Maana halisi ya udini na utanzania

KGARE

Senior Member
Jul 31, 2012
108
39
Wakati nchi yetu ikinyemelewa (na pengine ishaanza kutafunwa) na siasa hatari ya udini, ni vizuri kama watanzania turejee msingi wa nchi yetu kuitwa “HAINA DINI”. Msingi ule ulikuwa ni kwamba wananchi waliachwa huru kuabudu kwa uhuru kulingana na imani zao, serikali haikushawishi wala kulazimisha raia wake waabudu katika siku Fulani au katika imani fulani bali iliwekwa wazi hata katika katiba kwamba kila raia ana uhuru wa kuabudu kulingana na imani yake. Kiongozi yeyote hatachaguliwa au kuteuliwa kutokana na imani au dini yake, ila atachaguliwa kuongoza wananchi wa dini zote. Serikali na wananchi hawakupaswa kuangalia profile ya dini za viongozi wao ili kuangalia uwiano wa aina yoyote. Hakutakiwa kuwe na idadi sawa za viongozi wa dini katika nyadhifa zozote. Mtu ateuliwe kulingana na sifa (competencewise not regionwise, tribewise nor religionwise) zinazohitajika ili kutumikia taifa katika nafasi husika.
Nchi inapaswa kuendelea kuwa haina dini, watu wajitahidi kutumikia watanzania bila kujali wanatoka eneo gani la nchi, au wana imani gani za dini. Tuwachague kwa uwezo wao kutumika hata kama itatokeaa (unawares) kwamba wametoka dini Fulani wote, au wote hawana dini. Tusitafute religious representation katika siasa.
ILIVYO (AU inavyoelekea kuwa) SASA;

  1. Tunatafuta kujua nani ana dini gani katika nafasi gani. Hii ni hatari na ndio mwanzo wa udini.
  2. Tunaangalia uwiano wa dini katika nafasi za uongozi…KWA MFANO: unakuta waislam au wakristo au wasio na dini rasmi wanaweza kulalamika “mbona kati ya viongozi 8 waliochaguliwa, dini yetu inao 2 tu?, Ooh, Kiongozi fulani anapendelea dini fulani kwa kuwa nayeye ni muumini wao!!’’ Hii ni hatari sana. Na wakati wengine wakidhani hii ndio kuepuka udini kumbe kiuhalisia huu ndio udini wenyewe.
  3. Tunaangalia chama Fulani na kuona viongozi wakuu wote wanaweza kuwa dini fulani,tena chama kimoja kinaweza kutumia majukwaa kuwashutumu chama kingine kwa hili hadi watu wakaanza kuhoji “ooh, mbona dini nyingine hamjazipa nafasi za juu?, ooh chama hicho ni cha dini Fulani tu, ooh mkiepuke chama hicho, ooh wekeni usawa wa nafasi kwa dini zote!!”. Tukidhani hii ni kuepuka udini, tunapotea, huu ndio udini wenyewe.
  4. Tunapotumia serikali kuwaamuru watu waache kufanya vitu fulani visivyokuwa kosa mbele ya sheria ya nchi, eti kwa kuwa dini fulani iko katika kipindi fulani, au kwa kuwa dini hiyo ina wafuasi wengi eneo hilo, ni hatari. Huu ndio udini wenyewe. Dini ziwafundishe waumini wao kuwa waaminifu katika yale wanayoyaamini hata katikati ya dunia isiyoamini, katikati ya majaribu makubwa ya dhambi na sio kuwashawishi wananchi wote (tena kwa kutumia serikali) waondoe majaribu hayo kwao ili wasitende dhambi.
Mamoja, wasiobaguana kwa maeneo/mikoa wanakotokaudini, wala kutumia dini kama mojawapo ya sifa...HUU NDIO UTANZANIA.

Najua kuna mengine mengi kama mifano ya hatari ya udini wengine mnaweza kuyaongeza. Lakini tuanze na hayo. Najua wengine ngewasilisha mada hii vizuri kuliko mimi, lakini tupokeeukweli wa ujumbe huu na tujadili.
NAOMBA KUWASILISHA
 
Back
Top Bottom