Maamuzi yangu...

Maamuzi yangu...

Flamegood

Senior Member
Joined
Oct 27, 2018
Posts
129
Reaction score
293
Habari wana JF

Baada ya harusi niligundua Mke wangu anadate na cameraman wa harusi yetu, hii ilikuwa ni baada kufuma messages (conservation) wakati tupo honeymoon alipokwenda kuoga, inaonekana walikuwa wananichora tukiwa high table.

Sikumwambia chochote japo iliniuma nikapotezea kwa kuwa maji nilishayavulia nguo nikajua maybe baada ya pale wataachana maana mwamba atakuwa kashaamini kuwa tupo serious ndio maana tumeoana. Baada ya mwezi mmoja nikagundua kuwa mke wangu ana mimba ya miezi 3 na sikuwahi kulala nae kabla ya honeymoon Ila kabla ya kugundua kuwa ana mimba ya miezi mitatu nilikuwa nikihisi tu kuwa mke wangu ana mimba kwa kuwa niliziona dalili mbalimbali sikutaka kumuuliza ila kwanini kwa haraka vile yaani mwezi tu mtu ana dalili konk vile ila nilipotezea kwa kuwa nilijua kila mimba ina stail yake ngoja nisubir akifikia kuniambia ataniambia.

Ndipo siku moja nikagundua kuwa kweli ana mimba na tena ni ya miezi mitatu najua mnajiuliza nilijuaje kuwa ana mimba ya miezi 3.

Niligundua hilo baada ya kufuma tena messages(conservatins) nyingine aliposahau cm yake mezani baada ya kwenda sokoni. Alikuwa akichat na yuleyule cameraman. Inaonekana mwanaume alikuwa akiulizia kuhusu mimba ile inaendeleaje na mbinu zao jinsi watakavyoniuzia mbuzi kwenye gunia.

Mwanamke aliporudi nilijikausha japo nilikuwa na hasira sana kiasi kwamba usiku wa siku ile baada ya mwanamke kulala nilikuwa mwenye mawazo sana na nakumbuka niliinua mkono juu nilitaka kumchoma kisu afie usingizini kwa kuwa nilikuwa na hasira mno ila niliweza kujizuia ndipo nikaamua kujitengenezea kitanzi nijinyongee sebleni usiku ule (ndio nilijiona mjinga kwa kuwa nilifikiri mke wangu ni muaminifu kwangu kabla ya ndoa kumbe alinizunguka na vipi kuhusu muda na gharama nilizozitumia kufanya harusi na kwanini hakutaka kuniambia ukweli na bado walipanga kunizunguka na cameraman)

Nilijiona sina hatia nikajionea huruma ikabidi nifanye maamuzi magumu ya haraka usiku ule niliandika talaka tatu zilizokuwa na maelezo yote na kuzituma kwa njia ya cm kwenda kwa wazazi wake nikavunja line kisha niliamua kumtoroka kiukweli nilimuachia kila kitu cha ndani nashukuru MUNGU kwa kuwa nyumba tuliyoishi ilikuwa sio ya gharama sana ni kama million 15 tu Vyumba viwili na Sebule ilikuwa jijini Arusha ila hati ninayo hadi sasa nakumbuka niliondoka na hati ya nyumba na nguo nilizozivaa pekee ilikuwa mwaka juzi 2018 mwezi wa 7 ndipo nikahamia Dar es Salaam ndipo mwaka 2019 nikabahatika kupata mke mwingine kipenzi changu mahabuba ambae baada ya kunizalia mtoto huyu nilie nae nilienda kuthibitisha kwa kumpima DNA nikagundua sijaibiwa na mimi na mke wangu mpya tunapendana sana na sasa tunatimiza miaka miwili ya ndoa yetu. Yule malaya hadi leo cjui anaendeleaje na cameraman wake.

Najua wengi mnajiuliza kwanini niliondoka na hati ya nyumba ila kwa leo sitowapa majibu ila niambieni je, nilifanya makosa kufanya maamuzi yale?
 
Rudi kachukue na ile nyumba unamuachia nani? Kwani umeacha mtoto wako pale?!!
 
Mkuu talaka anapewa mzazi?..kwani mzazi ndo uliemuoa?

Ilitakiwa umpe talaka yeye mwenyewe na ajue kosa alilofanya...Sasa umetoroka TU

Ila pole Sana mkuu...hongera kwa kupata mahabuba wako...Mpendane muelewane wenye Kijiba waulizane.
 
uliondoka na hati ili siku moja uje kumkomoa ila angalia usijekuta kauza hiyo nyumba kiutapeli akamuuzia mtu mwingine kesi ,wewe unarudi kwenda kuuza nyumba unakutana na mambo mengine mkuu .
 
Hayo ni maamuzi soft sana, mimi ningetia vitu vyake kwenye gari na yeye mwenyewe ningemfunga kamba kama mwizi au kifurushi na kumpeleka kwa cameraman wake ili waendelee na mapenzi yao.
 
uliondoka na hati ili siku moja uje kumkomoa ila angalia usijekuta kauza hiyo nyumba kiutapeli akamuuzia mtu mwingine kesi ,wewe unarudi kwenda kuuza nyumba unakutana na mambo mengine mkuu .
Hiyo nyumba itakuwa imeshauzwa zamani au lah imebaki tu panya na majoka yanachezamo ndani
 
Nyumba ya Million 15 + Vitu vya Ndani Roughly Million 5 Vyote Umeviacha !#

[emoji848][emoji848]Hivi inawezekana kweli !? Na hasira zote zile
 
Back
Top Bottom