo husika kuandaliwa ramani ya mipango miji na atimaye kuweza kupimwa na kuandaliwa ramani ya upimaji, Baada ya hapo unaweza kumilikishwa eneo lako kwa kupewa hati miliki.

*Hati miliki unaipata toka kwa nani?*
Hati miliki ya viwanja au maeneo mengine ambayo yapo ndani ya mji uwa zinatolewa na wizara ya ardhi kwa kupitia halmashauri/manispaa husika. Baada ya eneo lako kufanyiwa upimaji na mpima ardhi (Land Surveyor)

*Kuna umuhimu wowote wa kuwa na hati miliki?*
Umuhimu upo tena mkubwa sana ukiwa na hati miliki inakuzuia kupunguza migogoro kwa kuwa utakua mmiliki wa eneo au kiwanja kisheria, unaipandisha thamani ardhi, pia unaweza tumia kama dhamana kwenye taasisi za kifedha kwa kuchukulia mkopo.

*Je kuna tatzo lolote usipokua na hati miliki?*
Matatzo yapo mfano uwezekano wa kubomolewa eneo lako kama hujajenga eneo husika mfano(eneo la hifadhi ya barabara, reli n.k, wazi, makaburi n.k), uwezekano wa kuzurumiwa ardhi yako kwa kuwa humiliki kisheria, kiwanja kuwa na thamani ndogo (kushindwa kuchukulia mikopo na kulipwa fidia ndogo endapo serikal itahitaji eneo lako).
Kumiliki ardhi kisheria ni kuwa na hati miliki ambayo inakutambulisha wewe kuwa ni mmiliki halali wa eneo au kiwanja.
*KWA UHITAJI WA YAFUATAYO*
-Kupima ardhi
-kujua ukubwa eneo lako.
-kujua kama eneo lako lina mchoro wa mpango mji.
-kujua kama eneo lako limepimwa au halijapimwa.
-kujua matumizi ya eneo kabla ya kujenga au kununua ili kuepuka kubomolewa..
-Namna ya Kupata hati miliki
-ushauri juu ya masuala ya ardhi
-Na jambo lolote linalo husu ardhi.
Tafadhari wasiliana nami;
By
*Surveyormunkondya*
(MPima ardhi na mtaalam wa masuala ya ardhi.)
MAWASILIANO.
calls&whatsapp
0673540985
0765532858
Au fika ofisini rufungira,mwenge katika jengo la SAVEI PLAZA ground floor nyuma ya calabash pub.

*UKITAKA KUJIUNGA NA GROUP LA WHATSAPP FUATA LINK HII.*

"ELIMU KUHUSU ARDHI"

*Share kwa watu wengi zaidi nao waepuke na matatizo ya ardhi kwa kupata elimu juu ya masuala ya ardhi.*

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je, yawezekana kupata Hati miliki kama Kiwanja hakijatambuliwa na Mamlaka ya mipango miji?

Kama haiwezekani, ni nini yaweza kuwa mbadala wake (nyaraka mbadala ya utambulisho wa ardhi) kwa kipindi cha kusubiri kufikia ardhi hiyo kutambuliwa na mamlaka/mipango miji? maana kwa nijuavyo mimi ni vigumu kwa Mtu mmoja tu kuibuka na kutafuta Hati miliki katikati ya eneo lisilo ndani ya mipango ya Halmahauri husika.
 
Back
Top Bottom