Maamuzi ya Serikali kuhusu shamba la Utegi

Maamuzi ya Serikali kuhusu shamba la Utegi

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,523
Nianze kumshukuru kwa dhati kabisa Mhe. Rais wa Jamhuri wa Tanzania kwa kuwarudishia Wananchi wa Vijiji sita vinavyozunguka shamba la Utegi. Ndugu zangu mnyonge mnyongeni lakini haki ya mpeni. Asante sana Mhe. Rais.

Otieno Igogo alitamba kuwa wananchi wa Vijiji hivyo hawawezi kumfanya lolote na wala chochote. Alitamba sana kwenye Serikali ya awamu ya nne.

Wananchi wameendesha kesi siyo chini ya miaka 15 lakini dunia hii kila kitu kina mwisho. Ameamriwa kulipa fidia kwa Vijiji hivyo sita na pia kuilipa Serikali kwa maeneo ambayo anatakiwa kulipa.

Sasa hivi Vijiji hivyo vinasubiri utaratibu mpya wa Serikali juu kuendesha Shamba hilo. Asante sana mhe. Rais. Umedhihirisha kuwa wewe ni Rais wa wanyonge. Mungu akujalie sana.
 
Safi sana Mh Rais kwa kufanikisha hilo km kulikuwepo na hujuma
 
Back
Top Bottom