SoC01 Maamuzi yenye nguvu

Stories of Change - 2021 Competition

Musase Manoko

Member
Nov 18, 2013
7
0
Sipo hapa kukufurahisha, Hapana. Sipo hapa kukupa utajiri, hapana. Lakin nitahitaji mpaka kufikia mwisho nibadilishe mtazamo wako kwasababu mtazamo wako ndo adui wa kwanza wa mafanikio yako.

Tulia ukiwa peke yako, fumbua macho yako, fikiria nini kikwako katika maisha yako.

Najua unajiuliza mambo mengi sana mpaka sasa; thamani yako, dhumuni na umuhimu wako katika maisha haya unayoishi ni yapi!?

Ushawahi jiuliza kwanini jirani ni tajiri na wewe ni maskini au huyaelewi maisha yako, unajiona upo upo tu mpaka unakosa amani furaha na kibaya zaidi unaona miaka hairudi nyuma yenyewe inasonga mbele na hapo ndo unazidi kuchanganyikiwa.

Msukumo huu si mbaya kama unavyofikiria, utumie kubadilisha mtazamo wako sasa, ndugu yangu kuna mstari mwembamba sana unaotofautisha uchumi mdogo, uchumi wa kati na uchumi huru; kati ya mtu mmoja na mwingine, kuna watu ni wazito sana kufanya maamuzi na maamuzi ndio sehemu ambayo inaweza kubadilisha maisha yako nduvu yako ndio kati ya kila kitu.

Fikiria hili, upo sehemu gani katika kutosheleza mahitaji yako. Je, unazalisha!? Unasambaza!? au wewe ni mtumiaji tu wa bidhaa au huduma taarifa ni kwamba kama upo kwenye hili la mwisho ukwel ni kwamba umesimama katika mafanikio hutembei anza kubadilisha hapo.

Kama nchi kumekuwa kuna dhana kwamba, kuna baadhi ya makabila ndo wafanya biashara ambao wako mbele sana katika kusukuma uchumi wao binafsi na uchumi wa nchi, nomba tu nikwambie huo ni mtazamo tu! uliowekea na ambao umeendelea kuaminishwa kwa vizazi na vizazi, binafsi unatakiwa kuukataa mtazamo huo kwasababu biashara ni nia maamuzi haina uhusiano na ukabila, rangi, uraiya.

Habari njema ni kwamba sisi kama watanzania tuna nafasi kubwa ya kubadilisha uchumi wa mtu mmoja mmoja.

Katika sekta nne za uchumi sisi tupo kwenye sekta ya msingi sekta ya kwanza: Kutoa na kuazalisha malighafi pamoja na mazao katika mazingira asilia kabisa. Mfano kilimo, uchimbaji wa madini, uvuvi n.k

IMG-20210727-WA0009.jpg


Sitaenda katika sekta 3 zilizobaki ambazo tupo nyuma sana kama nchi na kibaya zaidi wananchi ndo hawana habari nazo kwasababu wengi wamebaki katika sekta ya msingi ya uchumi wakiziacha sekta 3 zilizobaki ambazo ndo uchumi wenyewe sasa, matokeo yake yamesababisha tuwe tegemezi katika bidhaa nyingi tunazotumia kutoka nje ya nchi, na hiyo yote ni kwasababu ya fikra tuliopandikizwa kwa mda mrefu sasa na maamuzi tunayoendelea kufanyiwa na mataifa makubwa kiuchumi.

Najua unajua na nakujuza sasa na kukazia, Mtanzania wewe si dhaifu! Jiamini, Amua sasa kukifanyia kazi kile unachokiamini na kukisimamia mpaka ukikamilishe na hapo ndo furaha ya kweli utaanza kuiona kwa sababu ni jambo lako.

Biashara haianzi kuwa kubwa na kusimama kwa pesa bali uanza kuwa kubwa kwa maamuzi utakayofanya ya biashara hiyo, hakuna uchawi katika hili ukishaamua kwa dhati ukafanya maamuzi ukaamini juu ya jambo unalolifanya utafanya na hapo ndo mchakato mzima utanza na mzunguko kuwepo hiyo ndio nguvu iliojificha ambayo wengi hawaijui achana na habari ya kesho acha na habari ya ntafanya, fanya sasa.

Anza biashara usithubutu, wewe fanya kama mmiliki anaejiamini, tengeneza mpango wako na uishi humo, sikatai kwamba haitakuwa rahisi lakini wewe pambana kuiboresha, kuwa mmbinafsi juu ya ukitendacho na kwasababu unakiamini ng'ang'ania hapo katika maendeleo yako na biashara yako, hakuna kukata tamaa.

Tuingie katika mzunguko wa biashara za uzalishaji watanzania wengi tuwe katika umiliki wa viwanda mbalimbali na sio biashara za kula bidhaa zilizozalishwa tiyari tena na viwanga vya nje ya mipaka yetu ya nchi.

Biashara hizi ni biashara za kuona mbali, ambazo waamuzi wakuu ni mimi, wewe na sisi kiujumla wetu, biashara hizi zitatufanya twende kwenye sekta ya 2 ya uchumi: Shughuli za kubadilisha malighafi hizi kuwa bidhaa kama kutumia pamba kutengeneza nguo.

Wewe ni kila kitu nchi hii inaitaji, Kama mzalendo najua bila uoga utafanyia maamuzi juu ya uchumi wako na uchumi wa Nchi yetu. Nakupenda Tanzania. Nakupenda Mtanzania mwenzangu.
IMG-20210726-WA0016.jpg
my

IMG-20210729-WA0005.jpg


images%20(1).jpg


images%20(2).jpg
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom